15/06/2023
UHUSIANO KATI YA IDADI YA MILO KITAMBI, UZITO MKUBWA,KISUKARI NA MARADHI LISHE MENGINE
Nimekuwa nikirudia sentensi zangu kila siku na sitachoka kurudia kwamba endapo hadi leo hii bado unafikiria kukiondoa kitambi kwa njia ambazo tumekuwa tukishauliwa kila siku, mfano fanya mazoezi, punguza kula na epuka vyakula vya mafuta basi ninaweza kukuweka kundi la watu wasiotambua thamani ya afya zao. Maana ni ujinga mkubwa kuendelea kukumbatia na kutekeleza kitu ambacho hakikupi na haitatokea kikupe matunda na hakijawahi kutoa matunda yoyote na hata anayekushauri hayo anajua hayana msaada wowote kwako (Anatekeleza wajibu wake k**a mshauri anajua utakuja kumwambia hukufanikiwa kwa lolote).
Mimi najua kwamba k**a mtu anaweza kutoa ushauri kwa watu maana yake ushauri huo hata kwake una msaada mkubwa sana. Mimi naelewa ingekuwa tatizo la kitambi uzito mkubwa na maradhi mengine ya lishe yanatibiwa kwa ushauri huu wa kila siku basi tusingefika hapa kiafya. Na kitu pekee binadamu ambacho umebakiwa k**a silaha na mlinzi wa afya yako ni kutambua kwamba afya yako ipo mikononi mwako wewe ndiye mwenye mamlaka ya kuendelea kuibomoa au kuijenga.
KWANZA: Niliuzwa swali na rafiki yangu daktari kwamba sasa Dr Banda hebu niambie kwa mtizamo wako unataka kuniambia nini ambacho kinasababisha kitambi,uzito mkubwa na maradhi mengine k**a hukubaliani kwamba Ulaji kupindukia,kutofanya mazoezi na ulaji wa vyakula vya mafuta kunasababisha kitambi? Na matokeo yake juzi nimesoma Makala yako inasema kutokuwa na uwezo wa kufanya mazoezi na ulaji wa vyakula kupindukia ni dalili za kitambi na sio visababishi vya kitambi? Sikukuelewa kabisa unapingana na elimu ya kisayansi hapa duniani na niliyosoma chuo kikuu takribani miaka 6.
Kwanza huwa napenda kusikitika sana kwa kutumia miaka 6 hadi sasa kusoma aina kuu tatu za ushauri ambao ni punguza kula, fanya mazoezi na epuka mafuta kwamba ndio nguzo kubwa ya maradhi ya kisukari,kitambi nk maana sikuwahi hata siku moja kupata ushuhuda kwa aina hio ya ushauri ndio maana nikawa najiuliza ni daktari gani nilivyo mpumbavu na mkosa maarifa asiyebadirika k**a mimi kuendelea kumshauri mtu ushauri ambao hauleti matunda! Ndipo nilipofikia mwafaka kwamba, siwezi kuendelea kutimiza kile nilichojifunza kukipeleka moja kwa moja kwa jamii maana hakina matunda yoyote. Kwa sababu nilikuwa na msukumo wa ajabu kuhakikisha kila mtanzania,kila mwanadamu anaishi bila kitambi ndipo nikaanza kuangalia wanasayansi wangapi nao wameshagundua “Kwamba ushauri wa namna hii hauna matunda yeyote tofauti ya kuitekeleza elimu uliyoipata bila kuifanyia uchunguzi na kuchuja” Nilikuja kugundua kwamba sayansi ya lishe sasa imepiga hatua na nilichokuja kugundua ni kwamba Kitengo hiki kimeshabadilishiwa taswila kwa maslahi ya kifedha na limebaki jukumu la kila mtu kujitambua.
Ninavyojua kwa uelewa wangu wa kawaida kwamba, k**a wewe ni mtafiti unapotaka kuibua “mada ya tafiti yako” lazima uje na wazo kuu la tafiti yako ambalo litakuwa jukumu lako kulipatia jibu baada ya tafiti yako. Mfano, Mazoezi ya kuruka Kamba mara 100 kwa siku sita kwa wiki kwa akina mama wenye watoto wawili ni nguzo ya kupunguza uzito. Kazi yako kubwa ni kutafuta jibu la “Hypothesis” yako k**a ni ndio au hapana. Kumbuka pale inapotokea hakuna uhusiano wa kuruka Kamba na uzito kupungua basi unatakiwa “Ufute kauli” ina maana hio hypothesis yako haijafanikiwa k**a lengo lako lilikuwa watu wapungue kwa kuruka Kamba na hakuna aliyepungua. Hivyo hivyo k**a ulaji kupindukia kunasababisha kitambi,basi chukua kikundi cha watu walishe vyakula kupindukia na endapo kitambi kisipotokea basi tutakutaka ukanushe kauli yako na ufikirie upya kabisa maana yake swali lako la kiutafiti halina mahusiano na unachokitaka. Hivyo hivyo k**a vyakula vya mafuta k**a nyama,nazi,mayai,mafuta ya ng’ombe husababisha chembe moyo na kuongezeka kwa nyama uzembe na kitambi basi unaweza kufanya tafiti ukaona nini kitatokea na endapo usipo pata majibu uliyokuwa unatarajia ni wajibu wako kisayansi utengue kauli.
Hakuna mwanasayansi ambaye yupo katika historia ya sayansi yetu hii chini ya dunia ambaye ameshawahi kutunikiwa tuzo ya nobel (Heshima) kwa tafiti yake na akaja mbele ya uma kukanusha ukweli kwamba tafiti yake haijaweza kuzaa matunda yoyote katika jamii yake maana k**a ni maradhi ndio yanaongezeka. Hayupo na k**a yupo “Nitajie”
Mfano mzuri ni bwana Ancel Keys aliyetuambia mafuta aina ya “saturated” husababisha magonjwa ya moyo baada ya kufanya tafiti yake katika inchi 22 na baada yake akatoa ripoti ya uongo katika nchi 6 tu na kuita tafiti yake “Mkombozi wa maradhi ya moyo” Leo hii kila tafiti inayofanyika kwa binadamu inakuja na majibu tofauti kabisa na yanayojitosheleza kuwa mafuta ya saturated sio chanzo cha magonjwa ya moyo. Na gazeti maarufu la times magazine ambalo lilikuwa la kwanza kumtangaza bwana Ancel keys kuwa ni mkombozi wa magonjwa ya moyo na ni mwanasayansi wa kudunia aliyegundua suluhisho la maradhi tabia. Mwaka 1977 bwana Ancel keys aliweza kukutana na Taasisi ya lishe na kuwasilisha tafiti yake ya nchi 6 badala ya inchi 22 ambazo alifanya tafiti na American Nutritional Association aliipokea na kuingiza ndani ya mwongozo wa lishe wa kidunia. Hapo hapo bwana Ancel keys aliweza kukaa kimazungumzo na Taasisi ya moyo ya America na kufikia mwafaka wa kuipokea tafiti hio. Mwaka 1977 mwongozo wa lishe wa America (American Dietary Association ) ulitoka na ulikuwa na malengo makuu yafuatayo:
1. Kuongeza matumizi ya vyakula vya wanga asilimia 55 hadi 60 na kuonesha kwamba vyakula hivi ni rafiki kwa afya yako
2. Kupunguza matumizi ya vyakula vyote vya mafuta hadi asilimia 30 na hakikisha kwamba hio asilimia 30 kusiwepo kabisa na vyakula vya mafuta aina ya “saturated”
Hapo ndipo dunia ilipo anza kuugua na ukiangalia ongezeko la maradhi haya ni jambo la kusikitisha. Mwaka 1919 baada ya vita ndio ilikuwa historia ya kidunia mwanadamu kuglika na magonjwa ya moyo. Hebu tizama k**a suluhisho la bwana Dr Ancel Keys mwana Fiziolojia wa kidunia alileta suluhisho je tungefika hapa tulipo?
Huwa napenda kusema kuna maangamizi makubwa makuu 4 katika sayansi ya lishe na magonjwa ambayo moja wapo ni Mwongozo wa lishe wa kidunia maana huwa unanijengea maswali mengi sana bila majibu. Kwani bwana Dr Ancel keys ndiye aliyekuja kutuaminisha dunia nzima vyakula vya mafuta ni adui kwetu na vyakula vya wanga na sukari ni rafiki kwetu lakini hadi sasa hali ni mbaya kuliko siku ile anatamka maneno hayo kinywani mwake. Dunia imeugua,imeugua vya kutosha na imelemewa na maradhi tabia vya kutosha. Ingawaje gazeti lilelile mwaka 2000s lilikuja kukanusha kwa uma “sio kweli mafuta yanasababisha magonjwa ya moyo k**a bwana Ancel keys alivyosema katika tafiti yake” lakini sijawahi kuona taasisi yoyote inapokea ukweli kwamba “diet –heart hypothesis” haina faida yoyote tofauti na kuendelea kuuguza jamii. Hakuna mtu atakanusha na haitakuja kutokea maana viwanda vikubwa duniani ni viwanda cha madawa ya kushusha cholestro mwilini yaani “Cholestro lowering drugs” maana siku wakikanusha ndio itakuwa anguko la viwanda vyote vinavyotengeneza dawa za cholestro,kansa,presha nk.
Ukija kuchunguza tafiti nyingi zinanishangaza pia wewe k**a msomi pia lazima utizame kwa upana Zaidi maana huwezi kufanya tafiti ya chuma kupata kutu kwa siku 3 utapata majibu ambayo sio ya kweli. Leo hii tafiti za uzito mkubwa,kitambi,kisukari na magonjwa ya moyo yanafanywa kwa siku,wiki,miezi na hakuna tafiti nyingi zinazozidi mwaka. Mano, ukiweka chuma yako kwenye unyevunyevu ukitajia ipate kutu halafu ukaja kuangalia matokeo baada ya siku tatu utakuja na hitmisho hili “Chuma haiwezi kupata kutu hata k**a ukiweka katika unyevu unyevu wowote” je tafiti yako itakuwa na majibu sahihi?
Pili huwa najiuliza tafiti nyingi zinafanywa kwenye panya,nyani,chimpanzee swali la kujiuliza je sisi ni panya? Sisi ni nyani? Kwa nini kuna virusi wengeni kwenye nyani hawana maradhara lakini kwa binadamu wana madahara? Wewe utaamini tafiti gani kati ya mtu aliyefanya tafiti kwa kutumia binadamu na aliyefanya tafiti ileile kwa kutumia panya au nyani? Tafiti nzuri ni iliyofanyika kwa binadamu kwani wewe sio panya wewe sio nyani wewe ni binadamu!
Hadi sasa dunia ya kisayansi ina ukweli wote kuhusu kushindwa kwa sayansi ya kemikali kuondosha maradhi hasa maradhi ya lishe , hadi sasa BBC inakili kwamba huwezi kuondoa tatizo la kitambi kwa kutumia uelewa ule ule kwani hauna nafasi kwa sasa haujaonesha manufaa miaka na miaka. Ni jukumu lako kutafuta maarifa Zaidi mimi nakupa mwanga lakini mengi unaweza kuendelea kutafuta maarifa kila siku.
UKWELI NI KWAMBA KITAMBI NI MVURUGIKO WA HOMONI MWILINI MWAKO
Kumekuwa na tafiti nyingi ambazo hadi sasa zimeshindwa kuleta matunda imebaki jukumu lao kukiri na kutengua kauli na kurudisha tuzo za heshima ya kisayansi maana hazina matunda yoyote kwa binadamu. Sayansi ya kusema kitambi ni kutowiana kwa kalori zinazoingia na kalori zinatumika imewafanya watu wajinyime na kuibua maradhi tabia mengi k**a vidonda vya tumbo na uchovu sugu usio na suluhisho na baada tu ya kuacha kujinyima kilo zote hurudi. Najua hilo unalijua maana kila mtu linamtokea ndio maana kila mtu hajapata suluhisho la kudumu la kuhakikisha kilo haziongezeki tena,
Napenda kusema nakukaribisha katika sayansi mpya na sayansi ambayo imeleta matumaini kwa mamilion ya watu. Na itachukua muda mwingi sana sayansi hii kuja kukubarika lakini ukweli utabaki pale pale na mtu mwelevu anaweza kujikomboa kwa kujitambua afya ni hazina yake. Haipo siku itakubalika maana “Itakuja kuangusha biashara ya kila taifa tajiri”
Huwa nasema kwamba nikiwa na homoni mbili mkononi mwangu naweza kukunenepesha, homoni hizo ni insulin na cortisol. Nikimaanisha kuwa nataka nikupe mchango wa hizi homoni katika kusababisha kitambi na maradhi mengine tabia.
Unaweza kulifanya hili hata wewe chukua wagonjwa wote ambao unawaanzishia sindano za insulin k**a wana kisukari aina ya pili na kisha wafuatilie kwa miezi sita. Majibu yako utajie kilo kuongezeka,sukari inaweza kuwa imeimarika haimsumbui lakini kisukari kitaendelea kmshambulia. Kwani “Diabetes is not sugar diseases” kwa maana hio unashindwa kutambua chanzo cha sukari kuwa katika kiwango kisichostahili na kisha ushughurikie tatizo lakini cha ajabu Zaidi unashughurikia sukari ambapo ni dalili ya kisukari. Hivyo basi kwa wale ambao wanatumia insulin ni mashuhuda wangu wa kwanza kwamba insulin inaongeza kilo na kusababisha kitambi.
INSULIN NI NINI?
Hii ni homoni ambayo inatengenezwa na seli aina ya beta katika kongosho la binadamu. Homoni hii humwagwa na kongosho mara tu baada ya kula kwa malengo makuu yafuatayo
1. Hutusaidia kubadilishe kile kiwango cha viini lishe vinavyozidi kiasi na kubadilisha kuwa mafuta na gylycogen. Mwili huhifadhi kiwango maalumu tu cha glycogen na nishati yote inayobaki huhifadhiwa katika mfumo wa mafuta. Hii ni ishara kuwa mwili una stoo ya mafuta isiyokuwa na kikimo
2. Pili husaidia seli za mwili wako ziweze kutumia glucose au sukari inayopatikana katika lishe
Naweza nikasema hizo ndizo kazi kuu mbili za homoni hio na ndio maana huwa naita homoni hii ni “Fat cell Fertilizer” yaani ni mbolea ya mafuta maana yake kazi kubwa hii ni kuhakikisha hakuna nishati inayopotea ovyo zote zinahifahiwa katika mfumo wa mafuta.
Hivyo sote tumekubaliana kwamba homoni ya insulin inanenepesha, na swali la kujiuliza ufanyeji ili isiendelee kuninenepesha?
Kuna vitu vingi vinavyosababisha homoni hii kuwa katika kiwango kisichostahili katika miilini yetu ambavyo naweza kuvitaja vichache hapa
1. Ulaji wa vyakula vya wanga kupindukia
Wengi huniambia Dr Boaz mimi natumia wanga ambayo haijakobolewa, mwingine ataniambia natumia brown rice. Ni kweli tafiti zinasema hivyo lakini hakuna utofauti wa wanga iliyokobolewa na ambayo haijakobolewa kwenye kiwango cha sukari katika chakula chako. Maana huwezi ukaniambia gram moja ya nafaka ambayo haijakobolewa ina utofauti katika kiwango cha sukari na gramu moja ya nafaka ambayo haijakobolewa. Hivyo tunachoangalia ni “Glycemic index” ya vyakula na sio tofauti ndogo inataka kutumiwa kibiashara ndio maana kukaibuka na brown rice, jiulize babu zetu walitumia aina hio ya mchele? Actually no!
Katika aina zote za vyakula, wanga ni aina pekee ya vyakula ambavyo vinasababisha uchovyaji wa hali ya juu wa homon ya insulin. Ambapo vyakula vya protin vinaonesha kuongeza insulin kidogo sana na vyakula vya mafuta hakuna ongezeko lolote la insulin utashuhudia. Ndio maana sayansi mpya ya lishe na kitambi inapinga sayansi inayosema “calorie is a calorie” maana huwezi kusema kalori za wanga ni sawa na protini na ni sawa na mafuta katika kusisimua uchovyaji wa homoni ya insulin.Kauli hii ningependa siku moja “Itenguliwe jamii itakombolewa”
MADHARA YA INSULIN KUWA KATIKA KIWANGO CHA JUU MUDA WOTE
1. Kuongezeka uzito kupindukia
2. Uchovu wa muda wote
3. Kuzeeka mapema
4. Kujengeka kwa kitambi
5. Kupata vimbe mbalimbali k**a kansa
6. Magonjwa ya mifupa (Arthritis and gout)
7. Homon za kiume kupungua na za k**e kuvurugika
8. Ngozi yako kuzeeka
9. Kuongezeka kwa LDL (Low density lipoprotein) na Kupungua kwa HDL (High density Lipoprotein) na hatimaye kukusababishia magonjwa ya moyo
10. Seli za mwili wako kujenga usugu na homoni ya insulin(Insulin Resistance)
2. Ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi ambayo inapatika katika chakula asili au inaongezwa katika vyakula kukupa radha.
Huwa wengi wakiniambia kwa nini daktari kichwa kinauma, natetemeka mikono, na mapigo ya moyo yanaenda mbio nimeacha kutumia sukari na wanga jana! Wengi huwa nawaambia sukari ni “Pychotic drug” pia nimekuwa nikiwaambia sukari inalevya k**a pombe,heroin na co**in na hivyo basi unapo acha lazima upate dalili k**a mlevi wa gongo,bia,sigara ,heroin,bangi atakapo kosa kelevi chake kwa muda mfupi. Hivyo wote wanafunzi wangu wa darasa langu la mwongozo wa lishe The Health Eating Acedemy nimewafundisha mbunu za kuondokana na tatizo. Ndio maana nasema kila siku ukitaka ufike salama unakotaka kwenda k**a unaona giza hakikisha unakuwa na mwelekezi. Vyakula vya sukari huongeza sana uchovyaji wa homoni ya insulin
3. Vyakula vyenye vionjo ,rangi ambavyo ni kemikali katika mwili wako
Endapo ukiepuka mambo makuu hayo 3 lazima utasawazisha kiwango cha homoni yako.
HAKIKISHA!
Unaongeza matumizi ya vyakula ambavyo havipandishi kabisa kiwango cha insulin katika damu yako vyakula vya mafuta na protini k**a nyama,mayai,samaki nk kwani ni vyakula ambavyo vinapunguza uchovyaji wa insulin na kuondoa matatizo yote kiafya. Maana yake katika mwongozo wa lishe Healthy eating academy elimu yangu imejikita kukupa faida ya mwili wako katika kutumia mafuta k**a nishati ya mwili dhidi ya wanga.
KITAMBI CHAKO KINAPIMWA KATIKA MUDA
Tafiti zinaonesha kwamba kwa kawaida kitambi kinapatikana pale binadamu anapokuwa anaongezeka kilo 500gm hadi 1kg kwa kila mwaka. Sasa chukua mfano wewe una umri wa miaka 20 na una kilo 70 baada ya miaka 30 mbele utakuwa na kilo 100 maana yake umeongenezeka kilo 30. Nazani umenielewa rafiki yangu ninacho maanisha. Sasa iweje leo hii tunaaminishwa kwenye tafiti za siku? Mwezi?.
Mtu ambaye amepata uzito uliokithiri ndani ya muda mfupi ni tofauti na mtu ambaye amekuwa akilea kitambi chake kwa miaka takribani 20 katika kukiondoa inahitaji ustahimilivu kwa sababu zifutazo za kisayansi. Moja ya tafiti ambazo zilianyika kuonesha kwamba kuna utofauti gani katika muda na kuondoa kitambi na hapo walichukua makundi mawili, kundi la kwanza ni lile ambalo wamepata kitambi kabla ya miaka minne na nusu na lingine Zaidi ya hapo. Kundi la chini ya miaka 4.5 walipungua uzito haraka kuliko kundi la pili! Swali la kujiuliza kwa nini? Lakini sayansi ya kalori yenyewe inatuambia kwamba hata k**a una kitambi cha miaka mingapi ukipunguza kula na kujinyima lazima upungue! Inaonesha ni sentensi yenye matumaini lkn hakuna mtu ambaye alishawhi kufanikiwa na bila kuibua maradhi ndio maana nakupa sababu kwa nini hufanikiwi?
KUTOFANYA KAZI KWA INSULIN (INSULIN RESISTANCE)
Hii ni ile hali ya seli za binadamu kuonesha usugu katika kuitambua insulin. Maana yake insulin inafanya azi k**a vile funguo na kufuli la nyumba yako. Lazima insulin (funguo) ijishike kwenye seli ya binadamu sehemu iitwayo kipokea insulin (Receptor) ifungue mlango kuruhusu sukari iingie ndani ya seli.
Hivyo kazi kubwa ya insulin ni kufungua geti ili glucose ziweze kuingia ndani ya seli na inapotokea insulin ipo katika damu na haina uwezo wa kufanya hivyo basi hali hio ndio tunaita Insulin resistance.
Je nini kinatokea kunapokuwa seli zimetengeneza usugu kuitikia amri ya insulin?
Kinachotokea ni kwamba seli zinapopata usugu wa kutoitikia wito wa insulin kufungua viingiza glucose kwenye seli na matokeo yake seli yako haitajitosheleza kwa nishati. Na kinachotokea ni mwili kujaribu kwa namna yoyote kurekebisha tatizo na tatizo hilo hurekebishwa kwa kuongeza uzalishwaji wa insulin kwa wingi Zaidi.
Mfano :
Una funguo zako 10 (Insulin) kila ufunguo unafungua makufuli (Insulin Receptor) 10 na kila unapofungua unaruhusu glukosi mbili na hivyo jumla ya glucose 20 zitaingia ndani ya seli hizo. Lakini pale inapotokea seli zimejenga usugu na insulin, yaani zime “Tolerate” utendaji kazi wa insulin utapungua badala ya kila insulin 10 kuingiza glukosi 2 basi kila insulin itaingiza glucose 1 na hatimaye kutakuwa na mapungufu ya glucose kumi. Mwili utajitahidi kufidishia kwa kutengeneza funguo(insulin) zingine kumi.
Ndio maana tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu wenye kilo nyingi wengi wana kiwango kingi cha insulin na sio pungufu! Na watu wembamba wana kiwango kidogo cha insulin.
JE NINI KINASABABISHA USUGU HUU?
Kabla sijajibu swali hili naomba niongelee haya machache
1. Watu wengi tunajua kwamba matumizi mabaya ya ant bayotiki yanaweza kupelekea ile dawa kutokuwa na uwezo wa kuua tena wadudu wale hata kwa kiwango kikubwa cha dozi kiasi gani. Hivyo kadri unavyo ongeza dozi ndivyo na kiwango cha usugu kinaongezeka. Hivyo kisababishi vya usugu katika dawa ni dawa yenyewe.
2. Chukulia mfano mtoto ambaye amebebwa na mama yake yupo stendi na kuna kelele nyingi sana za hapa na pale, mtoto huyo itafikia hatua anazoea zile kelele na zinakuwa hazina madhara kwake na anapitiwa usingizi bila kujali makelele hayo. Maana yake mtoto ametengeneza usugu au “ame tolerate” hali ya kelele.
3. Pia kwa mtu anayekunywa pombe k**a unakunywa pombe mbili unalewa itafikia hatua hulewi tena. Utaongeza zinakuwa nne mwishowe nazo zinakuwa hazisikiki unaongeza dozi tena na tena hivyo basi kadri unavyo ongeza dozi hata usugu wa tatizo unaongezeka.
Hivyo hivyo tunaposema seli za mwili zimepata usugu katika kuitumia insulin inayotengenezwa na badala yake ili kuweza kusawazisha tatizo mwili na uendelee kuishi mwili unaitikia kwa kuongeza uchovyaji wa insulin nyingi na Zaidi na Zaidi. Kumbuka kadri kiwango cha insulin kinapo ongezeka na usugu wa tatizo unaongezeka!
Chukua mfano mgonjwa wa kisukari aina ya pili seli zake huwa zimejenga usugu katika kutumia insulin na hivyo basi mwili unaitikia kwa kutengeneza insulinnyingi Zaidi ili kuweza kusukuma sukari ya kutosha ndani ya seli. Hivyo mgonjwa wa kisukari aina ya pili (kisukari cha ukubwani) katika damu yake huwa ana kiwango kingi sana cha insulin kwani seli zake huwa zina usugu wa kutotumia insulin. Na tiba ya punguza usugu wa tatizo ni kupunguza kiwango cha insulin kwani tumeona kadri unavyo ongeza dozi ndivyo usugu wa tatizo unavyo ongezeka.
Lakini chakushangaza kisukari aina ya pili kinapofikia hatua mbaya kinakuwa k**a ugonjwa wa upungufu wa insulin (Insulin deficiency disease) na hivyo huanza kutibiwa kwa sindano za insulin. Kumbuka sindano hizi huongezea mwili insulin ambayo imetengenezwa kiwandani (exogenous insulin), rudi kwenye mfano wangu hapo juu nilisema k**a insulin moja ilikuwa inaingiza glukosi 2 na panapotokea usugu insulin inapunguza ufanisi wake kiutendaji inaanza kuingiza glukosi 1. Ili kuongeza idadi ya glukosi mwili wako uweze kuishi salama bila tatizo basi mwili huitikia kwa kutengeneza insulin nyingine nyingi kuja kusawazisha tatizo. Na dawa hizi zinaongeza idadi ya funguo yaani glukosi ili sukari nyingi zitumike. Kumbuka kadri unavyo ongeza idadi ya insulin katika damu ndivyo unavyozidi kuongeza tatizo la usugu kwa maana nyingine ni sawa na kumtibu mlevi wa gongo kwa gongo “Treating alcoholism with alcohol” nini ambacho unatarajia? Je pombe itaisha? Actually no! Hivyo sukari itashuka lakini usugu wa seli dhidi ya insulin utaongezeka(Blood sugar will normalize but diabesity gets worse) ndio maana kisukari ni ugonjwa endelevu na sugu k**a usiposhughurikia tatizo na tatizo hapa ni “Insulin resistance” na kibaya Zaidi tafiti zote za kwamba mafuta ndio chanzo cha seli kutengeneza usugu zimekosa matumaini. Njia pekee ya kuondoa insulin resistance ni kupunguza insulin na sio kuongeza insulin.
Hivyo hivyo watu wengi wanane kupita kiasi wapo hatua za mwanzo za ugonjwa wa kisukari kundi hili huitwa pre diabetes dalili zake ni k**a hizi:
1. Uzito mkubwa kupita kiasi
2. Mvurugiko wa homoni za k**e PCOS
3. Kukosa hamu ya tendo la ndoa
4. Kuongezeka kwa LDL, Triacylglycerol na Kupungua kwa HDL
5. Kiwango cha sukari huwa kipo sawa (Normal)
6. Weusi kwenye mikunjo ya ngozi, shingoni kwapani mapajani na sehemu zingine
7. Kuota ndevu usoni kwa wanawake na sehemu zingine kupita kiasi k**a kifuani
8. Matatizo mengine ya kiafya yanayo ambatana naa kitambi na nyama uzembe (Belly fats)
9. Maumivu makali wakati wa hedhi
10. Kukosa usingizi,gesi na misuli kuuma muda wote
Kwa pamoja dalili hizo naweza kuziweka katika kundi la Metabolic syndrome
Hivyo watu wengi huniambia dr Boaz mimi ni mnene sana lakini nashukuru Mungu sina ugonjwa wowote, sio kweli maana ugonjwa wa kisukari ni hatua ya mwisho kabisa. Ni sawa k**a tunapotumia neon UKIMWI maana yake upungufu wa kinga mwilini na sio wote wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) wana upungufu wa kinga mwilini hapana! Hivyo ukimwi ni hatua ya mwisho! Na kipimo chake ni dalili zake hatari,kiwango cha VVU na Kiwango cha seli nyeupe za damu (CD4). Hivyo hivyo hata ugonjwa wa kisukari kupima sukari ikawa kawaida haimaanishi wewe haumwi kisukari ningekushauri utizame dalili hizo hapo juu za pre diabetes au metabolic syndrome kisha utajua afya yako inaelekea wapi. Tafiti zinaonesha kwamba jamii kubwa ipo katika kundi hili la pre diabetes na muda si mrefu inaelekea kwenye kisukari kabisa na habari njema Zaidi ni kwamba ni virahisi sana kukurudisha kwenye afya njema k**a bado hujafikia kwenye kisukari kabisa.
KWA NINI WENGINE WANAPUNGUA UZITO HARAKA WENGINE POLEPOLE SANA
Nilisema mwanzo kitambi ni tatizo linalo endana na muda, mtu ambaye alikuwa na mwili wakawaida baada ya kujifungua akaongezeka kilo 30 na ndani ya miaka 2 ameshindwa kuurudisha uzito wake wa mwanzo akipata mwongozo mzuri wengi sana wanapungua uzito haraka sana kwa sababu wanakuwa hawana kabisa tatizo la insulin resistance. Na kumbuka usugu wa seli kutotumia insulin huongezeka kadri miaka inavyozidi kusonga. Na hivyo mtu ambaye amelea kitambi chake kwa miaka mingi akiendelea na lishe ileile na maisha yaleyale hata k**a atabadilisha lishe na kufanya mazoezi hataweza kutimiza malengo kiurahisi.
Kwani tatizo la insulin resistance linazidi kuwa sugu kadri miaka inavyosonga, na hivyo kuongeza ufanisi wa insulin itatakiwa ichukue muda mrefu sana hadi pale tutakapo hakikisha kiwango chako cha insulin kimerudi kawaida na dalili mbaya nilizotaja hapo zimepotea na baada ya hapo utaanza sasa kupungua uzito.
IDADI YA MILO NA KITAMBI
Sasa ni dunia ambayo inatakiwa iwe katika maajabu yake kwani si ulimwengu wa babu zetu ambao walikuwa wanakula chakula kwa kutenga kwa pamoja na katika hali tulivu. Leo hii mtu anakula akiwa kwenye gari, anakula akiwa kwenye boda boda,anakula akiwa saloon,anakula akiwa barabarani, anakula akiwa kwenye dressing table,anakula akiwa yupo mbele ya TV. Maisha haya inatakiwa tumtafute mchawi wetu ni nani na nini madhara yake kiafya na Imani potofu zilizosababisha binadamu wa kale atoke kwenye milo 2-3 kwa siku hadi sasa tuna idadi ya milo 6 kwa siku na sio tu hilo tunaambiwa na milo ya kiafya! Angalia maradhi yanavyongezeka toka mwaka 1960 na hadi 2014 unataka kuniambia idadi ya milo imeleta mchango gani kuboresha tatizo hilo au inaweza kuwa imechochea kutufikisha hapa!
FIKRA POTOFU 1
Tumefundwa na wataalamu wetu punde tu unaposhusha mguu wako kitandani breki namba moja ni kwenye jiko kupata chakula asubuhi. Na baada ya hapo tunakula mchana kutwa bila hata kutulia.
Kumbuka nilisema kwamba, utafiti wao ulilenga kukuwezesha wewe uwe na sukari ya kutosha mwilini mwako kukuwezesha wewe kufanya kazi zako za kila siku.
Hili linapingana na tafiti za sasa ambapo mwili wako binadamu hauwezi ukaishiwa sukari gafla labda uwe mgonjwa wa kisukari tena ambaye unatumia dawa! Lakini k**a wewe ni mzima mwenye afya, mwili pale tu sukari inapopungua kidogo hujaribu kufanya mbinu zozote kuhakikisha sukari inapatikana kupitia kitendo kiitwacho Gluconeogenesis and Gycogenolysis. Na hii naweza kukuambia binadamu aliyefunga rekodi ya kufunga siku 365 hapa duniani unaweza kuangalia katika historia alifikiaje siku zote hizo na kufunga rekodi ya dunia!
FIKRA POTOFU 2
Kula mara kwa mara kunakuzuia kupata njaa. Lakini hakuna ushuhuda wowote wa kisayansi unao bainisha au kuweka bayana maneno haya kwamba ukila mara kwa mara kuna mahusiano na kuzuia njaa. Kwani ninavyojua na tafiti zinaonesha sio idadi ya milo ndio hupunguza njaa bali aina ya vyakula ndio hupunguza njaa na baadhi kuongeza njaa.
FIKRA POTOFU 3
Ukila mara kwa mara kunaongeza kasi ya utumiaji wa viini lishe au nishati ndani ya mwili wako na inaweza kukusaidia kuondokana na maradhi ya kisukari,unene na mengineyo. Lakini ukweli ni kwamba hakuna mahusiano ya kupunguza uzito na kuongezeka kwa kasi ya shughuli za mwili maana miili yetu huwa inajisawazisha kutokana na mazingia yaliyopo, k**a ukiulisha kiwango kidogo utafanya kazi katika kiwango kidogo na wastani na k**a ukiulisha kiwango kikubwa utafanya kazi katika kiwango cha kasi Zaidi ili kuendana na nishati uliyo ingiza mwilini mwako. Mwili wako unafanya kazi k**a thermostat ndani ya AC au Fridge yako.
KUNA MADHARA GANI KIAFYA IDADI YA MILO INAPO ONGEZEKA?
Unapokuwa na tatizo la kitambi,kisukari na maradhi mengine tunayapima kwa nguzo kuu mbili k**a unataka kulipatia ufumbuzi tatizo lako haraka sana
1. MUDA
Nilisema mwanzo kuwa kadri muda unavyo enda seli zako ndivyo zinavyojenga usugu katika matumizi ya insulin yaani insulin resistance ndivyo inavyo ongezeka na ndivyo tatizo linavyozidi kuwa sugu kutibika. Ndio maana program yangu ya “THE HEALTHY EATING ACADEMY” nimekuwa nikilenga kuhakikisha nawaboreshea afya watu kwa kusawazisha kiwango cha homoni zao na kizuri Zaidi baada ya kusawazika wengi hunieletea shuhuda nyingi sana. Muda ni kitu cha kuzingatia sana kujua usugu wa tatizo lako katika lishe.
2. KUDUMU KWA KISABABISHI KINAONGEZA INSULIN RESISTANCE
Hapa ndipo penye tatizo katika idadi ya milo,kumbuka nilisema mwanzo homoni ya insulin inamwagwa na kongosho lak moja kwa moja kwenye damu baaada tu baada ya kula chakula. Na kazi yake kubwa ni kuja kuhifadhi nishati inayozidi katika mafuta na glycogen.
Na ili seli za mwili wako zisichenge usugu unatakiwa kuwepo na muda wa kuzipumzisha kupokea amri kutoka kwa insulin.
Mfano, Umeshawahi kujiuliza mbona k**a tunaisha katika nchi zenye malaria sana kwa nini tusiwe tunakunywa dawa ya mseto kujikinga na maradhi? Tunaogopa wadudi wa malaria watajenga usugu dhidi ya dawa zetu
Pia unajua kwa nini dawa hasa anti biotiki ukipewa kuna muda maalumu halafu unasitisha? Kwa nini k**a wewe unasumbuliwa na UTI usitumie muda wote? Hapana bakteria watajenga usugu na hio dawa!
Hivyo hivyo hata mwili wako ukitaka kuuzuia seli zako zisijenge usugu katika kutumia insulin (Insulin resistance) lazima mwili wako uwe kuna muda insulin ipo juu na muda insulin chini.
Je Ni muda gani insulin inapanda?
Insulin inapanda pale tu unapokuwa umekula kwenda kufanya kazi yake na kumbuka insulin hukaa katika damu sekunde 2 hadi tatu na hatimaye humaliza kazi yake. Ndio maana vipimo vyake imekuwa ni kazi sana na kiwango chake kinabadilika kulingana na uwepo wa chakula mwilini. Ndio maana tukitaka kupata jibu sahihi la kiwango cha insulin tunapima kiwango cha insulin ambacho hujala kwa muda mrefu (Fasting insulin)
Je insulin inashuka wakati gani?
Insulin hushuka mara tu baada ya kukaa masaa kadhaa baada ya kumaliza kula.
Kwa maana hio lazima nione insulin yake iwe katika mtiririko wa Kupanda na Kushuka na sio kuwa katika kiwango cha juu muda wote kwa sababu ya kula masaa yote.
Nilisema mwanzo kuwa sayansi inayotuambia ukiamka asubuhi amka na chakula kisha shinda muda wote unakula inafanya insulin yako muda wote iwe kazini inapiga mziko na hatimaye itafikia sehemu insulin haitakuwa na uwezo wa kufanya kazi tena maana seli zitajenga usugu.
Mfano, Mtu anayekula saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni ndipo anakula mimi naweza kumsema kwamba ana masaa 10 ya kula na masaa 14 ya bila kula.
Wakati wa masaa kumi ndipo insulin inakuwa ipo katika kiwango cha juu kufanya kazi yake nay ale masaa 14 insulin inakuwa imeshuka kiwango chake.
NOTE: Kitaalamu tunaita “Insulin Pulses” yaani kule kuongezeka na kushuka kwa insulin mwilini mwako.
Kiafya muda ambao insulin inatakiwa iwe katika kiwango cha chini UNATAKIWA KUWA MKUBWA kuliko muda ambao insulin ipo katika kiwango cha juu. Hii inatoa muda kwa seli kutojenga usugu au tolerance to insulin.
Kibaya Zaidi watu tumeugua kwa sababu mwongozo wa lishe unatushauri kuongeza idadi ya milo hadi 6 kwa siku na matokeo yake “Insulin Pulses” zinatoa ishara nyekundu ya hatari kwamba MUDA WA INSULIN KUWA JUU ni mkubwa kuliko muda wa insulin kuwa katika kiwango cha chini. Hii ni kwa sababu muda wote unakula hauna wakati maalumu wa kupata chakula. Hii pia inaweza ikakupa maelezo ya kisayansi kwa nini vijijini maradhi tabia ni kiwango kidogo ukilinganisha na mjini huko nao wanatumia vyakula vya wanga vile vile, hii ni kwa sababu idadi ya milo yao bado ni 2 mpaka 3.
Najua umejifunza kwa nini sasa Milo sita inaweza kuwa hatari kwa afya yako k**a ndoto yako ni kuishi mwenye afya, katika program yangu najua kwamba wanga ni moja wapo ya vyakula vinavyongeza njaa na sio kukata njaa ndio maana waandishi wa mwongozo wa lishe hadi sasa wanashauri kula hata kila baada ya masaa 2 na nusu kwa sababu wanga inaongeza njaa na hakuna sayansi yoyote inayo onesha wanga inapunguza njaa. Na sababu kubwa tunatumia wanga kwa wingi ni kwa sababu viini lishe vingine vinavyo upa mwili nguvu na ndivyo mashuhuri kwenye kukata njaa alisema Dr Ancel Keys ni hatari kwa afya zetu na tukampatia tuzo ya heshima kwa kutuongezea milo kutoka 2 hadi sita na njaa kali hatuwezi tena kukaa hata masaa 6 bila kula tumefikia hatua tunakula kila baada ya masaa 2.
Katika program yangu ya The Eating Academy watu wengi wanafurahia jinsi gani walihangaika na maradhi, na kupuuzia njaa wakilenga kupunguza uzito leo hii wanaishi maisha ya bila njaa za mara kwa mara wanapunguza uzito bila kufanya mazoezi na kisukari kinapotea na kupunguza idadi ya dawa! Napenda kukushauri kam ukitaka kuanza program hii ni bora ukapata mwongozo wa karibu kwani huwezi kufika unakofika k**a unaona ni giza, kupunguza uzito,kuondoa kitambi ni kitendawili lakini sasa kinateguka.
Nimefurahi kuwa umekuwa miongoni mwa wasomaji wangu wazuri Mungu akubariki. Share Ujumbe huu kwa ndugu yako naye Akombolewe nimejitahidi kueleza kwa wepesi hata k**a ulikuwa unakimbia biolojia ujue kwa nini dunia imeugua kwa kuengeza idadi ya milo, shule zetu watoto wetu wanakula milo mingi hadi tunashindwa kuelewa watoto hawa tunawapeleka wapi, Chai, snacks, mchana,snach,usiku milo yote hio yao unategemea utaepuka lini Kitambi cha utotoni? Hebu vita ianzie nyumbani kwako ndio maana sasa kumekuwa na viwanda vingi sana vinadhidi kuendena na sera kutengeneza “Snacks” Ambapo zinadhidi kudhoofisha miili ya watoto wetu. Madiliko yanaanzia ndani ya nyumba yako, pinga kabisa, k**a wewe umeathirika na kitambi,kisukari iwe ndoto yako kuhakikisha watoto wako wanakuwa wenye afya
SHARE MAKALA HII NA MARAFIKI ZAKO
0757842606