AFYA.com

AFYA.com Am a Doctor. Am a young motivator and am live to inspire other people. And also if you want to know

HATUA ZA KUPUNGUZA UZITO BAADA YA KUJIFUNGUA.Kupunguza uzito baada ya kujifungua ni jambo gumu na linaloleta stress sana...
04/10/2024

HATUA ZA KUPUNGUZA UZITO BAADA YA KUJIFUNGUA.

Kupunguza uzito baada ya kujifungua ni jambo gumu na linaloleta stress sana kwa wanawake wengi. Kila mmoja wetu anapenda kuwa na uzito wa kawaida ili kufurahia maisha na kutoogopa kuvaa nguo yoyote.

Uzito mkubwa na kitambi hasa baada ya kuzaa unakera sana na kukupunguzuia urembo wako. Najua unahitaji kupunguza uzito na kurudi kwenye shape yako ya zamani kabla hujashika mimba.

Usiwe na hofu haupo peke yako, tumefanya utafiti na kukuletea maelezo ya kuzingatia ili upunguze uzito na uanze kufurahia maisha k**a zamani.

Wanawake Huongezeka unene wakati wa Ujauzito
Zaidi ya nusu wya wanawake wenye mimba huongezeka uzito zaidi kuliko kiwango kinachohitajika wakati wa ujauzito. Uzito mkubwa na kitambi unasababisha madhara zaidi kwa mjamzito ikiwemo

hatari ya kuugua kisukari na presha
kupata matatizo wakati wa kujifungua na
kifafa cha mimba
Hatua za kufuata ili upunguze Uzito baada ya kujifungua

1.Jiwekee malengo
Unataka kupungua kilo ngapi baada ya muda gani? lazima uandike kwenye daftari ama notebok yako, bila hivyo ni ngumu kufikia mafanikio. Mfano unataka kupungua kilo 20 ndani ya miezi mi4, maana yake ukivunja vunja malengo yako unatakiwa upungue kilo 5 kila mwezi.

Ukishajiwekea malengo, andika na mikakati ya kuchukua ili kufikia lengo la kila mwezi, kisha anza mara moja kutimiza.

2.Usijinyime kula baada ya kujifungua
Wakati huu ambao mtoto wako anahitaji zaidi maziwa ya mama, usinjinyime kula. Ukifanya hivo utamkosesha mtoto virutibishi vya muhimu. Badala yake chagua ule vitu gani na usile vitu gani. Punguza kula vyakula vya wanga na sukari, badala yake kula zaidi vyakula vyenye protini na mafuta mazuri.

3.Mnyonyeshe mtoto inavotakiwa
Shirika la afya duniani linapendekeza mtoto anyonye kwa miezi 6 bila kupewa chakula kingine chochote. Kunyonyesha mtoto kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu itakusaidia sana afya yako na ya mtoto pia kwa kumpa mtoto virutubishi vya kutosha.

Virutibishi hivi husaidia kuimarisha kinga ya mtoto dhidi ya maambukizi ya fangasi na bakteria, kupunguza hatari ya mtoto kuugua magonjwa ya utotoni k**a pumu na kupunguza hatari ya mama kupata saratani ya matiti, kisukari, presha na uzito mkubwa

Miezi mitatu ya mwanzo ya kunyonyesha unaweza usione mabadiliko katika kupunguza uzito wako, usikate tamaa endelea kunyonyesha zaidi utaona matokeo.

4.Kula kwa wingi vyakula vyenye kambakamba(fiber)
Kwenye shopping yako ongeza vyakula vya nafaka ambavyo havijakobolewa na mboga za majani kwa wingi. Vyakula vyenye kambakamba kwa wingi vinapunguza kasi ya uchakataji chakula tumboni na hivo kukufanya usiwe mtu wa kula kula kila mara.

5.Ongeza na vyakula vya protini kwa wingi baada ya kujifungua
Vyakula vya protini vinaimarisha shughuli za mwili, kupunguza njaa na hivo kupunguza kiwango cha chakula unachotakiwa kula katika siku.

Tafiti zinasema kwamba mwili unatumia nguvu kubwa zaidi kuchakata protini kuliko aina zingine za chakula. Kwa mantiki hiyo mwili utachoma zaidi mafuta yaliyohifadhiwa mwili kupata nishati ya kuchakata chakula, na kupelekea upungue uzito bila kutumia nguvu nyingi.

Vyanzo vya protini ni pamoja na nyama ya ngombe au mbuzi, nyama ya kuku, mayai, samaki , karanga, mbegu na maziwa.

6.Epuka Sukari iliyoongezwa kwenye vinywaji na vyakula vya kusindikwa
Sukari iliyoongwezwa kwenye vyakula unavyovipenda zaidi k**a baga, mandazi, mikate, sosage,pombe, icecream , keki na energy drinks,vinakufanya uendelee kunenepa zaidi. Epuka vyakula hivi na uanze kula chakula ulichopika wewe nyumbani.

Usitumie tena vyakula vya kwenye makopo au pakiti. Nenda mwenyewe sokoni fanya shopping, rudi nyumabani pika chakula chako upike ule.

Weka ratiba ya kufanya mazoezi
Kabla ya kuanza mazoezi ongea na daktari ni muda gani unafaa kuanza kufanya mazoezi hasa k**a ulijifungua kwa upasuaji. Mazoezi yatakusaidia kuchoma mafuta mengi zaidi yaliyohifadhiwa mwilini.

8.Pata usingizi wa kutosha baada ya kujifungua
Kila siku pata muda mzuri wa kulala usiku masaa 8 au 9. Itakusaidia kuweka sawa homoni zako ili uweze kupungua kiurahisi. Baada ya kujifungua ongeza wafanyakazi wa nyumbani kukusaidia kubeba mtoto na kufua ili muda mwingi upate kupumzika.

  CHA KUVUJA DAMU MAPEMA KATIKA UJAUZITO NI NINI?Chanzo cha kuvuja damu mapema katika ujauzito ni nini?Kuvuja damu kabla...
27/03/2024

CHA KUVUJA DAMU MAPEMA KATIKA UJAUZITO NI NINI?

Chanzo cha kuvuja damu mapema katika ujauzito ni nini?
Kuvuja damu kabla ya wiki 28 za ujauzito hudhaniwa kuwa ni kuvuja damu mapema katika ujauzito. Ikitokea baada ya wiki 28, huitwa utokaji wa damu wa baadaye katika ujauzito.
Mgawanyo huu wa wiki 28 umezingatia uwezekano wa kuishi ikiwa mtoto atazaliwa kabla ya tarehe iliyotarajiwa katika wiki 28,
Matumaini ya kuishi kabla ya wiki 28 ni madogo sana katika nchi nyingi zinazoendelea maana kuna upungufu wa vifaa vya afya vya utunzaji maalum kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

Siku hizi nchi zingine zimepunguza mgawanyo huu hadi wiki 20 kwa sababu ya utunzaji ulioimarishwa na teknolojia inayotolewa na mfumo wao wa afya.

cha kuvuja Damu Wakati wa Ujauzito
Visababishi vikuu vya kuvuja damu mapema katika ujauzito ni ;

--utokaji wa mimba au mimba kutishia kutoka.
--mimba iliyotungwa nje ya kizazi au uterasi (hapa mtoto hujishikiza na kukua nje ya kizazi au uterasi),

-Uvimbe kwenye kizazi

-Kondo la nyuma au placenta kuachia ambapo kitaalamu huitwa (placenta abruption)

-Kondo la nyuma kushuka chini hali inayojulikana k**a Placenta previa

-Mama mjamzito kupigwa au kuanguka na kupelekea mshtuko kwenye tumbo la uzazi n.k

NB; Ukiona unavuja damu hakikisha unapata msaada mapema kutoka kwa Wataalam wa afya

Tatizo la Uke Kuwa na Maji: Sababu, Dalili na Matibabu.Tatizo la uke kuwa na maji ni mojawapo ya matatizo yanayowakumba ...
28/04/2023

Tatizo la Uke Kuwa na Maji: Sababu, Dalili na Matibabu.

Tatizo la uke kuwa na maji ni mojawapo ya matatizo yanayowakumba wanawake wengi. Hata hivyo, kuna wasiwasi mkubwa linapokuja suala la kuzungumzia tatizo hili.
Wanawake wengi wanajisikia vibaya kuzungumza kuhusu tatizo hili kwa sababu ya aibu. Kwa bahati mbaya, kutotibu tatizo hili kunaweza kusababisha shida kubwa kiafya.

Makala hii inalenga kutoa ufahamu wa kina kuhusu tatizo la uke kuwa na maji, ikiwa ni pamoja na sababu, dalili, na matibabu.

Sababu za Tatizo la Uke Kuwa na Maji
Tatizo la uke kuwa na maji linaweza kusababishwa na sababu tofauti, ikiwa ni pamoja na:

1. Maambukizi ya Ukeni
Maambukizi ya ukeni ni sababu kuu ya tatizo la uke kuwa na maji.

Bakteria wanaoishi kwenye uke wanaweza kusababisha maambukizi. Maambukizi haya huathiri usawa wa bakteria wanaoishi kwenye uke na kusababisha kuongezeka kwa ute wa ukeni.

Hata hivo katika hali ya kawaida,uke unaweza kuwa na maji ambayo ni meupe na ambayo hayana harufu yoyote,

maji maji haya yanaweza kuwa meupe, kubadilika na kuwa na weupe k**a wa yai,kuvutika na mazito kidogo kulingana na mabadiliko mbali mbali kwenye mzunguko wa hedhi,
ngawa, endapo maji haya yakabadilika gafla na kuanza kuwa na harufu,rangi au muonekano usiyowakawaida,hii huweza kuashiria uwepo wa maambukizi mbali mbali, hasa pale ambapo yameambatana na matatizo mengine k**a vile miwasho ukeni,uke kuvimba,kupata maumivu n.k

Baadhi ya maambukizi ambayo huweza kuhusika ni Pamoja na;

bacterial vaginosis
Fangasi sehemu za siri-candidiasis
trichomoniasis
chlamydia
Kisonono-gonorrhea
ge***al herpes
Hakikisha unapata vipimo na matibabu endapo unapata matatizo k**a nilivyoeleza hapa juu.

2. Kutumia Dawa za Kuzuia Mimba
Baadhi ya aina za dawa za kuzuia mimba zinaweza kusababisha tatizo la uke kuwa na maji.

Dawa hizi hupunguza kiwango cha homoni za uzazi kwenye mwili wa mwanamke.

Hii inaweza kusababisha mabadiliko kwenye uke na kusababisha kuongezeka kwa ute wa ukeni.

3.Mabadiliko ya Hormones
Mabadiliko ya homoni mwilini yanaweza kusababisha tatizo la uke kuwa na maji.

Hii inaweza kutokea wakati wa hedhi, wakati wa ujauzito, au wakati wa kuingia kwenye kipindi cha ukomo wa hedhi-menopause.

Dalili za Tatizo la Uke Kuwa na Maji
Kuna dalili kadhaa ambazo zinaweza kuashiria kuwa una tatizo la uke kuwa na maji, ikiwa ni pamoja na:

– Uchafu Mweupe au Kijivu kutoka ukeni
Uchafu kutoka kwenye uke ambao ni mweupe au kijivu ni dalili kuu ya tatizo la uke kuwa na maji.

– Kuvimba kwa Uke
Kuvimba kwa uke ni dalili nyingine ya tatizo la uke kuwa na maji.

Hii inaweza kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au hata wakati wa kukojoa.

– Kuhisi Kuwashwa na Kuumwa
Kuwasha na kuuma kwenye sehemu za siri ni dalili nyingine ya tatizo la uke kuwa na maji. Hii inaweza kusababisha wasiwasi na kufanya mambo yawe magumu.

Matibabu ya Tatizo la Uke Kuwa na Maji
Kuna njia kadhaa za matibabu ya tatizo la uke kuwa na maji, ikiwa ni pamoja na:

✓ Matumizi ya Antibiotiki
Ikiwa tatizo la uke kuwa na maji linasababishwa na maambukizi ya ukeni yanayotokana na vimelea k**a bacteria, daktari anaweza kukuagiza dawa za antibiotic n.k.

✓ Dawa za Kurekebisha hali ya Uke
Dawa zinazorekebisha hali ya ukeni zinaweza kutumika kupunguza kiwango cha maji kwenye uke. Dawa hizi zinaweza kuwa kwenye mfumo wa vidonge, suppositories, au gel.

✓ Kuhakikisha Usafi wa Uke
Ni muhimu kuhakikisha usafi wa uke ili kuzuia maambukizi ya ukeni. Hii inaweza kujumuisha kuosha kwa maji safi na sabuni laini, kubadilisha taulo za hedhi mara kwa mara, na kutumia kinga wakati wa tendo la ndoa.

FAQs
Je, tatizo la uke kuwa na maji linaweza kuwa hatari kwa afya yangu?
Ndio, tatizo la uke kuwa na maji linaweza kuwa hatari kwa afya yako. Ikiwa halitotibiwa, linaweza kusababisha maambukizi zaidi ya magonjwa ukeni au shida zingine za kiafya.

Je, matibabu ya tatizo la uke kuwa na maji ni salama?
Ndio, matibabu ya tatizo la uke kuwa na maji ni salama. Ni muhimu kushauriana na daktari kabla ya kuanza matibabu yoyote.

Je, ninaweza kuzuia tatizo la uke kuwa na maji?
Ndiyo, kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuzuia tatizo la uke kuwa na maji, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usafi wa uke, kuvaa nguo za ndani za pamba, na kutumia kinga wakati wa tendo la ndoa.

Conclusion(Hitimisho)
Tatizo la uke kuwa na maji ni jambo ambalo linaweza kumfanya mwanamke ajisikie aibu na kuvuruga maisha yake ya kila siku.

Hata hivyo, kuna njia nyingi za matibabu na kuzuia tatizo hili. Ni muhimu kuzungumza na daktari wako ikiwa una wasiwasi wowote kuhusu afya yako ya ukeni.

Kumbuka kwamba kuzingatia usafi wa uke ni muhimu katika kuzuia tatizo la uke kuwa na maji. Pia, unapaswa kuvaa nguo za ndani za pamba na kutumia kinga wakati wa tendo la ndoa.

Ikiwa una dalili za tatizo la uke kuwa na maji, unapaswa kutafuta ushauri wa kitaalam kutoka kwa daktari wako. Daktari wako anaweza kufanya vipimo na kugundua sababu ya tatizo hilo na kukusaidia kupata matibabu sahihi.

Kumbuka pia kujiepusha na matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari,kwani kunaweza kuwa hatari kwa afya yako. Ni muhimu kuzungumza na daktari wako kabla ya kuanza matibabu yoyote.

Kwa hiyo, endapo utakuwa na dalili za tatizo la uke kuwa na maji ni muhimu kuwasiliana na daktari wako mapema ili kugundua chanzo na kutibu tatizo hilo kwa wakati.

Hii itasaidia kuzuia athari kubwa za kiafya na kumwezesha mwanamke kuendelea na shughuli zake za kila siku kwa amani na utulivu.

JINSI YA KUONGEZA MBEGU ZA KIUME(JINSI YA KUONGEZA MANII)Hizi hapa ni baadhi ya tips za kuwasaidia wanaume wenye tatizo ...
28/04/2023

JINSI YA KUONGEZA MBEGU ZA KIUME(JINSI YA KUONGEZA MANII)

Hizi hapa ni baadhi ya tips za kuwasaidia wanaume wenye tatizo la Mbegu chache au kwa kitaalam hujulikana k**a Low s***m count. Tips hizi zitakusaidia kuongeza mbegu za kiume au manii

1. Kupunguza uzito wa mwili, Watu wengi hawajui kwamba, k**a una tatizo la uzito kuwa mkubwa(overweight/obesity) huweza kuathiri mpaka mfumo wako wa uzazi,

Baadhi ya tafiti zinaonyesha mtu mwenye shida ya uzito mkubwa akipunguza uzito wake husaidia sana kuboresha afya ya mbegu za kiume(overall s***m health) ikiwemo kuongeza Semen Volume,concentration pamoja na mobility,Hivo hakikisha unapunguza uzito wako wa mwili k**a una shida hii ya uzito mkubwa(Overweight).

2. Fanya mazoezi mbali mbali ya mwili, mbali na faida lukuki za mazoezi ikiwemo kuimarisha mzunguko wa damu mwilini, pia mazoezi husaidia sana kwenye afya ya uzazi ikiwemo swala la mbegu za kiume,

Hivo hakikisha unafanya mazoezi ya mwili angalau kwa dakika 30 au nusu saa kila siku kwa ajili ya afya ya mwili pamoja na afya ya uzazi.

3. Hakikisha unapata Vitamins D,C,E Pamoja na madini ya Calcium vyote hivi ni muhimu kwenye afya ya uzazi,Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba kwa mwanaume ambaye anapata 1,000mg za Vitamin C kila siku husaidia sana kuongeza s***m concentration pamoja na mobility hivo huongeza uwezo wa mwanaume kutungisha mimba,

Na utafiti huo unazidi kuonyesha kwamba, wanaume ambao hupata kiwango kidogo cha Vitamin D wanakuwa na uwezo mdogo sana wa kutungisha mimba.

4. Epuka matumizi ya Pombe kupita kiasi, Miongoni mwa vitu ambavyo huchangia uwepo wa tatizo la mbegu chache kwa wanaume au Low s***m count ni pamoja na matumizi ya Pombe kupita kiasi

5. Epuka uvutaji wa sigara ikiwemo tumbaku,ugoro, au vilevyi vingine k**a vile Coccaine n.k

6. Jikinge ukiwa kwenye mazingira ya kemikali, heavy metals,solvents,Au dawa za kuua wadudu(pesticides) kwani vyote hivi huweza kuathiri s***ms.

7. Vaa nguo za ndani ambazo hazibani sana na zenye material ya pamba(cotton boxers) ili kuruhusu hewa kupita na kuepuka joto zaidi,

Kumbuka moja ya vitu muhimu kwenye utengenezaji wa mbegu za kiume ni pamoja na joto(temperature),

Hivo uwepo wa korodani nje ni mahususi kabsa ili kuwa na joto kiasi(moderared temperature) ambalo litasaidia katika utengenezaji wa mbegu za kiume.

8. Pata muda wa kutosha wa kupumzika na kulala, hakikisha unaondoa Stress au msongo wa mawazo,maana vyote hivi huweza kuathiri mpaka uzalishwaji wa Mbegu za kiume

9. Epuka matumizi ya dawa hovio,Tumia dawa hizi kwa uangalifu na maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya;

– Baadhi ya antibiotics,Anti-Inflammatories,Antipyschotics,Antidepressants,Anabolic steroids,methadone n.k

10. Epuka matumizi ya madawa k**a Vumbi la Congo n.k na tumia dawa k**a Vi**ra kwa maelekezo maalumu kutoka kwa wataalam wa afya.

Pia tafiti zinaonyesha Dawa za asili ambazo hujulikana k**a ashwagandha au Indian Ginsey,zimekuwa zikitumika kwa muda mrefu na kusaidia sana wanaume wengi wenye shida hii. Japo faida na hasara za matumizi yake huhitaji utafiti zaidi(Research).

11. Hakikisha unakula vyakula ambazo vitakupa health fat k**a vile;Polyunsaturated fats ambayo ni muhimu sana kwa afya ya mbegu za kiume hasa kwenye utengenezaji wa s***m membrane,

aina hii ya Fats ina omega-3 and omega-6.

Epuka matumizi ya chakula ambayo yatakupa unhealthful fat,

Utafiti huu ambao ulifanyika Mwaka 2014 Nchini Spanish kwa wanaume 209 wenye umri wa miaka 18–23 ulionyesha kwamba,
Wanaume hao walikuwa wanatumia kiwango kikubwa cha trans fatty acids na wakati huo huo tatizo la Low s***m count lilionekana kwao.

12. Hakikisha unapata madini ya ZINC pamoja na FOLATE, Bila shaka umekuwa ukisikia sana habari za Zinc kwenye swala la mbegu za kiume, yeah ni kweli Zinc ni muhimu sana kwenye mbegu za kiume ikiwemo faida ya kuongezea mwendo mbegu za kiume yaani mobility.

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba ukipata Zinc pamoja na Folate kwa kiwango kinachotakiwa mwilini hata afya ya mbegu za kiume(Overall s***m health) ikiwemo concentration pamoja na Count huongezeka sana.

KUMBUKA; Ni salama na Unaweza kutumia supplements ambazo zina virutubisho vinavyotakiwa k**a vile Vitamins,Madini(Minerals),antioxidants n.k, ila Mwili hauwezi kufanya ufyonzwaji kwa urahisi zaidi k**a mtu ambaye anakula vyakula vyenye virutubisho hivi.

Hivo badala ya kukimbilia Supplements, kula vyakula vyenye virutubisho hivi itasaidia mwili kufanya ufyonzwaji kwa urahisi zaidi na kwa haraka,

“The best way to increase s***m count naturally may be to increase the consumption of foods high in s***m-friendly nutrients, such as vitamin C, antioxidants, and polyunsaturated fats.Than taking Supplements directly”.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584..afyaclass
AFYA.com

TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME,CHANZO,DALILI NA TIBAatizo la upungufu wa nguvu za kiume huweza kuhusisha; Uume kus...
28/04/2023

TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME,CHANZO,DALILI NA TIBA

atizo la upungufu wa nguvu za kiume huweza kuhusisha; Uume kushindwa kabsa kusimama, uume kutokusimama kwa muda mrefu, Kukosa nguvu ya kuanza au kuendelea na tendo n.k

hali ambazo hupelekea mwanaume kushindwa kumridhisha mwenza wake ambaye anashiriki naye tendo la ndoa kwa wakati huo.

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Zipo sababu nyingi sana ambazo huchangia wanaume kuwa na tatizo hili la Kukosa nguvu za kiume, na baadhi ya sababu hizo ni pamoja na;

• Working hours:Whatsapp Link,Bofya hapa
– Mtindo mzima wa maisha kwa mwanaume ikiwemo ulaji wake wa kila siku

– Mwanaume kuwa na magonjwa ya moyo ambayo huweza kuathiri usafirishaji wa damu mwilini

– Uwepo wa kiwango kikubwa cha lehemu yaani High cholesterol unaweza kusababisha tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri(erectile dysfunction)

– Tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha hormones za kiume yaani Low testosterone Level

– Tatizo la Clogged blood vessels (atherosclerosis)

– Ugonjwa wa presha ya kupanda yaani High blood pressure huweza kuleta effect mpaka kwenye mfumo wa uzazi

– Ugonjwa wa kisukari(Diabetes),huweza kuathiri uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa ikiwemo tatizo hili la uume kushindwa kusimama vizuri yaani erectile dysfunction

– Tatizo la Uzito kuwa mkubwa yaani Overweight/Obesity, Mwanaume mwenye uzito mkubwa sana,Bonge n.k anaweza kushindwa kufanya vizuri hata kwenye tendo la ndoa.

Hivo unashauriwa kuhakikisha unazuia tatizo hili la uzito kuwa mkubwa/kupita kiasi.

– Tatizo la Metabolic syndrome, ambalo huhisisha vitu hivi kwa ujumla wake; Presha kuwa kubwa zaidi,Level ya Insulin kuwa kubwa sana,Mafuta ya mwili(Body fat) kuzidi pamoja na kiwango cha cholestrol kuwa kikubwa zaidi.

– Matatizo mengine k**a vile;Parkinson’s disease,Multiple sclerosis n.k pia huweza kuleta athari kwenye mfumo wa uzazi

– Uvutaji wa Sigara ikiwemo matumizi ya Tumbaku(Tobacco)

– Matumizi ya baadhi ya Dawa k**a vile dawa jamii ya antidepressants, antihistamines,dawa za kutibu presha(high blood pressure), maumivu au matatizo ya tezi dume

– Unywaji wa Pombe kupita kiasi pamoja na aina nyingine za ulevi au madawa ya kulevyia

– Ugonjwa wa Peyronie’s disease, ugonjwa huu huhusisha kutokea na kuendelea kwa kovu(Scar tissues) ndani ya Uume

– Tatizo la kukua kwa tezi dume(enlarged prostate),kansa/Saratani ya Tezi Dume(prostate cancer) pamoja na Matibabu yake

– Mwanaume kuumia au kupata majeraha kwenye maeneo ya via vyake vya uzazi ikiwemo kwenye nyonga pamoja na uti wa mgongo

– Mwanaume kufanyiwa upasuaji kwenye eneo la nyonga(Pelvic) au uti wa mgongo(Spinal cord)

– Tatizo la msongo wa mawazo,hofu,wasi wasi pamoja na matatizo mengine ambayo huhusisha afya ya akili(mental health problems),Vitu hivi huweza kuleta athari mpaka kwenye uwezo wako wa kufanya tendo la ndoa.

– Migogoro ya kila mara kwenye mahusiano yako ambayo pia huweza kuleta tatizo la msongo wa mawazo au stress,wasi wasi,hofu n.k

– Pia tafiti zinaonyesha kadri Mwanaume anavyokuwa na umri mkubwa(mzee) ndivo na nguvu zake za Kiume huendelea kupungua sana ikiwemo uwezo wa uume kusimama vizuri na kwa muda mrefu.

– Baadhi ya matatibu k**a vile;Upasuaji wa Tezi Dume(prostate surgery) au huduma ya mionzi(radiation treatment) kwa wagonjwa wa kansa pia huweza kuathiri uwezo wa tendo kwa mwanaume

– Pamoja na Sababu zingine…

DALILI ZA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI PAMOJA NA;

• Uume kushindwa kusimama kabsa

• Uume kutokusimama vizuri

• Uume kusimama ila sio kwa muda mrefu

• Mwanaume kushindwa kurudia tendo, goli moja chali hawezi tena kurudia tendo

• Mwanaume kuwahi kufika kileleni na kushindwa kabsa kuendelea

• Kukosa kabsa hisia au hamu ya kufanya tendo la ndoa n.k

MADHARA YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI PAMOJA NA;

✓ Mwanaume kushindwa kumridhisha mwenza wake wakati wa tendo la ndoa

✓ Kuongeza wasi wasi,woga na hofu kubwa ya kufanya mapenzi kwa Mwanaume

✓ Mwanaume kutokujiamini tena

✓ Mwanaume kukosa kabsa hamu ya kufanya tendo la ndoa

✓ Kuanza migogoro kwenye mahusiano au ndoa,kusalitiana n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584..afyaclass.

Chanzo cha Uume Kulegea au Kusinyaa,dalili na Tiba yakeSHIDA YA UUME KUSHINDWA KUSIMAMA NA KUFANYA KAZI VIZURI WAKATI WA...
28/04/2023

Chanzo cha Uume Kulegea au Kusinyaa,dalili na Tiba yake

SHIDA YA UUME KUSHINDWA KUSIMAMA NA KUFANYA KAZI VIZURI WAKATI WA TENDO LA NDOA. (ERECTILE DYSFUNCTION).

Kutokana na Mfumo wa maisha yetu,kazi tunazofanya,vyakula tunavyokula au mtindo wa maisha kwa ujumla, tunajikuta kupata madhara mbali mbali katika miili yetu pasipo kujua sababu hasa ni ipi.
Tatizo hili la uume kushindwa kusimama na kufanya kazi vizuri,huwatokea wanaume wengi kwa hivi sasa, na kusababisha madhara makubwa yakiwemo ya mahusiano au Ndoa kuvunjika.

JE SABABU ZA TATIZO HILI NI ZIPI?

✓ Uchovu mzito wa mwili kutokana na shuhuli nyingi za Siku nzima

✓ Kuwa na shida ya msongo wa mawazo au Stress huweza kusababisha hali hii

✓ Kutawaliwa na wasiwasi pamoja na hofu kubwa wakati wa tendo la Ndoa

✓ Matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na Uvutaji wa Sigara

✓ Kuwa na umri mkubwa

✓ Ukiwa unatumia baadhi ya Dawa flani

✓ Kuwa na shida ya uzito kupita kiasi au Unene huweza pia kuchangia hali hii

✓ Kuwa na historia ya kupata tatizo katika sehemu za siri siku za nyuma

✓ Kuwa magonjwa mbali mbali k**a magonjwa ya moyo, presha au kisukari.

DALILI ZA TATIZO HILI LA ERECTILE DYSFUNCTION

– Hamu ya tendo la Ndoa kupote kabsa au kukosa hisia za kufanya mapenzi

– Kupata wasiwasi kabla ya kuanza kufanya mapenzi kuhusu kumridhisha mwenzako

– Hali ya uume kusinyaa mapema

– Hali ya uume kushindwa kusimama kabsa

– Uume kunyong’onyea wakati wa tendo la ndoa

– N.k

TIBA YA TATIZO HILI

Mgonjwa atatibiwa baada ya chanzo cha tatizo kujulikana hivo matibabu yake yatahusu chanzo cha tatizo lake,ambapo kwa ujumla wake, Mgonjwa anaweza kupewa ushauri wa kumsaidia kukaa sawa, mtindo wa maisha kuubadilisha ikiwemo vyakula,kazi n.k Pamoja na dawa k**a shida itahitaji dawa pia.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584. afyaclass
by dr andembwisye wa afya.com

Kutokwa na damu chache au tone la damu kabla ya hedhi kwa ujumla inaweza kuwa ishara ya mapema ya ujauzito (Implantation...
17/09/2022

Kutokwa na damu chache au tone la damu kabla ya hedhi kwa ujumla inaweza kuwa ishara ya mapema ya ujauzito (Implantation bleeding) au kutokana na mabadiliko ya homoni, au hali nyingine ya kiafya.
Kutokwa na damu kidogo ukeni ambayo hutokea nje ya kipindi cha kawaida cha hedhi inachukuliwa kuwa ni kutokwa na damu isiyo ya kawaida ukeni.

MADHARA AMBAYO UTAWEZA KUYAPATA KWA KUNYONYA SEHEMU ZA SIRI.Kutokana na kukua kwa teknolojia kunyonya sehemu za siri kum...
01/05/2022

MADHARA AMBAYO UTAWEZA KUYAPATA KWA KUNYONYA SEHEMU ZA SIRI.

Kutokana na kukua kwa teknolojia kunyonya sehemu za siri kumekua jambo la kawaida leo Dr msua nitazungumzia madhara ambayo unaweza kuyapata kwa kufanya hivyo.

Yapo madhara ambayo unaweza kuyapata kwa muda mmfupi na kuna madhara ambayo unaweza kuyapata baada ya muda
Magonjwa ambayo unaweza kuyapata ni yafuatayo:

1.HPV hawa ni virusi ambao husababisha kansa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kansa ya koo,kansa ya shingo kizazi ,kansa ya uume,kwa kufanya hivyo hurahisisha kuambukizwa virusi hivyo aina ya HPV.

2.Kisonono na kaswende:Kwa hali ya kawaida magonjwa haya hua ni ya sehem za siri tu lakini kwa kunyonya sehemu za siri waweza sababisha kuhamisha wadudu wasabishao magonjwa hayo

3.Magonjwa ambayo pia yaweza kuambukizwa kwa kunyonya sehemu za siri ni k**a:1.VVU
2.Virusi vya homa ya ini
3.Klamidia.
Imeandaliwa na Kutolewa na Dr Andebwisye
endela kunifuatilia.
insta @ koreanswahiliman.
Facebook .com

USITHUBUTU KUTUMIA VIDONGE AMA SINDANO ZA UZAZI WA MPANGO K**A UNA MAMBO HAYA.....1.Kama ni mjamzito2.Historia ya ugonjw...
20/04/2022

USITHUBUTU KUTUMIA VIDONGE AMA SINDANO ZA UZAZI WA MPANGO K**A UNA MAMBO HAYA.....

1.Kama ni mjamzito

2.Historia ya ugonjwa wa saratani ya in i(hepatocellurar carcinoma) ama manjano

3.Saratani ya matiti (breast cancer)

4.shinikizo la damu (hypertension)

5. historia ya maumivu makali ya kichwa.

6.Saratani ya mfuko wa uzazi.(uterine tumor)

k**a una mambo haya sita niliyoyaorodhesha kabla hujatumia dawa za uzazi wa mpango fika kituo cha afya kwanza kwa uchunguzi zaidi.

By Dr andembwisye.

MWANAMKE anaweza akapoteza mimba tatu mfatano au zaidi ya tatu ''Habitual abortion'', Kila akibeba mimba inatoka (recurr...
14/04/2022

MWANAMKE anaweza akapoteza mimba tatu mfatano au zaidi ya tatu ''Habitual abortion'', Kila akibeba mimba inatoka (recurrent pregnancy loss).

Hali hii inaweza kupelekea mwanamke kupoteza uwezo wake wa kushika mimba kwa siku za baadae.

Kuna sababu nyingi zinazopelekea mimba kutoka mara kwa mara, moja wapo ni kulegea kwa shingo ya kizazi na kushindwa kuhimili uzito wa mtoto (Cervical incompetence).

Sababu nyingine ni kutoendana kwa makundi ya damu kati ya mama, baba na kiumbe kilichoko tumboni.

Uliza chochote kuhusu mama mjamzito kwa kututumia ujumbe kupitia messenger kwa kubofya hapa m.me/occdoctors

Address

Seoul

Telephone

0759557506

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AFYA.com posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to AFYA.com:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram

Category