05/01/2025
NJIA 5 MUHIMU ZA KISAYANSI ZINAZOWEZA KUKUSAIDIA KUISHI MAISHA MAREFU YENYE FURAHA
Watu wengi wanataka kuishi maisha maisha marefu na ya furaha, au walau kuepuka maisha mafupi na mabaya. Iwapo unajipata miongoni mwa watu hao walio wengi, una bahati.
Changamoto ni kugeuza uelewa huu kuwa ushauri na tiba ambavyo tunaweza kunufaika nayo. Hapa tunaelezea mambo ambayo yanarefusha maisha ya kiafya kulingana na inavyofikiriwa kisayansi na kuonyesha jinsi mambo haya ni ukweli wa kisayansi.
1. Virutubisho na mtindo wa maishaUtafiti wa makundi makubwa ya watu unaonyesha kwamba kuwa kutoongeza uzito wa mwili, kutovuta sigara, kunywa vilevi kwa kiasi, na kula walau milo mitano ya matunda na mboga kwa siku inaweza kuongeza umri wako wa kuishi kwa miaka 14 ikilinganishwa na mtu anayevuta sigara au tumbaku, kunywa vilevi kupita kiasi, na kuwa na uzito wa mwili wa kupita kiasi.
Punguza wanga hata zaidi, kwa karibu theluthi tatu, kile kinachoitwa sheria ya udhibiti wa chakula, kuliboresha afya na kuongeza muda wa maisha katika panya na nyani, ilimradi wanakula vyakula sahihi, ingawa hicho ni kitu kigumu kumtaka binadamu afanye hivyo, ambaye ana majaribu ya chakula.
Kula chakula kidogo kwa saa chache za siku au kufunga na kula katika masaa manane kwa siku au kufunga kula chakula siku mbili kwa wiki ni mambo yanayoaminiwa kupunguza hatari za watu wenye umri wa kati wa maisha za kupata magonjwa yenye uhusiano na umri.
2. Mazoezi ya mwili Kwa ujumla duniani, maisha ya kutofanya mazoezi ya mwili husababisha moja kwa moja 10% ya vifo vya mapema kutokana na magonjwa ya kudumu, k**a vile ugonjwa wa moyo, kisukari aina ya mbili, na aina mbali mbali za saratani. K**a kila mtu duniani atafanya mazoezi ya kutosha, athari yake inaweza kuwa ni ongezeko la kuishi umri mrefu wa maisha ya afya kwa karibu mwaka mmoja. Lakini ni kiasi gani cha mazoezi kilicho bora? Mazoezi ya viwango vya juu zaidi kwa ukweli ni mabaya kwako, sio tu katika kuimarisha misuli au kukunja mifupa laini inayounganisha viungo.
Mazoezi ya viwango vya juu yanaweza kuzuia utendaji kinga ya mwili na kuongeza hatari ya mtu kupata ugonjwa wa mfumo wa upumuaji. Mazoezi ya zaidi ya dakika 30 kidogo, rahisi na ya haraka yanatosha kwa watu wengi. Sio tu kwamba yanakufanya uwe mwenye nguvu na imara tu , pia imeonesha kuwa husaidia kupunguza majeraha yenye madhara mwilini na hata kuboresha hali yako.
3. Inua kiwango cha mfumo wa kinga ya mwili
Haijalishi una ukak**avu wa kiwango gani na haijalishi unakula vyema kiasi gani, mfumo wako wa kinga ya mwili, kwa bahati mbaya huwa na kiwango cha chini cha ufanisi kadri unavyoendelea kukua kiumri. Uwezo duni wa ufanishi wa chanjo na kushindwa kupambana na maambukizi kwa mwili wako ni matokeo ya udhaifu wa mfumo wa kinga ya mwili.
Huanza kupungua katika miaka ya kuelekea utu uzima wakati kiungo cha Imo kilichopo kooni kinapoanza kufungika.
Hilo ni jambo baya kulisikia, lakini pia linatisha zaidi pale unapogundua kwamba kiungo cha koo (au thymus) ndio mahali ambapo seli zinazopambana na maradhi zinazoitwa -T cells zinaishi.Kufungwa kwa kituo cha elimu cha T cells-zinazotambua maambukizi na kupambana nayo ina maanisha kuwa haziwezi kutambua maambukizi mapya au kupambana na saratani kwa ufanisi miongoni mwa watu wenye umri mkubwa. Njia nyingine ni kutumia virutubishi mbadala ili kuamsha seli za kinga ili kuondoa uchafu ndani ya mwili, k**a vile protini zilizoharibika. Hii kwa pamoja huboresha mfumo wa kinga mwilini wa wazee na kwa sasa mbinu hii inafanyiwa majaribio k**a njia bora ya kuwasaidia wazee waliopata chanjo ya Covid-19 kuwa na hali bora kiafya. 4. Uzalishwaji upya wa seli Senescencia ni hali ya kuwa na sumu ambayo huzipata seli zetu tunapokuwa wazee, zinasambaa mwili mzima na kusababisha majeraha ya kiwango cha chini na ugonjwa wa udumu, na hivyo kusababisha kuzeeka kibaiolojia. Mwaka 2009, wanasayansi walionyesha panya wenye umri wa kati walioishi kwa muda mrefu na walikuwa wenye afya zaidi walipopewa dawa inayoitwa rapamycin, ambayo hutunza protini inayoitwa mTOR . Inasaidia kudhibiti seli zinavyopokea na kufanyia kazi virutubisho, msongo wa mawazo, homoni, na uharibifu.