27/09/2025
Kisukari ni moja ya sababu kuu za magonjwa ya figo.
Sukari ikiwa nyingi mwilini huathiri mishipa midogo ya damu kwenye figo, jambo linalopunguza uwezo wa mishipa hii kuchuja uchafu na maji ya ziada mwilini.
Kadiri uharibifu unavyoongezeka, figo hushindwa kufanya kazi ipasavyo kwa sababu hazipati damu ya kutosha hali inayopelekea matatizo mengine makubwa k**a shinikizo la damu, kuvimba kwa mwili, magonjwa au shida za figo na hatimaye figo kushindwa kabisa kufanya kazi (kidney failure).
Jinsi ya kulinda figo zako:
β
Dhibiti kiwango cha sukari mwilini, k**a unatumia dawa za sukari zingatia utaratibu wa dawa na usiache kutumia dawa na usibadili dawa bila maelekezo ya daktari.
β
Kunywa maji ya kutosha
β
Punguza chumvi kupita kiasi
β
Epuka matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari
β
Fanya uchunguzi wa figo
0767 536 986 MTAfrica Wellness