Maabady.003

Maabady.003 Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Maabady.003, Medical and health, mkoani pemba, Chake Chake.

🌹Perfumes kubwa original ni kuanzia Jumla 25500 rejareja 28500Ndogo ni jumla 4000 reja reja 5000 karibun wateja wetu
15/08/2025

🌹Perfumes kubwa original ni kuanzia Jumla 25500 rejareja 28500
Ndogo ni jumla 4000 reja reja 5000 karibun wateja wetu

💜 MAABAD COSMETICS STORE 💜Pata vipodozi na urembo vya kiwango cha juu: Perfume za kisasa, Body Spray zenye harufu za kuv...
11/08/2025

💜 MAABAD COSMETICS STORE 💜
Pata vipodozi na urembo vya kiwango cha juu: Perfume za kisasa, Body Spray zenye harufu za kuvutia, Lotion za ngozi, na Sabuni bora za ngozi.

📍 Tunapatikana darajan Zanzibar
🚚 Tunatuma mzigo Dar es Salaam na mikoa yote kwa uaminifu wa hali ya juu.

📲 Mawasiliano:
Facebook: Maabad Interpresses
WhatsApp: 0629771737
Instagram: maabad_alshirazy

✨ Urembo Wako, Fahari Yetu! ✨
Pia kuona mfano wa bidhaa zetu tembele
https://www.facebook.com/profile.php?id=100083557621118

✨🌹 MAABAD COSMETICS STORE🌹✨– Uzuri wa Kweli Unaanzia Hapa!Unatafuta vipodozi vya kuvutia, harufu ya kupendeza na ngozi l...
19/05/2025

✨🌹 MAABAD COSMETICS STORE🌹✨
– Uzuri wa Kweli Unaanzia Hapa!

Unatafuta vipodozi vya kuvutia, harufu ya kupendeza na ngozi laini k**a hariri?
Maabad Cosmetics Store ndiyo suluhisho lako!

Tunapatikana Zanzibar
Tunauza:
✨Perfume za kisasa

✨Body spray zenye harufu ya kuvutia🌹🌹

✨Lotion laini kwa ngozi yako

✨Shampoo za ubora wa kimataifa

✨Deodorants zinazodumu siku nzima⌚⌚

Tembelea duka letu upate huduma ya kipekee!
Kwa bei ya kitonga kabisa
Wasiliana Nasi:
Call: 0715 217 198
WhatsApp: 0629 771 737
Au tembelea page zetu za fb na
Instagram kuona baadh ya bidhaa zetu
Facebook: Maabad interpresess
Instagram:

Urembo, Harufu Mzuri, Kujiamini – Vyote ni
M. Cosmetics Store.✍️✍️
Pia ukinunua bidhaa zetu kwa wingi unapata punguzo mpaka asilimia 15%karibun sana wateja wetu

UVIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROID )Tatizo la uvimbe kwenye kizazi (fibroids) ni kubwa na linawatokea wanawake wengi sana. In...
13/07/2022

UVIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROID )

Tatizo la uvimbe kwenye kizazi (fibroids) ni kubwa na linawatokea wanawake wengi sana. Inakadiriwa kwamba 75% ya wanawake hupata tatizo hili la fibroids katika kipindi flani cha maisha yao. Kwa mujibu wa jarida la New England Journal of Medicine, kila mwaka zaidi ya wanawake 200,000 wanafanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi chote (hysterectomy) kutokana na tatizo hili la fibroids.

Fibroids ni nini?

Fibroids ni uvimbe usio wa saratani ambao hujitokeza kwenye kuta za mfuko wa mimbauitwao uterusi. Uvimbe huu husababisha kubadilika kwa shape na size ya kizazi na pia dalili zingine mbaya. Wanawake wengi huanza kupata maumivu makali wakati wa hedhi kutokana na uwepo wa uvimbe kwenye kizazi(fibroids . Ni jambo la msingi zaidi kwa wanawake wote kuchukua hatua katika kuzuia kutokea kwa fibroids.

Tafiti mbalimbali zinaonesha kwamba kuzuia au kutibu tatizo la kupanda kwa presha ya damu husaidia kupunguza hatari ya kupata uvimbe kwenye kizazi (fibroids). Utafiti uliofanyika katika chuo kikuu cha Havard unasema kuna uhusiano mkubwa kati ya presha ya damu na hatari ya kupata uvimbe kwenye kizazi(fibroids) kwa wanawake wanaokaribia kukoma hedhi.

Je Utajuaje k**a tayari una uvimbe kwenye kizazi (fibroids)
Je fibroids inaweza kusababisha kuvuja damu, maumivu ya mgongo na dalili zingine mbaya? Inawezekana kabisa lakini siyo kila mwanamke mwenye fibroids hupata dalili hizi, lakini pia uwepo wa dalili hizi siyo lazima kwamba una fibroids.

Unaweza kuwa na tatizo lingine la kiafya, ushauri mzuri ni kuonana na dactari haraka ili kupata vipimo. Zifuatazo ni dalili zinazojitokeza kwa wanawake wengi zaidi wenye uvimbe kwenye kizazi

Kupata Hedhi inayochukua siku nyingi kuanzia 7 na zaidi
Hedhi nzito
Kujiskia umeshiba mda mwingi
Maumivu ya nyonga
Kupata mkojo mara kwa mara na kushindwa kutoa mkojo wote kwenye kibofu.
Kukosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu
Kupata maumivu wakati watendo la ndoa
Maumivu chini ya mgongo na kwenye miguu.
Madhara mbalimbali ya uzazi k**a ugumba na mimba kutoka.
Uvimbe kwenye kizazi(fibroids) wakati wa ujauzito
Wakati mwingine mwanamke anaweza kupata fibroids akiwa kwenye ujauzito, ni dalili gani zinaweza kujionesha? Uvimbe kwenye kizazi(fibroids) inaweza kusababisha shida wakati wa kujifungua na kupelekea mwanamke kujifungua kwa upasuaji.

Inaweza kupelekea ugumba pia k**a tatizo ni kubwa sana kutokana na ugumu kwa yai kurutubishwa na kisha kujishikiza kwenye ukuta wa uterus.

Kwa wanawake ambao bado hawajazaa hushauriwa kutumia dawa ili kupunguza ukubwa wa uvimbe kabla ya kupata ujauzito. K**a tatizo ni kubwa zaidi basi upasuaji hufanyika kabla ya kushika mimba. Kumbuka ni vizuri kufanya vipimo kabla hujaamua kushika ujauzito, hii itakusaidia kupunguza hatari ya kumpoteza mtoto.

Fibroids huweza kuongezeka ukubwa wakati wa ujauzito kutokana na kiasi kikubwa cha homoni ya estrogen. Kuvuja damu na maumivu ya tumbo pia huweza kutokea kutokana na uvimbe kupoteza damu yake. Kwahiyo madaktari wa wanawake hupendekeza mgonjwa kufanyiwa ultrasound mara kwa mara ili kufatilia maendeleo ya uvimbe.

Aina za uvimbe kwenye kizazi(fibroids)
Jina la kitabibu la fibroids ni leiomyoma au myoma. Ukubwa, mahali ulipo uvimbe na pia idadi ya vimbe hizi inachangia zaidi kwenye uwepo wa dalili mbaya aatakazopata mwanamke. Inawezekana kabisa kuwa na aina zaidi ya moja ya fibroid katika mda mmoja k**a zitatokea mahali tofauti tofauti kwenye uzazi wa mwanamke. Aina kuu za uvimbe kwenye kizazi(fibroids) ni k**a zifuatazo

Intramural fibroids; ni aina maarufu zaidi na zinawatokea zaid wanakwake. Aina hii ya fibroid hukua na kumea kwenye misuli ya ukuta wa uterus. Kadiri zinavokua basi husababisha kupanuka au kuvutika kwa kizazi na kusababisha dalili k**a hedhi ya muda mrefu inayoambatana na maumivu ya nyonga.

Subserosal fibroids: aina hii ya fibroids hukua nje ya ukuta wa mfuko wa mimba, wakati mwingine kuelekea kwenye kibofu cha mkojo. Aina hii ya fibroids huweza kusababisha maumivu ya chi ya mgongo kutokana na kwamba uvimbe huu unasukuma neva za uti wa mgongo na kusababisha presha kubwa kwenye eneo la chini ya mgongo.

Submucosal fibroids: aina hii ya fibroid hukua karibu na ukuta wa kizazi. Inaweza kusababisha bleed ya muda mrefu na shida kwenye kushika ujauzito.

Cervical fibroids: hizi hukua kwenye tishu za mlango wa kizazi ambao huitwa cervix. Hutokea mara chache sana ukilinganisha na aina zingine za fibroids.

Vihatarishi gani vinaongeza uwezekano wa kupata fibroids?
Mambo yafuatayo yanaongeza uwezekano kwa mwanamke kupata uvimbe kwenye kizazi

Kurithi: k**a mama au dada yako aliwahi kuugua tatizo hili basi wewe pia utakuwa kwenye hatari zaidi ya kupata uvimbe huu.
Umri: uvimbe kwenye kizazi (fibroids) hutokea zaidi kwa wanawake wanaokaribia kukoma hedhi kuanzia miaka 35 mpaka 40.
Lishe: matumizi ya vyakula vya wanga na sukari kupita kiasi huongeza hatari ya kupata fibroids
Uzito mkubwa na kitambi: wanawake wenye uzito mkubwa na kitambi wako kwenye hatari zaidi ya kupata fibroids .
Wanawake wenye shinikizo kubwa la damu
Matumizi ya njia za kupanga uzazi: k**a vidonge huongeza ukuaji wa fibroids kwani vidonge hivi huweza kupandisha homoni ya estrogen kwa wingi
Kubalehe mapema: wanawake wanaobalehe mapema na kuanza kupata hedhi chini ya miaka 10 wako kwenye hatari zaidi ya kuugua fibroids na
Wenye matatizo ya tezi ya Thairodi
Hatua saba za kuepuka na kutibu uvimbe kwenye kizazi (fibroids)
Hatua ya kwanza: Epuka vyakula vyote vinavyoongeza ukubwa wa tatizo: vyakula vya kupiga chini ni k**a vifuatavyo.
Vyakula vyenye mafuta mabaya na vilivyosindikwa: mfano nyama zilizosindikwa , baga na suausage huongeza mpambano (inflammation) na aleji. pia vyakula vilivyosindikwa vina kiasi kingi cha kemikali zinazowekwa ili kuongeza ladha hivo unapofanya uchaguzi wa nyama basi hakikisha unakula nyama kutoka kwa mnyama aliyefugwa kwa kula majani na siyo nafaka.
Maziwa yaliyosindikwa na kuhifadhiwa kwenye makopo: maziwa haya yana homoni nyingi za steroids na kemikali pia ambazo zinabadili ufanyaji kazi wa homoni zako za mwili na hivo kuongeza ukuaji wa fibroids.
Sukari: matumizi ya sukari kwa wingi iwe imesindikwa au ya asili huongeza mpambano kati ya tishu za mwili na kinga ya mwili na hivo kusababisha kuvimba au kututumka kwa tishu . hii huongeza maumivu na kupunguza uwezo wa kinga ya mwili. Unaweza kusoma vizuri uhusiano kati ya kuvurugika kwa homoni, kuongezeka uzito na uvimbe kwa kubonyeza hapa.
Wanga iliyokobolewa sana; katika kupambana na tatizo la uvimbe kwenye kizazi basi hakikisha unapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya vyakula vyenye wanga kwa wingi maana vyakula hivi hupandisha insulin nyingi kwenye damu na kuongeza hatari ya kupata uvimbe
Pombe na vinywaji vyenye caffeine. Matumizi makubwa ya pombe huongeza mcharuko au kututumka kwa tishu kwenye mwili . pombe pia huzorotesha kinga ya mwili na kusababisha uzito mkubwa na kuvurugika kwa homoni, unaweza kusoma makala yetu kuusu kuvurugika kwa homoni za k**e na suluhisho lake jikoni kwa kubonyeza hapa.
Hatua ya pili : Kula kwa wingi vyakula vya kukusaidia kutibu na kupunguza makali ya uvimbe.: vyakula hivi ni k**a.
Vyakula vilivyoandaliwa pasipo matumizi ya kemikali (organic foods), sababu ni k**a tulivoona hapo juu kwamba kemikali hizi zilizosheheni kwenye dawa za kuua wadudu zinaharibu mpangilio wa homoni na kusababisha seli za mwili kukua ovyo bila mpangilio. Kuhusu matunda na mbogamboga basi hakikisha unaosha kwa maji ya uvuguvugu yaliyochangnywa na vinegar hii husaidia kutoa kemikali za sumu zilizoganda kwa juu.
Mbogamboga za kijani : mboga za kijani zina viambata vinavyoondoa sumu kwenye mwili . pia mbogamboga za kijani zina Vitamin K kwa wingi sana ambazo husaidia katika kuganda kwa damu na hivo kusaidia kwenye bleeding.
Vyakula vyenye beta carotene kwa wingi na madini ya chuma: Mwili una uwezo wa kubadilisha beta carotene kuwa Vitamin A , na kazi ya vitamin A ni kujenga seli mpya zilizokufa na hivo kusaidia wenye fibroids.
Baadhi ya vyakula vyenye beta carotene kwa wingi ni Nyanya, karoti na spinach. Kutokana na kwamba fibroid husababisha wanawake kupoteza damu nyingi kwa wakati fulani hivo ni muhimu kutumia vyakula k**a maini, fogo, moyo ili kuongeza uzajishaji wa madini chuma ambayo husaidia katika utengenezwaji wa seli mpya nyekundu za damu.
Hatua ya tatu: Jaribu kutumia baadhi ya virutubisho kwa ajili ya kupungeza ukubwa wa uvimbe; hakikisha unapata ushauri wa daktari kabla ya kuanza kutumia virutubisho hivi,
Mafuta ya samaki(fish oil) au mafuta ya flaxseed, kijiko kimoja kwa siku inaweza kusaidia kpunguza mcharuko kwenye mwili na hivo kusaidia kupunguza uvimbe kwenye kizazi
Vidonge vya vitamin B complex: hii husaidia kurekebisha kiwango cha homoni ya estrogen kwenye mwili na hivo kupunguza ukuaji wa uvimbe
4. Hatua ya nne. Kunywa chai tiba(herbal tea) unaweza utembelea kwenye stoo yetu ili kuweka oda: chai tiba zipo aina nyingi baadhi ya chai hizi ni Pine pollen na Kuding tea, chai hizi husaidia kubalansi homoni zako na hivo kusaidia katika kutibu uvimbe.

5.Hatua ya tano, Tumia mafuta ya castor: unapopakaaa mafuta ya castor kwenye tumbo lako husaidia kuongeza usafirrishaji wa damu na hivo kurahisisha utolewaji wa sumu haraka kwenye mwili. Watafiti wengi wa tiba wanaamini kwamba mrundikano wa sumu ndio unaopelekea kukua kwa fibroids. Jaribu pia detox package yetu ndani ya siku 30 ili kusafisha sumu kwenye mwili.

6. Hatua ya sita: Jiepushe na mzingira hatarishi yenye sumu : mazingira yenye sumu mbalimbali k**a za kuua wadudu kwenye mazao, kemikali kwenye vyakula vya viwandani kuzuia ili visiharbike, kemikali za kuua magugu, na kemikali kwenye sabuni na mafuta , vyote hivi huchangia kukua kwa uvimbe kwenye kizazi (fibroids) kwa kuharibu mpangilio wa homoni. Na mwisho kabisa

7. Hatua ya saba: Fanya mazoezi ya kutosha walau mara 3 kwa week: Mazoezi husaidia kuzuia kutokea kwa uvimbe kwenye kizazi. Mazoezi hurekebisha presha ya damu, kuimarisha kinga, na kubalansi homoni zako

SABAB NYENGINE ZINAZOPELEKEA MWANAMKE KUTOSHIKA UJAUZITO . Katika ukurasa huu tutarejea kwenye mada kuu ya kuona sababu ...
03/06/2022

SABAB NYENGINE ZINAZOPELEKEA MWANAMKE KUTOSHIKA UJAUZITO . Katika ukurasa huu tutarejea kwenye mada kuu ya kuona sababu za ugumba au utasa kwa mwanamke na kutazama mapungufu katika mwili wa mwanamke yanayochangia tatizo hili. K**a ada, katika ukurasa mwingine tutaona njia zinazotumika kuondoa tatizo hili la mwanamke kukosa mtoto.

Tulisema kwamba ugumba ni hali ambapo mwanamme na mwanamke wamejamiiana kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kinga na bado mwanamke hakuweza kupata ujauzito. Tuliona kuwa hali hii inachangiwa na jinsia zote na si mwanamke peke yake k**a ilivyozoeleka kuamini hapo zamani. Ilibainishwa kuwa theluthi moja ya nyumba zenye tatizo hili huwa imeathirika kutokana na mapungufu ya mwanamme, theluthi nyingine kutokana na mwanamke na inayobakia inaathiriwa na matatizo au ya wote wawili au yale ambayo hayaeleweki.Tulishauri kuwa linapotokea tatizo hili, wote wawili wanatakiwa wapimwe ili kujua ni nani kati yao ndiye chanzo cha tatizo.

Sababu Za Mwanamke Kukosa Kizazi

Ili mwanamke apate mimba, sehemu zote za mwili wake zinazohusika na uzazi zinatakiwa zifanye kazi inavyotakiwa na katika hatua zote. Hatua katika utengenezaji wa mimba ni k**a zifuatazo:

1. Moja kati ya ovari mbili za mwanamke kuachia yai lililokomaa
2. Yai hii kusafirishwa na mrija wa uzazi (fallopian tube)
3. Mbegu za mwanamme kusafiri hadi kwenye cervix, kupitia tumbo la uzazi (uterus) hadi kwenye mrija wa uzazi, kulifikia yai na kulipevusha.
4. Yai lililopevushwa kusafiri kupitia mrija wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi (uterus).
5. Yai kunata kwenye ukuta wa uterus na kukua.

Ugumba kwa mwanamke unaweza kutokana na dosari katika hatua yo yote katika hizo tulizozitaja na mara niyingine kutokana na dosari katika hatua zaidi ya moja.

Pamoja na kuwa kuna sababu nyingi za mwanamke kutopata mimba, lakini sababu kuu tatu ndizo zinazohusika zaidi k**a tutakavyozielezea hapa chini.


Kushindwa Kuzalisha Mayai (Anovulation)


Hili ndilo tatizo ambalo linachangia ugumba kwa wanawake kwa asilimia 30 lakini kwa bahati nzuri asilimia 70 ya wanawake wenye tatizo hili hupata tiba na kufanikiwa kupata watoto. Mwanamke mwenye tatizo hili hutoa mayai mara chache au hatoi mayai kabisa. Chanzo cha tatizo huwa ni moja ya yafuatayo:

1. Matatizo Ya Homoni

Matatizo ya homoni ndiyo yenye mchango mkubwa zaidi kwenye kumfanya mwanamke ashindwe kuzalisha mayai. Uzalishwaji wa mayai hutegemea mchanganyiko wa homoni utakaofanya kazi kwa kuhusiana bila kuvurugwa katika utendaji wake wa kazi.

Dawa Ya Ugumba Kwa Wanawake – Bonyeza juu ya picha kusoma maelezo yake



Kuna matatizo ya aina tatu yanayoweza kuvuruga mpangilio huo.

Kuzalisha Mayai Yasiyokomaa:

Matatizo Ya Hypothalamus: Hypothalamus ni sehemu ya ubongo inayohusika na kutoa ishara kwa tezi ya pituitary (pituitary gland) ambayo nayo huamsha homoni za ovari zinazoruhusu yai kukomaa. Hypothalamus isipofanya kazi yake, mayai hushindwa kufika ukomavu. Asilimia 20 ya dosari za ukomavu wa mayai husababishwa na matatizo ya hypothalamus.

Matatizo Ya Pituitary Gland: Tumeona hapo juu kuwa tezi ya pituitary inahusika katika kukomaza mayai. Endapo pituitary itatoa homoni kwa kiwango kidogo au kikubwa kupita kiasi, ovari zitashindwa kuzalisha na kutoa mayai ipaswavyo. Hali hii hutokea pale tezi hii inapoharibiwa kwa ajali, kunapotokea uvimbe ndani yake au kunapokosekana ulingano wa k**emikali ndani ya tezi hiyo.

2. Makovu Kwenye Ovari

Uharibifu kwenye ovari unaweza kusababisha ovari hizi kushindwa kuzalisha mayai. Operesheni za mara kwa mara hujenga makovu kwenye ovari hizo na kuzifanya zishindwe kuzalisha mayai. Maambukizi ya magonjwa huweza pia kusababisha ovari kushindwa kuzalisha na kutoa mayai.

3. Kukoma Hedhi Mapema

Kukoma hedhi mapema ni tatizo ambalo halijaeleweka vizuri kisayansi. Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao za kawaida kwenye umri usiotegemewa. Dhana moja ni kuwa hifadhi yao ya mayai imekwisha au nyingine ni kuwa inatokana na wanawake hawa kuwa wenye historia ya kuwa wanariadha waliokuwa na miili yenye uzito mdogo na waliofanya mazoezi ya nguvu kwa muda mrefu. Kuna uwezekano kuwa kukoma hedhi mapema ni suala la urithi.

4. Matatizo Ya Follicle

Kuna tatizo lisilo na maelezo ya kisayansi “unruptured follicle syndrome” ambapo mwanamke hutengeneza mfuko wa kawaida wa yai wenye yai ndani yake kila mwezi lakini mfuko huo hugoma kupasuka na kuachia yai. Hivyo kwamba, yai hubaki ndani ya ovari na utolewaji wa yai nje ya ovari kutotokea.

Mirija Ya Uzazi (Fallopian Tubes) Kushindwa Kufanya Kazi Vizuri


Magonjwa katika mirija ya uzazi huathiri asilimia 25 ya wanafamilia ambapo tatizo laweza kuwa dogo la kunata kwa yai au kubwa la mirija kuzibwa kabisa. Tiba kwa matatizo ya mirija ya uzazi mara nyingi ni upasuaji. Matatizo yanayopelekea kuziba kwa mirija ya uzazi ni k**a yafuatayo:

1. Maambukizi Ya Wadudu

Maambukizi ya virusi na bacteria yanayoenezwa kwa ngono husababisha makovu na uharibifu, kwa mfano, maambukizi ya Hydrosalpinx yanayosababisha mirija ya uzazi kuziba pande zote na kujaa maji .

2. Magonjwa ya Tumbo

Magonjwa ya appendicitis na colitis huleta madhara kwenye tumbo ambayo yanayoweza kuiathiri mirija ya uazazi kwa kujenga makovu au kuiziba.

3. Upasuaji

Hii ni sababu kubwa ya magonjwa na uharibifu wa mirija ya uzazi. Upasuaji wa kwenye maeneo ya kinena na tumbo huweza kusababisha uharibifu utakaozuia upitaji wa yai.

4. Mimba Ndani Ya Mirija Ya Uzazi (Ectopic Pregnancy)

Mimba zinazotunga ndani ya mirija ya kizazi huweza kuleta uharibifu kwenye mirija hiyo hata k**a tahadhali ya juu itachukuliwa kuziondoa.

5. Matatizo Ya Kuzaliwa Nayo

Mara chache huweza kutokea kuwa mwanamke akazaliwa akiwa na dosari katika mirija yake ya uzazi.

Endometriosis
Endometriosis ni kuota kwa seli (endometrial cells) zinazofanana na zile zinazotanda ndani na nje ya mfuko wa uzazi (uterus) kwenye eneo nje ya mfuko wa uzazi. Endometrial cells ndizo zinazoufunika mfuko wa uzazi na seli hizi hubadilishwa kila mwezi wakati wa hedhi. Seli hizi huweza kuota kwenye maeneo mengine yaliyo nje kabisa ya mfuko wa uzazi na huitwa endometriosis implants. Maeneo ambayo seli huweza kuota ni kwenye ovari, mirija ya uzazi (fallopian tubes), kuta za nje za nyumba ya uzazi, utumbo, pelvis, kuma , cervix, kibofu na mara chache kwenye maini, mapafu na ubongo.

Endometriosis imegundulika zaidi kwenye kundi la wanawake wenye umri kati miaka 25 na 35, ingawa mara chache imeonekana kwa wasichana wadogo wa miaka k**a 11. Endometriosis ni nadra kuonekana kwa wanawake waliokoma hedhi. Wanawake warefu , wembamba wenye uzito mdogo huonekana zaidi na tatizo hili. Kupata ujauzito katika umri mkubwa sana, kutozaa na kukoma siku mapema huongeza uwezekan wa kutokea endometriosis.

Kuota kwa seli hizi za ziada – na tendo la kuziondoa kwa operesheni – huweza kusababisha makovu ambayo huweza kuzuia yai la mwanamke lisiungane na mbegu ya mwanamme. Kuathirika kwa utando huu juu ya uterus huweza kuzuia kutungwa kwa yai lililopevushwa.

Sababu Nyinginezo

1. Sababu Za Kitabia

Baadhi ya tabia zetu huathiri afya zetu ikiwa ni pamoja na afya ya viungo vya uzazi na kupunguza au kuondoa uwezo wetu wa kuzaa watoto. Bahati nzuri tabia hizi zinaweza kudhibitika.
Chakula Na Mazoezi: Ili tuwe na uwezo mzuri wa kuzaa watoto tunahitaji kupata chakula kizuri na kuipa miili yetu mazoezi ya kutosha. Wanawake wenye unene wa kupindukia au uzito mdogo sana wanapata shida kushika mimba.
Uvutaji Wa Sigara: Uvutaji wa sigara umethibitika kupunguza kiwango cha mbegu (low s***m count) kwa wanaume, kuongeza uwezekano wa mimba kutoka, kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo au kabla ya wakati (njiti) kwa wanawake.
Pombe: Unywaji wa pombe huongeza uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye matatizo na unywaji uliozidi huweza kuleta ugonjwa, Fetal Alcohol Syndrome. Kwa mwanaume, pombe hupunguza kiwango chake cha mbegu.
Madawa: Madawa k**a bangi (ma*****na) hupunguza kiwango cha mbegu kwa wanaume. Utumiaji wa co***ne kwa wanawake huathiri figo za watoto watakaozaliwa.

2. Sababu Za Kimazingira

Uwezo wa mwanamke kutunga mimba unaweza unaweza kuathiriwa na uwepo wake kwenye mazingira yenye sumu au kemikali. Hii inaweza kuwa kwenye mazingira ya kazi au sehemu anayoishi. Baadhi ya kemikali zilizobainika na kuandikwa kuwa
zinapunguza uwezo wa mwanamke kupata mimba ni:
Lead – husababisha mimba kutoka. Tiba – tiba ya mionzi ya mara kwa mara na chemotherapy huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na matatizo ya ovari. Ethylene Oxide – kemikali inayotumika kuua wadudu kwenye vifaa vya upasuaji na kutengenza dawa za kuulia wadudu huleta dosari kwenye mimba changa na kusababisha mimba kutoka. Dibromochloropropane (DBCP) – Kemikali inayopatikana kwenye dawa za kuulia wadudu husababisha mwanamke kukoma hedhi mapema.

Katika mfululizo wa mada hii, tumejadili maana ya mzunguko wa hedhi wa mwanamkena kuona awamu nne za mzunguko wa hedhi kwa mwanamke. Tumeona pia sababu za ugumba kwa mwanamme. Tumejadili kwa kina sababu za mwanamke kukosa mtoto na kuelezea tiba za ugumba kwa mwanamke.

Katika ukurasa unaofuata “Tiba Ya Ugumba Kwa Wanawake” tutaona jinsi ya kuondoa au kupambana na tatizo hilo.

Usisite kutuuliza maswali yako au kuomba ushauri kuhusu matatizo ya kukosa watoto. Tumia njia yo yote iliyo rahisi kwako baina ya hizi tulizoziorodhesha hap
Kwa maelezo na ushaur zaid kuhus elimu ya afya ya mwanamke tafadhali wasiliana na nasi kwa sim no 0629771737 /0715217198 utapatiwa ushaur bure kabisaa bila gharama yoyote

SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA NA TIBA ZAKETatizo la kutopata mimba linawasumbua wengi na huwapata familia kadhaa ka...
03/06/2022

SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA NA TIBA ZAKE

Tatizo la kutopata mimba linawasumbua wengi na huwapata familia kadhaa katika jamii, huweza kumpata mtu mmoja kati ya wanandoa 12 na ni tatizo linalowapata watu zaidi ya milioni 24 duniani kote.

Ugumba ni hali ya kutoweza kupata ujauzito katika kipindi cha mwaka mmoja au zaidi kwa wenzi ambao wamekuwa wakifanya mapenzi bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango. Mtiririko wa upataji ujauzito ni k**a ifuatavyo;

Baada ya mwezi mmoja wa ndoa uwezo wa kushika ujauzito ni asilimia 20, baada ya miezi mitatu ya ndoa ni asilimia 50, baada ya miezi sita ya ndoa ni asilimia 75 na baada ya miezi 12 ni asilimia 90 mwanamke huweza kupata ujauzito.

Hali hii inaweza kutokea kutokana na tatizo kwa mwanaume au mwanamke, ingawa baadhi ya watu wamekuwa wakidhani wanawake peke yao ndio ambao hupata tatizo hilo.

Tatizo hili limegawanywa katika vipengele viwili kimoja ni kile ambacho mwanamke hushindwa kupata mimba baada ya mwaka mmoja wa kufanya tendo la ndoa na mume wake bila kutumia kinga kwa mwanamke mwenye umri chini ya miaka 35 (primary infertility).

Kipengele cha pili ni kile kijulikanacho k**a 'secondary infertility' ambapo mwanamke hushindwa kubeba mimba wakati siku za nyuma alishawahi kupata ujauzito.

Tatizo la ugumba huweza kupatiwa matibabu na kuisha.

KUNA TAFAUTI GANI KATI YA UGUMBA NA UTASA?

Tofauti na ugumba, utasa ni hali ya mwanamke kutoweza kushika ujauzito kabisa au mwanaume kutoweza kusababisha ujauzito kwa mwanamke kabisa.

Mtu tasa hana uwezo wa kupata mimba au kumpa mwenzi wake mimba kabisa, wakati mgumba ana uwezo wa kuja kupata mimba iwapo tatizo litaondolewa.

NINI HUSABABISHA UGUMBA?

Kuna sababu mbalimbali ambazo hupelekea ugumba kutokea kwa mwanaume au mwanamke.

WANAUME
Ugumba kwa wanaume hutokana na tatizo katika mbegu za kiume, manii kuwa kidogo, manii kushindwa kutembea, manii kuwa na umbo lisislo la kawaida au kuziba kwa mijira ya mbegu za kiume.

Tatizo kwenye mbegu za kiume linaweza kutokana na;

- Uvutaji wa sigara
- Dawa za kulevya k**a matumizi ya bangi kwa wingi,
- Mionzi (radiations)
- Unywaji wa pombe
- Kemikali k**a DDT, risasi (lead)
- Kufanya kazi mazingira yenye joto kali k**a viwanda vya chuma.
- Kuziba kwa mirija ya mbegu za kiume kutokana na magonjwa ya zinaa

WANAWAKE
Tatizo la ugumba husababishwa na sababu kuu mbili:

- Kuziba kwa mijrija ya kupitisha mayai
- Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi au kutoa mayai isiokuwa na nguvu (lazy egg).

Mirija ya kupitisha mayai inaweza kuziba kutokana na;

- Ugonjwa wa Pelvic Inflammatory Disease (PID) ambao unatokana na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa k**a kisonono na klamidia.
- Mirija ya mayai kujaa maji
- Utoaji mimba usio salama (unsafe abortions)
- Upasuaji maeneo ya kiunoni
- Ugonjwa wa endometriosis

Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi inaweza kutokana na;

- Umri mkubwa wa mwanamke, hasa miaka 35 – 40 na kuendelea.
- Uvutaji wa sigara
- Saratani ya Ovari
- Mionzi (radiations)
- Ugonjwa wa Polycystic ovarian disease (Ovarian Cyst)

Sababu nyingine za ugumba kwa mwanamke zinaweza kuwa;

- Makovu katika mji wa uzazi kutokana na kutoa mimba.
- Mabonge ya kizazi (uterine fibroids)
- Kuziba kwa shingo ya uzazi
- Kulegea shingo ya uzazi
- Kisukari
- Matatizo ya tezi ya shingo (hyperthyroidism)
- Kufanya mazoezi ya kupitiliza (excessive exercising)

VIPIMO VYA KUJUA UGUMBA

Vipimo mbalimbali vinapatikana ili kuwezesha kugundua chanzo cha ugumba. Licha ya uwezo wa vipimo hivi, zaidi ya asilimia 10 ya watu wenye tatizo hili chanzo kinaweza kisijulikane kabisa. Ni vizuri kwa wenzi wote wawili wenye tatizo hili kuonana na daktari kwa ajili ya ushauri na vipimo.

KWA WANAUME HUFANYIKA;

Kipimo cha manii (seminalysis) kuona k**a manii zipo za kawaida na kwa kiwango kinachoatakiwa. Manii huchukuliwa kwa kondomu maalum wakati wa kufanya mapenzi au kwa kupiga punyeto na kisha kuchunguzwa kwa darubini.

Homoni za kiume kwenye damu; kipimo hiki hupima homoni za testosterone na Follicle Stimulating Hormone(FSH) ambazo huusika katika utengenezaji wa mbegu za kiume.

KWA WANAWAKE KUNA VIPIMO VINGI HUWEZA KUFANYIKA VIKIWEMO;

- Hysterosalpingography – hutazama mirija ya uzazi (Fallopian tubes) k**a imeziba au la. Pia huonesha k**a tumbo la uzazi lina vivimbe.

- Ultrasound – kipimo hiki huonesha k**a kuna vivimbe kwenye tumbo la uzazi, pia kwenye ovari k**a kuna magonjwa yanayoweza kusababisha ugumba k**a Polycystic Ovarian Syndrome.

- Homoni za k**e katika damu – kipimo hiki hupima homoni za 'Oestrogen' na 'Follicle stimulating hormone' ambazo huusika kwenye kuandaa yai la uzazi kutoka kwenye ovari na upandikizaji kwenye mji wa uzazi.

- Endometrial biopsy – tishu za mji wa uzazi huchukuliwa kuchunguza k**a yai la uzazi limetoka. Pia huweza kuonesha k**a kuna saratani ya mji wa uzazi au vinyama kwenye mji wa uzazi.

MATIBABU YA UGUMBA

Matibabu ya ugumba huhusishwa wenzi wote wawili, mwanaume na mwanamke. Yanahitaji uvumilivu na uelewa kwani wakati mwingine yanaweza yasiwe na mafanikio haraka au kabisa k**a tunavyotarajia. Kuna njia mbalimbali za kutibu ugumba, hizi zote zikijumuisha kuondoa tatizo linalosababisha mimba ishindwe kutunga au kutumia njia za kusaidia mimba itunge.

Njia za matibabu ya ugumba hujumuisha:

UPASUAJI
Mirija iliyoziba, vivimbe kwenye mji wa uzazi au kuta za uzazi kushik**ana huweza kutibiwa kwa njia za upasuaji. Matibabu haya husaidia kuongeza uwezekano wa wenzi kupata mtoto.

DAWA
Mirija iliyoziba, vivimbe kwenye mji wa uzazi au kuta za uzazi kushik**ana huweza pia kutibiwa kwa Dawa mara nyingine. Matatizo ya ugumba yanayotokana na ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi huweza kutibiwa kwa dawa pia. Dawa hizi hutumika kuziwezesha ovari kutoa mayai ya uzazi ili yawe tayari kurutubishwa. Mara nyingi huweza kusababisha kutoa mayai mengi katika mzunguko mmoja na kusababisha ujauzito wa watoto wengi (mapacha au zaidi) pale yanaporutubishwa.

TEKNILOGIA SAIDIZI ZA UZAZI (Assistive Reproductive Technologies).

Hizi ni njia za kitaalamu ambazo zinatumika kusaidia wenzi kupata ujauzito kutokana na tatizo kwa mwanaume au mwanamke. Njia hizi ni k**a 'Artificial Insermination' na 'In Vitro Fertilization'.

- Artificial Insermination; Njia hii hutumika pale ambapo mbegu za kiume zipo kwa kiasi kidogo. Mbegu za kiume hukusanywa na kuingizwa kwenye mji wa uzazi kwa njia za kitaalamu.

- In Vitro Fertilization; Njia hii hutumika hasa pale mirija ya mwanamke imeziba kabisa. Mayai na mbegu za kiume hukusanywa kitaaalamu na kisha yai kuchavushwa. Baada ya hapo yai lililochavushwa hupandikizwa kwenye mji wa uzazi.

Ugumba huathiri wanaume kwa wanawake wa kiwango kinachofanana, hivyo ni muhimu kwa wenzi wote wawili kushiriki katika matibabu.

Ugumba huathiri wenzi wengi kisaikolojia kwa kuleta hasira, majuto, msongo wa mawazo na hata kusababisha mvurugano katika mahusiano yao. Katika nchi zetu za kiafrika, wanawake wamekuwa wahanga wakubwa wa tatizo hili. Ni vizuri wenzi washirikiane katika hili, kwa kupeana moyo na kufuatilia matibabu kwa pamoja. Matibabu yanaposhindwa kabisa kuleta mafanikio, wenzi wanaweza kuasili mtoto/watoto k**a watakuwa na utayari.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wetu wa Facebook wa 'Al- Shifaa Natural Remedie' kupata mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya mwanadamu na tiba mbalimbali. Usikose kuweka LIKE endapo utafurahishwa na mada hizo.

JEE, UNA TATIZO LA UGUMBA?

K**a una tatizo hili na umeshindwa kulipatia ufumbuzi, wasiliana nasi.

Kwa mawasiliano nasi tuma ujumbe mfupi au piga simu kwenye nambari zifuatazo
0629771737 /0715217198

Ikiwa wewe ni mwanaume na unasumbuliwa na tatizo la ugumba au hauko sawa katika mpangilio wako wa uzazi nina habar njema...
19/04/2022

Ikiwa wewe ni mwanaume na unasumbuliwa na tatizo la ugumba au hauko sawa katika mpangilio wako wa uzazi nina habar njema
Leo nitashea na wewe

Sababu tano zinazosababisha ugumba miongoni mwa wanaume

Wanaume wengi hunyamaza wakati wanapoanza kuathiriwa na tatizo la kushindwa kutekeleza wajibu wao katika ndoa ikiwemo tatizo la kushindwa kushiriki tendo la ndoa.

Hivyobasi mara nyingi hulazimika kujiondolea lawama hiyo na badala yake kusema kwamba kizazi cha wake zao ndicho chenye tatizo.

Utafiti umeonesha kwamba wanaume wenye kati ya umri wa miaka 18 hadi 35 ni asilimia 15 ya idadi ya watu.

Kwanini baadhi ya vifo hutokea ghafla wakati wa tendo la ndoa?
‘Walitulazimisha tufanye mapenzi hadi mara 15 kwa siku’
Vilevile wanaume wenye zaidi ya umri wa miaka 40 ni asilimia 40 ya wale wasioweza kuwatosheleza wake zao kindoa kutokana na tatizo linaloathiri sehemu zao za siri. (uume kushindwa).

Hali hiyo humfanya mwanaume kuhisi kukejeliwa na jamii ambayo hubeza hali hiyo.

Mwanaume au mwanamke aliye katika hali hiyo pia anaweza kukejeliwa au kupokea shutuma chungu nzima kutoka kwa jamii iwapo siri yake itajulikana nyumbani ama mahala popote pale.

Kutokana na hilo wanaume ambao hujipata katika hali hiyo ya kiafya hupendelea sana kutoshiriki katika mjadala kuhusu suala hilo kwasababu hujihisi kukatishwa tamaa.

Maelezo ya sauti,
Upungufu wa nguvu za kiume na athari za matumizi ya mitishamba isiyoidhinishwa kisayansi

Kunapotokea hali k**a hiyo , magonjwa mengine pia huanza kumwathiri mwanaume k**a huyo na mara nyingi huogopa kushiriki na wake zao katika tendo la ndoa.

Na iwapo mwanaume anashindwa kutekeleza wajibu wake nyumbani, humfanya mke wake kuanza kumshuku na hivyobasi kusababisha kuzuka kwa ugomvi wa mara kwa mara bila sababu.

Daktari Rasheed Adedapo Abassi, kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani ana uzoefu wa miaka 19 katika afya ya wanaume.

Anaelezea kile kinachosababisha mwanamke kushindwa kushika ujauzito ,tiba yake na jinsi ya kujilinda na hali hiyo.

Je ina maana gani mwanamume kushindwa kushiriki tendo la ndoa na mke wake?
Hali ya maumbile nyeti kushindwa kuwa tayari, kwa kitaalamu Erectile dysfunction (ED) ni wakati ambapo mwanamume hawezi kushiriki katika tendo la ndoa kwa dakika 15 mfululizo.

Utafiti umeonesha kwamba iwapo mwanaume ana uwezo wa kushiriki katika tendo la ndoa, sehemu yake ya siri huonesha mihemko nyakati za alfajiri anapoamka.

Lakini daktari Abass anasema kwamba iwapo sehemu ya siri ya mwanaume haina mihemko, au iwapo hawezi kushiriki katika tendo la ndoa basi huenda yeye ana tatizo la ugumba.

Kuna sababu kadhaa kwanini hali hii huwakumba waathiriwa.

1.Ukosefu wa homoni za kiume za kutosha mwilini:
Testosterone ni homoni za kiume zinazowafanya wanaume kuhisi kuwa wanaume huku estrogen zikiwa homoni za k**e ambazo humsaidia mwanamke kupata ujauzito .

K**a wanaume, viwango vya homoni za oestrogen katika mwili wa mwanamke hupungua wakati mwanamke anapofikisha umri wa miaka 50.

Maelezo ya picha,
Wanaume wengi hunyamaza wakati wanapoanza kuathiriwa na tatizo la kushindwa kutekeleza wajibu wao katika ndoa ikiwemo tatizo la kushiriki katika tendo la ndoa.

Kwa upande wa wanaume viwango vya homoni za kiume havipungui , lakini hukabiliwa na changamoto ambazo mara nyingi hupuuzwa.

2.Msongo wa mawazo:
Shinikizo la kiakili ni miongoni mwa sababu kuu zinazosababisha ugumba miongoni kwa wanaume. Msongo wa mawazo unaweza kutokea iwapo mwanaume hana kazi, iwapo mwanaume hana fedha ama iwapo kuna changamoto katika ndoa yake ama kutoka kokote kule.

Dalili hizi ni tofauti na zile za kufanya mazoezi , kwasababu mazoezi husaidia moyo kusukuma damu vyema katika misuli muhimu. Sonona husababishwa na mgando wa damu kila mahali mwilini.

3.Kushiriki mazoezi mbali na tendo la ndoa mara kwa mara:
Hili ni suala linalohitaji msisitizo ili kuzuia ugumba. Mtu anapaswa kujifunza kufanya mazoezi kwa muda mfupi kila siku.

''Je Unajua mazoezi ambayo huwashauri wagonjwa wangu kufanya? Ni kushiriki katika tendo la ndoa mara kwa mara.

Na kuna utafiti unaothibitisha hili, ambao naweza kusema kwamba ni ushahidi ulio sawa'', alisema Dkt Abbas.

4.Unyanyasaji wa kingono:

Dkt. Abass anawashauri wanaume kushiriki katika tendo la ndoa mara 21 kwa mwezi . Inadaiwa kwamba kushiriki katika tendo la ndoa mara kwa mara kunasaidia kuzuia saratani ya tezi dume.

5.Ukosefu wa maji safi

Suala hili linaonekana k**a la kushangaza kwa watu wengi, kulingana na Dkt Abbas.

Hatahivyo , anaelezea kwamba ukosefu wa maji safi , ambayo hayana virutubisho , huathiri afya ya uzazi ya wanaume. Aliongezea kwamba serikali imelazimika kuhakikisha uwepo wa maji safi ya kunywa kwa kuweka dawa k**a vile Fluoride, Calcium na Selenite.

Inahakikisha kwamba maji yana virutubisho vyote ili afya ya wanaume iwe bora.

Si hayo tu na mengine meng kuhusu afya ya uzazi
Waspp no(0715217197)
Au click batan ya wasap chini ya post hii pia usisahau kushea kwa faida ya wengine

Checkout the full domain details of 1.uk. Click Buy Now to instantly start the transaction or Make an offer to the seller!

Address

Mkoani Pemba
Chake Chake
1203

Opening Hours

09:00 - 17:00

Telephone

+255629771737

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maabady.003 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram