18/02/2022
Tatizo hili huripotiwa kuwa katika wanaume watano (5) basi mmoja kati yao anatatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kuto kuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.
Hili tatizo huwanyima watu raha kwa kuwa na mawazo, kuwa na matatizo katika mahusiano, watu wengi wenye tatizo hili wanahitaji kutumia dawa zisizo na madhara na kubadilisha mitindo ya maisha yao ili kuweza kurudisha hali zao na kuondoa tatizo, cha msingi ni kuzingatia yale utakayoelekezwa.
Kuna matatizo ya kutofanya mapenzi kikamilifu, nayo ni; kuwahi kumwanga mbegu za uzazi, Kuto kumwaga, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa
CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;
*Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo
*Kuvuta sigara na unywaji wa pombe
*Uzito kupita kiasi na unene uliozidi
*Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
*Kisukari
*Kuwa na mawazo na wasiwasi
*Matumizi ya madawa mbalimbali
*Umri hasa wazee
*Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
Kuwa na tatizo la kibofu
*Tabia za kujichua kwa mda mrefu
*Kutopata usingizi kamili
*Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa k**a kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine