Afya Solutions

Afya Solutions Tunatoa ushauri bure wa changamoto zote za Afya

  therapy   Saratani
06/06/2025

therapy
Saratani

*Tafiti*: Mazoezi kwa wanaume huongeza nguvu za kufanya tendo la ndoa na husaidia kuboresha mbegu za kiume.-🏋️Mazoezi hu...
10/02/2025

*Tafiti*: Mazoezi kwa wanaume huongeza nguvu za kufanya tendo la ndoa na husaidia kuboresha mbegu za kiume.

-🏋️Mazoezi husaidia mzunguko wa damu kuwa vizuri mwilini na hivo hupelekea uume kusimama kwa muda mrefu wakati wa tendo la ndoa.

-🏋️Pia Mazoezi huongeza stamina wakati wa tendo na kuondoa uchovu baada ya tendo la ndoa.

-Faida Kubwa za Kufanya Mazoezi Asubuhi husaidia kuweka sawa kiwango cha cholesterol au mafuta yaliyopo mwilini. hupunguza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa kisukari, hushusha kupanda kwa shinikizo la damu. hupunguza uwezekano wa mtu kupata baadhi ya maradhi ya saratani.

Wasiliana nasi kwa number 0694 435 649
22/11/2024

Wasiliana nasi kwa number

0694 435 649

Haya ni matunda yanayozuia kusambaa kwa seli za kansa ,pia kuzia kupata kansaJitahidi kila ulionapo tunda mojawapo kati ...
24/09/2024

Haya ni matunda yanayozuia kusambaa kwa seli za kansa ,pia kuzia kupata kansa

Jitahidi kila ulionapo tunda mojawapo kati ya haya,usiache kulipata na kulitumia

Solutions

06/09/2024

DOKEZO LA KUJALI AFYA YAKO MWEZI HUU.

🧠. Angalia/Jali afya yako ya akili (Looking after your Mental Health)

Moja ya njia za kujijali Ili kupata Afya njema ni pamoja na kuchunga/kutunza Afya yako ya akili. Afya ya mwili si kitu bila afya njema ya akili.

Fanya mambo yafuatayo Ili kujenga Afya yako njema ya akili.

▪️Fanya mazoezi ya mwili. Angalau kutembea kwa dakika 30 kwa siku Ili kuchochea Hali nzuri ya mwili (mood activation).

▪️Pata muda wa kutosha kupumzika. Hakikisha unapata muda wa kutosha kulala Ili kupata nguvu mpya ya mwili na akili.

▪️Kula mlo wenye Afya. Jitahidi Kula mlo kamili Ili kuupatia mwili nguvu na kuupatia ubongo wako afya njema katika kuimarisha afya ya akili.

▪️Epuka kukaa kimya na Tatizo. Unapokuwa na tatizo Epuka kujifungia na kubaki na tatizo lako wewe mwenyewe Bali jenga tabia ya kuwashirikisha watu wako wa karibu. Tabia ya kushirikisha hukupatia nafasi ya kupata ushauri na njia Bora ya kuondokana na tatizo kuliko kukaa kimya mwenyewe.

▪️Fanya jambo unalolipenda zaidi wakati umechoka. Jenga tabia ya kufanya jambo unalipenda zaidi hasa pale unapokuwa umechoka k**a vile kucheza mchezo unaopenda, kutazama vichekesho, kutembelea maeneo unayopenda n.k.

▪️Weka mipango na vipaumbele (Set goals and Priorities). Ili kuepuka mlundikano wa mambo yenye kuchosha akili yako wakati wa kuyafanya, kuwa na tabia ya kuandika/kuweka mipango pamoja na vipaumbele vya kuanza navyo. Hii itakusaidia kuzingatia Kila jambo Kwa wakati wake na kuipa akili uwezo wa kufikiri katika eneo husika kwa wakati.

▪️Jenga tabia ya kujipongeza kwa Kila jambo ulilokamilisha hata k**a ni dogo. Kila jambo utakalofanya, Jenga tabia ya kulifurahia na kujipongeza hata k**a ni dogo. Hali hii itakujengea uwezo wa akili na kukupa ujasiri wa kufanya mambo makubwa zaidi ukiwa na afya njema ya akili.

▪️Jiunganishe kijamii (Stay socially connected). Kuwa na tabia ya kuzungumza, kujamiiana, kuwa na marafiki wengi na kujiunganisha kadiri uwezavyo. Tabia hii itakuwezesha kuwa na jamii kubwa ya kubadilishana mawazo na kuepukana na tatizo la msongo wa mawazo.

Wakati ni Sasa kwani Afya sio Afya bila afya ya akili.

*Afya Solutions*

"We care about you"

*TEZI DUME* Tezi dume ni tezi inayopatikana kwa jinsia ya kiume. Tezi hii ina kazi ya kutengezeza  majimaji meupe mepesi...
28/08/2024

*TEZI DUME*

Tezi dume ni tezi inayopatikana kwa jinsia ya kiume. Tezi hii ina kazi ya kutengezeza majimaji meupe mepesi yenye unato kidogo. Majimaji haya husaidia mbegu za kiume kutembea kwa urahisi.

🧑🏻‍⚕️Tezi dume iko mwishoni mwa kibofu cha mkojo. Pia inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na mrija wa mkojo wa uume (urethra) na iko mbele kidogo ya utumbo mpana ndani ya mfupa wa nyonga.

🚨Saratani ya tezi dume maana yake ni tezi dume imepata ugonjwa wa saratani..Na hii hutokea pale ambapo chembechembe hai za tezi huasi na kuanza kujigawanya bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili, chembechembe asi hizi mwishowe hutengeneza vivimbe hatari ndani ya tezi dume na hatimaye husambaa mwilini

*VISABABISHI HATARISHI KWA SARATANI YA TEZI DUME*

➡️Umri Mkubwa kuanzia miaka 50

➡️Vinasaba (ukoo wenye historia a saratani hii

➡️Lishe hatarishi-nyama nyekundu kwa wingi, mafuta/samli,maziwa ya krimu

➡️Unene uliokithiri

➡️Ukosefu wa mazoezi

➡️Upungufu wa virutubisho,mfano vit D.

➡️Maambukizi ya mara kwa mara kwenye tezi dume

*Dalili zake ni zipi?*

Udhaifu katika utoaji wa mkojo, mkojo hauishi.
Kwenda kukojoa mara kwa mara.
Damu ndani ya mkojo.
Kushindwa kukojoa.
Maumivu ya kiuno na mifupa ya nyonga.
Wagonjwa wengi huanza maumivu ya nyonga k**a ni dalili za awali.
Udhaifu katika utoaji wa mkojo pia kunaweza kutokea kwa kuvimba kwa tezi dume bila ya saratani.
Damu kwenye mkojo nakushindwa kumaliza mkojo ni ishara tosha ya kuwa tezi dume imeathirika.

*UCHUNGUZI*

Wanaume wote wanpaswa kufanya uchunguzi wa saratani ya tezi dume kuanzia miaka 50. Kwa wale wenye historia katika familia wanapaswa kuanza wakiwa na umri wa miaka 45.

Uchunguzi unafanyika kwa njia zifuatazo

👉Uchunguzi kwa cancer marker kwa kuchunguza damu (PSA).
👉Uchunguzi kwa njia ya kipimo cha njia ya haja kubwa (DRE)
Biopsy.
👉Ultrasound.
👉X-ray.
👉Bone scan.
Jinsi ya kutibu saratani ya tezi dume

🧑🏻‍⚕️Upasuaji.
🧑🏻‍⚕️Mionzi
🧑🏻‍⚕️Dawa ya saratani
🧑🏻‍⚕️Homoni.
🧑🏻‍⚕️Matibabu hutegemea

Ngazi na ukali wa ugonjwa.
Je, ugonjwa upo ndani ya tezi dume tu au umesambaa.
Umri na afya ya mgonjwa.
Magonjwa ambatanishi na saratani hiyo, shinikizo la damu, matatizo ya moyo na kisukari.

*TIBA*

*UPASUAJI*

Kuondoa tezi dume yote peke yake inaweza ikatosha.
Kuondoa tezi dume na tezi jirani.
Kuondoa tezi dume na kuhasi
Kuondoa tezi dume kidogo kupitia njia ya mkojo na kumpa mgonjwa tiba shufa.

*MIONZI* .

Sawa na upasuaji inaweza kuondoa ugonjwa iwapo haujasambaa.
Mionzi pia hutolewa k**a tiba shufaa.

*DAWA YA SARATANI*

Baadhi ya wagonjwa hufaidika na tiba hii, dawa hutolewa kwa muda mfupi na kufuatilia maendeleo ya mgomjwa kwa kufanya PSA,dawa inaweza kuwa moja au mchanganyiko.

*HOMONI*

Hutolewa mfullulizo kwa njia ya vidonge au sindano.

*Ufuatiliaji wa karibu*

Ni muhimu kufuatilia hali ya tezi isirejee baada ya ugonjwa kutibiwa kwa kufanya kipimo cha PSA mara kwa mara angalau miezi mitatu mara moja.

Athari zitokanazo na matibabu mbalimbali yaliyotajwa.

*Upasuaji*

Unaweza kusababisha kutoweza:

👉Kuzuia mkojo
👉Kupoteza nguvu za kiume.

*Homoni*

👉Homoni huongeza joto mwilini
👉Kupungukiwa na nguvu za kiume

*Afya Solutions*

💊💊💉Dawa zipo za kutibu na Kumaliza kabisa Tatizo la KUTANUKA KWA TEZI DUME Pamoja na SARATANI YA TEZI DUME Bila upasuaji

Karibuni sana

Epuka Saratani ya UTUMBO MPANA kwa kufanya haya👇👇K**a tayari una changamoto ya Kansa ya utumbo,wasiliana nasi0694 435 64...
25/06/2024

Epuka Saratani ya UTUMBO MPANA kwa kufanya haya👇👇

K**a tayari una changamoto ya Kansa ya utumbo,wasiliana nasi

0694 435 649

🧑‍💻🌍💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦👍🏼Muda mzuri sana wa kunywa maji ni asubuhi... kabla ya kula kitu chochote...☺️Ingawa k**a ni mara...
04/06/2024

🧑‍💻🌍

💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦💦

👍🏼Muda mzuri sana wa kunywa maji ni asubuhi... kabla ya kula kitu chochote...

☺️Ingawa k**a ni mara yako ya kwanza Kunywa Maji Asubuhi sana hii utahisi Vibaya sana _mfano_ Kichefuchefu Nusu kutapika ( lakini hautotapika kabisa) au hali fulani Tofauti kidogo
Ikitokea hivyo Sio uache, Wala Haina Madhara yoyote isipokuwa hapo ndipo utajifahamu mwili wako unasumu Nyingi mwilini jitahidi kuendelea Kunywa Maji Kila Siku huku pia ukitenga Muda wa Mazoezi ya mwili angalau Dkk 30

Hapa Wapendwa zipo Faida NYINGI SANA tukiweka Desturi ya Kunywa Maji asubuhi.
Pia Kunywa Maji safi na salama ya Kutosha Kwa Siku Nzima

*Mfano*
🚚 Usalama wa Gari Katika safari ya Siku nzima huwa linachunguzwa Asubuhi maona kuwekewa maji asubuhi mapema kabla ya Safari zake..
Ikiwemo na *kujaza Maji* 🚰,

💁🏻‍♂️..Kwa mtu Mzima Kunywa lita moja:
K**a una asali waweza kuchanganya vijiko viwili vikubwa ..

Na maji yawe vugu vugu yasiwe baridi sana.....

Maji usiku ukienda kulala haipendezi kunywa maji isipokuwa kidogo tu: kwasababu mwili waenda kupumzika na kibofu cha mkojo haitakiwi kiwe na mkojo na huku umelala ni hatari kwa Afya yako .

Na pia ukimaliza kula chakula usinywe maji hapo hapo mpaka ipite k**a nusu saa hivi ndio unywe maji mengi...

*Kumbuka:*

Kiwango Sahihi Cha Kunywa Maji Kwa Siku hutegemea sana Umri wako na Kilo zako Mwenyewe
*_Lakini_*
usiache kabisa Kunywa Maji mengi na ya kutosha

*SARATANI YA KOO* 👨🏽‍⚕️Saratani ya koo ni miongoni mwa magonjwa ya kutisha. Ingawa baadhi ya wagonjwa wa saratani ya koo...
21/05/2024

*SARATANI YA KOO*

👨🏽‍⚕️Saratani ya koo ni miongoni mwa magonjwa ya kutisha. Ingawa baadhi ya wagonjwa wa saratani ya koo wanaweza kutibiwa na kupona kabisa, kuna mjadala miongoni mwa matabibu juu ya tiba sahihi ya ugonjwa huu. Bila kujali ni aina gani itakayotumika, karibu aina zote za tiba za saratani hii huwa na madhara kwa mgonjwa na wakati mwingine kusababisha kifo badala ya kuponya.

✍️Muundo wa Koo
Ili tuweze kujadili vizuri ugonjwa huu, ni vema kwanza tuangalie muundo wa koo. Koo ni sehemu mojawapo ya mfumo wa chakula likiwa na urefu wa takribani sentimita 25 kuanzia mdomoni mpaka kwenye mfuko wa tumbo yaani stomach.

Ukuta wa koo unajengwa na tando (layers). Tando hizi zimetengenezwa kwa aina tofauti ya chembe hai au seli ambazo kila moja ina kazi zake maalum. Sehemu ya ndani kabisa ya ukuta wa koo huitwa mucosa ambayo hufanya kazi ya kulowanisha chakula ili kiweze kupita vizuri kuelekea kwenye mfuko wa chakula.

Chini ya utando huu, kuna utando mwingine unaoitwa submucosa ambao umejaa tezi zenye kuzalisha ute unaoitwa mucus ulio na kazi ya kulainisha koo na kulifanya liwe na hali ya umajimaji muda wote. Utando wa tatu unajulikana k**a muscle layer. Utando huu umejaa misuli inayosaidia koo kusukuma chakula kuelekea tumboni. Utando wa juu kabisa unaolizunguka koo huitwa outer layer ambao una kazi ya kulinda koo kwa ujumla.

Aina za saratani ya koo
Kuna aina kuu mbili za kansa ya koo, nazo ni:-
1) *Adenocarcinoma* na
2) *squamous cell carcinoma* .
Aina hizi hutofautiana kulingana na jinsi seli zake zinavyoonekana kwenye darubini. Hata hivyo, pamoja na tofauti hizi za kimuonekano, utambuzi na matibabu ya aina hizi za saratani ya koo hufanana.

Aina zote hizi mbili huanza kwanza kuathiri seli zilizo katika utando wa ndani wa ukuta wa koo yaani mucosa kabla ya kusambaa maeneo mengine.

Vihatarishi vya kansa ya koo
Ingawa chanzo halisi cha kansa ya koo hakijulikani, mambo yafuatayo yanaweza kusababisha mtu kupata saratani ya koo. Hata hivyo, pamoja na kuwepo vihatarishi hivi, ni vigumu kueleza kwa ufasaha kwa nini mtu au watu fulani wanaweza kupatwa na kansa ya koo na mtu mwingine asipate. Vihatarishi hivi ni

*Umri:* Hatari ya kupata saratani ya koo huongezeka zaidi kwa watu walio na umri wa miaka 65 na kuendelea. Hata hivyo saratani ya koo aina ya adenocarcinoma inaweza kutokea hata kwa wanawake walio na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea.
*Jinsia:* Tafiti nyingi zimeonesha kuwa wanaume wana uwezekano wa kupata saratani ya koo mara tatu zaidi ya wanawake.
*Uvutaji sigara:* Wavutaji sigara wapo katika hatari ya kupata saratani ya koo ukilinganisha na wasio wavutaji.
*Unywaji pombe wa kupindukia:* Unywaji wa pombe kwa kiasi cha chupa tatu na zaidi kwa siku unamuweka mnywaji katika hatari ya kupata saratani ya koo ikilinganishwa na mtu asiyekunywa kabisa pombe. Aidha wanywaji wa kupindukia ambao pia ni wavutaji sigara wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya koo ikilinganishwa na wanywaji wa pombe wasio wavutaji sigara. Kwa maneno mengine, unywaji pombe pamoja na uvutaji sigara hufanya kazi kwa pamoja kuongeza uwezekano wa mtu kupata saratani ya koo.
*Lishe* : Kuna mjadala kuhusu mchango wa aina fulani za vyakula katika kusababisha saratani ya koo. Wakati watafiti wengine wanasema ulaji wa matunda na mboga mboga husaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya koo, watafiti wengine wanapinga kuhusu suala hilo.
*Unene kupindukia* : Unene wa kupitiliza huongeza uwezekano wa kupata saratani ya koo aina ya adenocarcinoma.
*Matatizo ya tumbo:* Matatizo sugu katika tumbo yanayosababisha tindikali kurudi kwenye koo (acid reflux) kutoka tumboni husababisha madhara katika seli za koo na hatimaye kupelekea saratani ya koo kwa baadhi ya watu.
*Tatizo sugu la kucheua kwa tindikali:* Iwapo tatizo la tindikali kucheuliwa kwenye koo litaendelea kwa muda mrefu mpaka kuwa sugu, sehemu ya chini ya koo yaweza kuathiriwa na kusababisha hali ijulikanayo kitaalamu k**a Barrett esophagus. Hali hii huongeza uwezekano wa kutokea kwa saratani ya koo.

*Dalili za saratani ya koo*

Mgonjwa mwenye saratani ya koo katika hatua za awali anaweza asioneshe dalili zozote zile. Hata hivyo, kadiri saratani inavyozidi kukua na kuenea, mgonjwa anaweza kuwa na dalili zifuatazo:

👉🏻Chakula kukwama kwenye koo
Siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate
👉🏻Maumivu wakati wa kumeza chakula hasa chakula kigumu
👉🏻Maumivu kwenye kifua au mgongoni
👉🏻Kupungua uzito
👉🏻Kiungulia
👉🏻Sauti ya mkwaruzo au kikohozi kikavu cha zaidi ya wiki mbili
👉🏻kupaliwa mara kwa mara

🧏🏻‍♂️Hata hivyo ifahamike kuwa dalili hizi zinaweza kutokea pia kwa baadhi ya magonjwa mengine tofauti na saratani ya koo. Hivyo ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

Uchunguzi na vipimo
Ili kujiridhisha kuwa mgonjwa ana saratani ya koo, daktari atasikiliza historia ya mgonjwa kisha atamfanyia uchunguzi wa mwili wake kabla ya kuagiza kufanyika kwa vipimo kuthibitisha zaidi.

Vipimo kwa ajili ya utambuzi wa saratani ya koo ni pamoja na

👨🏻‍💻Aina ya X ray iitwayo Barium swallow ambayo huonesha muundo wa koo pamoja na tumbo (stomach).
Kipimo cha Endoscopy ambacho husaidia kuchunguza ndani ya koo, tumbo pamoja na eneo lote la utumbo
Kuchunguza sehemu ya koo kwenye darubini (biopsy). Kwa sasa, njia hii ndiyo ya uhakika zaidi ya kutambua uwepo wa seli za saratani katika koo.

✍️Iwapo itathibitika kuwepo kwa saratani katika koo, madaktari hupendelea kufahamu hatua ya ugonjwa ilipofikia. Kitendo hiki huitwa staging. Faida ya kufanya staging ni kuwa husaidia kufahamu ukubwa wa tatizo yaani ni kwa kiasi gani seli za koo zimeathiriwa, iwapo saratani imesambaa na kuathiri maeneo ya jirani na k**a imesambaa ni viungo gani vilivyo athirika.

Aidha staging husaidia pia kufanya maamuzi ya njia gani ya tiba itumike katika kumtibu mgonjwa. Saratani ya koo huweza kusambaa na kuathiri sehemu k**a mifupa, ini na mapafu.

Ili kufahamu k**a saratani imesambaa kwenye viungo hivi, vipimo vifuatavyo vyaweza kufanyika:

👨🏽‍⚕️Kipimo kiitwacho endoscopic ultrasound ambacho husaidia kutambua iwapo viungo vilivyo jirani na koo vimeathirika ama la. Pia husaidia kufahamu hali ya tezi (lymph nodes) zilizo karibu na koo. Daktari pia anaweza kuchukua sehemu ya tezi hizo (lymph node biopsy) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
👨🏽‍⚕️CT Scan husaidia kutambua jinsi koo na sehemu nyingi za mwili zilivyoathirika.
👨🏽‍⚕️MRI ni kipimo kingine kinachosaidia kuonesha iwapo saratani ya koo imesambaa na kuathiri tezi na sehemu nyingine za mwili.
👨🏽‍⚕️PET scan: Nia aina ya kipimo ambacho huonesha kwa uhakika na ubora zaidi ukilinganisha na vipimo vingine uwepo wa saratani ya koo na k**a imesambaa sehemu nyingine za mwili. Hata hivyo, kipimo hiki kwa sasa hakipatikani nchini kwetu.
👨🏽‍⚕️Bone scan ni kipimo ambacho huwezesha kutambua iwapo saratani imesambaa mpka kwenye mifupa.
Wakati mwingine madaktari hulazimika kufanya upasuaji ili kuweza kufanya staging kwa uhakika zaidi.

Kwa mujibu wa staging, kuna hatua tano za saratani ya koo:

*Hatua ya 0:* Hatua hii huitwa carcinoma in situ ambapo seli za saratani hupatikana tu kwenye utando wa juu wa koo.

*Hatua ya I:* Saratani husambaa kutoka utando wa juu mpaka kwenye tando nyingine za koo.

*Hatua ya II* : ina tabia mojawapo kati ya hizi zifuatazo:
✍️Saratani husambaa kutoka kwenye utando wa juu wa ukuta wa koo mpaka kwenye utando wa chini yake yaani submucosa na kisha kuenea kwenye tezi za karibu, AU
Saratani husambaa na kushambulia utando wa misuli wa koo (muscle layer) na baadhi ya seli nyingine za saratani hufika kwenye tezi za jirani, AU
Saratani husambaa kutoka katika utando wa ndani mpaka kufikia utando wa nje kabisa (outer layer) wa koo.

*Hatua ya III* : ina tabia mojawapo kati ya hizi:
Saratani husambaa kufikia kwenye utando wa nje kabisa wa koo na kisha kusambaa hadi kwenye tezi za jirani, AU
Saratani husambaa na kushambulia viungo vya karibu na koo k**a vile njia ya hewa. Aidha seli za saratani huwa zimesambaa mpaka kwenye tezi za jirani.

*Hatua ya IV* : Seli za saratani husambaa na kuathiri viungo vingine vilivyo mbali na koo k**a vile mapafu, ini na mifupa.
Matibabu ya Saratani ya Koo
Uchaguzi wa aina gani ya tiba itumike hutegemea sana eneo lililoathiriwa na saratani, iwapo saratani imeshambulia viungo vilivyo karibu na koo, iwapo saratani imesambaa mpaka kufikia kwenye tezi au viungo vingine vya mwili, na hali ya mgonjwa kwa ujumla.

Kutokana na hayo, saratani ya koo yaweza kutibiwa kwa kufanya upasuaji, kutumia mionzi, kutumia kemikali maalum, au mchanganyiko wa yote matatu.

Hivi ni vyakula muhimu vya kusaidia kupambana na ugonjwa wa cancer
15/05/2024

Hivi ni vyakula muhimu vya kusaidia kupambana na ugonjwa wa cancer

Saratani inazuilika na inatibika pia,wahi mapema matibabu
26/04/2024

Saratani inazuilika na inatibika pia,wahi mapema matibabu

25/04/2024

Tunazidi kuwasaidia wagonjwa wenye cancer za Aina mbalimbali k**a na wewe unasumbuliwa na changamoto hii,tafadhari wasiliana nasi

0694 435 649

Address

Dar Es Salaam
SURVEY

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Solutions posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afya Solutions:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram