27/04/2022
UGONJWA WA HOMA YA INI
Dalili za ugonjwa wa Homa ya INI na jinsi unavyoambukizwa (ugonjwa huu ni hatari kuliko UKIMWI)
Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambavyo vikishaingia mwilini hushambulia ini kabla ya kugeuka maradhi sugu.
Virusi hivyo vinaitwa HEPATITIS VIRUS (vipo vya aina nne yaani Hepatitis A, B, C na D). Utafiti unaonesha kuwa hepatitis B na C ndio hatari sana.
Virusi hivyo husambazwa kwa njia ya damu au majimaji mengine ya mwilini, mfano mate au jasho. Watu takribani 1000000 wanapoteza maisha duniani kote kutokana na ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis).
Ugonjwa huu k**a haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye kifo.
JINSI UNAVYOAMBUKIZWA
Katika maeneo hatari zaidi duiani, virusi vya Hepatitis B (HBV) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hususan nyakati za utotoni.
K**a ilivyo kwa UKIMWI virusi vya homa ya ini pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate,jasho na mwingiliano ule wa damu.
Zifuatazo ni njia kuu za maambukizi;
- Kujamiiana bila kinga
- Kunyonyana ndimi (denda)
- Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua
- Kuchangia damu isiyo salama
- Kuchangia vitu vyenye ncha kali k**a sindano, wembe nk
- Kuchangia mswaki
- Kuchangia taulo na mwenye ugonjwa Huu
- Kubadilishana nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho.
Tafiti za kitalamu zinaonesha kwa kuwa virusi hivyo ni hatari sana kuliko UKIMWI kwa sababu vinaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu (yaani nje ya mfumo wa damu) kwa siku saba.
Virusi vya ukimwi havina uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.
Kutokana na usugu wa HBV, maana yake ni kwamba k**a kirusi kipo kwenye ngozi, kitaendelea kuwa hai kwa siku saba na katika kipindi hicho mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya damu au jasho.
Kwa wastani kirusi cha HBV kikishaingia mwilini, hupevuka ndani ya siku 75, hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya siku 30-180.
Ndani ya siku 60, mtu mwenye HBV anaweza kugundulika ikiwa atapimwa.
Mtu mwenye HOMA YA INI ana wastani mdogo wa kuishi kuliko HIV.
Kwa maana hiyo, mwenye maambukizi ya virusi vya Homa ya Ini hufariki dunia haraka kuliko VVU.
DALILI ZA UGONJWA HUU
Watu wengi hawaoneshi dalili yoyote. Kwa maana hiyo mtu anaweza kuishi na HBV na kusababisha maambukizi kwa wengine bila kugundulika.
Hata hivyo, watu wengine hushambuliwa na homa kali na dalili ambazo hudumu kwa wiki kadhaa.
Dalili hizo ni;
√ Uchovu
√ Kichefuchefu
√ Kupungua uzito
√ Maumivu makali ya tumbo
√ Homa Kali
√ Kupoteza hamu ya kula
√ Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
√ Macho na ngozi kuwa vya njano
√ Mkojo mweusi
Kwa wagonjwa wengine, virusi vya Hepatitis husababisha ini kuharibika kabisa (cirrhosis of the liver) au saratani ya ini (liver Cancer).
KINGA
√ Chanjo
√ Kutumia kinga wakati wa kijamiiana
√ Kuacha kuchangia vitu vyenye ncha Kali k**a sindano,wembe,nk
√ Kutochangia miswaki
√ Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
√ Kutochangia damu isiyo salama
Jali afya yako usizarai changamoto ulonayo kwani mpk sasa hujui ulivyo mwilini mwako wala desturi ya kwenda hospital huna na unashauriwa kila siku tumia virutubisho kuimarisha afya yako umekuwa mtu wa kusahau ✍️