AFYA Care

AFYA Care Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from AFYA Care, Medical and health, kimara stop over, Dar es Salaam.

NJIA RAHISI YA KUPUNGUZA UZITO, KITAMBI NA NYAMA UZEMBE✔ Punguza vyakula vya mafuta na sukari✔ Kula mboga za majani na m...
12/02/2026

NJIA RAHISI YA KUPUNGUZA UZITO, KITAMBI NA NYAMA UZEMBE

✔ Punguza vyakula vya mafuta na sukari
✔ Kula mboga za majani na matunda kila siku
✔ Kunywa maji ya kutosha (glasi 6–8)
✔ Tembea au fanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku
✔ Epuka kula usiku sana
✔ Lala muda wa kutosha

🔥 Anza leo – mwili wako ni uwekezaji wako!
Usisubiri kuumwa ndipo ubadilike.




Dalili 9 za Awali za Saratani ya Mlango wa Kizazi (Cervical Cancer) Ambazo Wanawake Wengi Huzipuuza 👇👇👇1.Kutokwa na damu...
28/01/2026

Dalili 9 za Awali za Saratani ya Mlango wa Kizazi (Cervical Cancer) Ambazo Wanawake Wengi Huzipuuza 👇👇👇

1.Kutokwa na damu isiyo ya kawaida
Hasa kati ya hedhi au baada ya tendo la ndoa.

2.Kutokwa na damu baada ya kukoma hedhi
Hata kidogo, ni ishara ya hatari.

3.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
maumivu yasiyo ya kawaida au yanayoendelea.

4.Uchafu ukeni wenye harufu mbaya au una rangi ya kahawia/kijani.

5.Maumivu ya chini ya tumbo au nyonga
Yanayodumu bila sababu ya wazi.

6.Hedhi nzito au ndefu kuliko kawaida
. mabadiliko makubwa ya mzunguko wa hedhi.

7.Kuhisi uchovu wa kudumu hata bila kufanya kazi nzito.

8.Kupungua uzito bila sababu , mwili kudhoofika taratibu.

9.Maumivu ya mgongo au miguu hasa yakifuatana na dalili nyingine.

⚠️ Muhimu: Dalili hizi zinaweza kufanana na magonjwa mengine, lakini kupima mapema huokoa maisha.

👉 Fanya uchunguzi wa mlango wa kizazi mara kwa mara.

Kwa ushauri na tiba sahihi wasiliana nasi 0765343998



UNASUMBULIWA NA MENO KUUMA, KUFA GANZI AU KUTOBOKA?USING'OE JINO NJOO UPONE NA DAWA ASILIA Kwa ushauri na tiba sahihi wa...
27/01/2026

UNASUMBULIWA NA MENO KUUMA, KUFA GANZI AU KUTOBOKA?
USING'OE JINO NJOO UPONE NA DAWA ASILIA

Kwa ushauri na tiba sahihi wasiliana nasi 0765343998




‎✏️Tezi dume ni kiungo cha uzazi cha mwanaume kinachosaidia katika utengenezaji wa mbegu za uzazi (manii) na homoni ya t...
27/01/2026

‎✏️Tezi dume ni kiungo cha uzazi cha mwanaume kinachosaidia katika utengenezaji wa mbegu za uzazi (manii) na homoni ya testosterone.

‎✏️Kwa ufupi:
‎👉 Tezi dume = korodani (te**es)

‎✏️Kazi za tezi dume:

‎🧬 Hutengeneza mbegu za uzazi (manii)

‎💪 Hutengeneza homoni ya kiume (testosterone)

‎🧔 Huchangia sifa za kiume k**a:
‎ .sauti nzito
‎ .ndevu
‎ .misuli
‎ .hamu ya tendo la ndoa

‎✏️Tezi dume zipo wapi?

‎ .Zipo ndani ya mfuko wa korodani

‎ . (sc***um) chini ya uume.

‎Kuna pia tezi dume (prostate), ambayo:

‎.Husaidia kutengeneza maji ya mbegu
‎Iko ndani ya mwili, karibu na kibofu cha mkojo

‎⚠️ Watu wengi huchanganya:
‎Tezi dume (korodani)
‎Tezi dume – prostate

Kwa ushauri na tiba wasiliana nasi 0765343998



Kamwe Usipuuzie tatizo dogo maana baadae itakuletea madhara usiyotarajia kiufupi zingatia afya yako . Na kuitwa mama ni ...
27/01/2026

Kamwe Usipuuzie tatizo dogo maana baadae itakuletea madhara usiyotarajia kiufupi zingatia afya yako . Na kuitwa mama ni wajibu wako wewe mwanamke na k**a changamoto unayo usisite kunitafuta

Kwa ushauri na tiba wasiliana nasi 0765343998



PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni chanzo kikubwa cha mimba kutoka kwa baadhi ya wanawake kwa sababu huathiri moja kwa...
23/01/2026

PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni chanzo kikubwa cha mimba kutoka kwa baadhi ya wanawake kwa sababu huathiri moja kwa moja viungo muhimu vya uzazi.

‎ Hivi ndivyo inavyosababisha mimba kutoka 👇

‎ 1. Maambukizi hufika kwenye mfuko wa uzazi
‎ PID husababishwa na bakteria wanaopanda kutoka uke hadi:
‎-mfuko wa uzazi
‎-mirija ya uzazi
‎ - ovari
‎Maambukizi haya husababisha uvimbe na majeraha kwenye mfuko wa uzazi, hivyo mimba hushindwa kujishikiza vizuri.

‎ 2. Uvimbe huathiri placenta
‎Kwa mwanamke mwenye mimba, PID inaweza:
‎ kuharibu sehemu ya placenta
‎kupunguza damu na virutubisho vinavyomfikia mtoto
‎Hii husababisha mtoto kushindwa kukua na mimba kutoka.

‎3. Maambukizi husababisha uchochezi (inflammation)
‎Uchochezi mkali:
‎ husababisha mfuko wa uzazi kusinyaa
‎husababisha maumivu na kutokwa damu
‎Hatimaye mfuko huanza kumsukuma mimba itoke.


‎🔴 4. PID isipotibiwa mapema
‎Ikiwa PID haikutibiwa kabla au wakati wa mimba:
‎.bakteria huendelea kushambulia mfuko wa uzazi
‎.hatari ya mimba kutoka huongezeka sana, hasa miezi ya mwanzo.

‎⚠️ Dalili za PID kwa mjamzito (hatari)

‎ .maumivu ya tumbo la chini

‎ .homa

‎ .chafuuchafu wenye harufu mbaya

‎ .kutokwa damu isiyo ya kawaida

‎✏️Nini ufanye
‎ . Pima mapema k**a una dalili za PID

‎ .Anza matibabu haraka kabla ya
‎ kushika mimba au mara tu unapogundua mimba
‎Hudhuria kliniki ya wajawazito mapema

‎📌 Ujumbe wa muhimu:
‎PID ni ugonjwa unaotibika, lakini ukichelewa kutibiwa unaweza kusababisha mimba kutoka au ugumba

Wasiliana nasi Kwa ushauri na tiba 0765343998




21/01/2026
✏️ UTAHIDI WA AFYA – UTI Sungu (Urinary Tract Infection)UTI sungu ni nini?         UTI sungu ni maambukizi ya njia ya mk...
21/01/2026

✏️ UTAHIDI WA AFYA – UTI Sungu (Urinary Tract Infection)

UTI sungu ni nini?
UTI sungu ni maambukizi ya njia ya mkojo yanayosababisha maumivu, kukojoa mara kwa mara, na kuharibu figo ikiwa hayatatibiwa.

✏️Dalili na Madhara Makubwa:

🩸 Maumivu Makali: Maumivu wakati wa kukojoa, maumivu ya chini ya tumbo au mgongoni.

🩸Kukojoa Mara kwa Mara: Hata kidogo mkojo kinapojitokeza, unahisi haja ya kukojoa mara kwa mara.

🩸 Mkojo wa Rangi Mbaya: Mkojo unaweza kuwa na harufu mbaya, rangi ya njano/kahawia, au hata damu.

🩸 Maambukizi ya Figo: UTI zisizotibiwa zinaweza kuenea kwenye figo, kusababisha homa, baridi, maumivu makali ya mgongo, na figo kudhoofika (pyelonephritis).

🩸Hatari kwa Wajawazito: Mwanamke mjamzito anayepata UTI sungu anaweza kuathiri afya yake na ya mtoto.

🩸 Kuathiri Uhai wa Kijamii: Maumivu na kukojoa mara kwa mara vinaweza kuingilia maisha ya kila siku, usingizi, na kazi.

✏️Sababu za UTI Sungu:
Kutokufuata usafi wa sehemu za siri 🧼
Kukojoa kidogo au kujizuia kukojoa 🚽
Maambukizi ya bakteria kutoka sehemu za siri au kwa nyendo zisizo safi
Mfumo dhaifu wa kinga mwilini

✏️Ushauri Muhimu:
Kunywa maji mengi kila siku 💧
Kutibu mapema kwa madaktari 💊
Kuepuka kujizuia kukojoa
Kufanya usafi wa sehemu za siri kila siku
Kufuatilia dalili na kuripoti mara moja kwa daktari

📞 Ushauri na Tiba Sahihi: 0765343998


Wanawake wanaweza kutoka uchafu (maji/ute) sehemu za siri wenye harufu kali kwa sababu mbalimbali, zikiwemo hizi 👇🏽‎‎🔴 S...
19/01/2026

Wanawake wanaweza kutoka uchafu (maji/ute) sehemu za siri wenye harufu kali kwa sababu mbalimbali, zikiwemo hizi 👇🏽

‎🔴 Sababu kuu

‎Maambukizi ya bakteria (Bacterial Vaginosis – BV)
‎👉 Harufu kali k**a samaki 🐟, uchafu wa rangi ya kijivu au mweupe.
‎Fangasi (Candida)
‎👉 Uchafu mweupe k**a mtindi 🥛, kuwasha sana (mara nyingi harufu si kali sana).
‎Maambukizi ya zinaa (STI)
‎👉 K**a Trichomonas, Kisonono, Klamidia
‎👉 Uchafu wa kijani/manjano, harufu mbaya, maumivu wakati wa kukojoa au kujamiiana.
‎Usafi usio sahihi wa sehemu za siri
‎👉 Kutumia sabuni kali, dawa za kuingiza ukeni, au kutosafisha vizuri.
‎Mabadiliko ya homoni
‎👉 Kipindi cha hedhi, ujauzito, au matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango.
‎Kubaki na pedi/tampon muda mrefu
‎👉 Husababisha bakteria na harufu mbaya

‎⚠️ Dalili za hatari

‎. Harufu kali sana isiyoisha
‎. Uchafu wa rangi isiyo ya kawaida
‎. Maumivu ya tumbo la chini
‎. Kuwasha au kuungua sehemu za siri
‎ Ukiona dalili hizi, ni muhimu kumuona mtaalamu wa afya mapema

‎🩸Ushauri wa kujikinga

‎. Osha sehemu za siri kwa maji safi (nje tu)
‎. Epuka sabuni kali na dawa za kuingiza ukeni
‎. Badilisha pedi mara kwa mara
‎. Vaа chupi za pamba
‎. Fanya vipimo kabla ya kutumia dawa

‎📌 Kumbuka: Uchafu wenye harufu kali si wa kawaida — unatibika endapo utapata tiba sahihi mapema

Kwa mtu atakae chukua package ya uzaziTunatoa ofa ya  punguzo na kwa wewe ambaye unataka kusafisha na kulinda uke.....Wa...
18/01/2026

Kwa mtu atakae chukua package ya uzazi
Tunatoa ofa ya punguzo na kwa wewe ambaye unataka kusafisha na kulinda uke.....
Wasiliana nasi kupitia simu no 0765343998 pia namba hii ipo whatsup


Habari! Suruhisho la changamoto ya uzazi kwa Wanawake na wanaume  sasa limefika mwisho.wasiliana nasi ili kutatua changa...
17/01/2026

Habari! Suruhisho la changamoto ya uzazi kwa Wanawake na wanaume sasa limefika mwisho.wasiliana nasi ili kutatua changamoto yako ;
🩸Je unasumbuliwa na kutokushika mimba?
🩸Je mbegu zako za kiume haziwezi kukupatia matunda /kurutubiasha yai la mwanamke na kutungisha mimba?
🩸 Huna hisia na mwenzi wako tena?

Wasiliana nasi kupitia 0765343998



Address

Kimara Stop Over
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AFYA Care posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram