16/09/2022
Bawasiri (Piles au hemorrhoids) ni mkusanyiko wa tishu zilizovimba/kuumuka ndani ya njia ya mkundu. Zina mishipa ya damu, tishu zinazosapoti, misuli, na nyuzinyuzi zenye kuvutika.
Watu wengi wana bawasiri, lakini dalili haziwezi kufanana mara zote. Bawasiri huonesha dalili walau kuanzia asilimia 50 ya watu wa Marekani kabla ya umri wa miaka 50.
Makala hii itaielezea bawasiri, sababu zinazopelekea kupata ugonjwa huu, namna ya kuufahamu, ngazi zake, na namna ya kutibu, na athari gani gani zinaweza kuleta kwenye mwili.
Ukweli wa Haraka Kuhusu Bawasiri:
Bawasiri ni mkusanyiko wa tishu na mishipa ya damu ambayo huumuka na kuvimba.
Ukubwa wa bawasiri unatofautiana, na hupatikana ndani na nje ya mkundu.
Bawasiri hutokea kutokana na tatizo la kuvimbiwa lililo komaa, tatizo la kuharisha lililo komaa, mazoezi ya kunyanyua vitu vizito, ujauzito, au kujikamua wakati kinyesi kinapotoka.
Daktari mara nyingi hutambua bawasiri kwa vipimo.
Bawasiri hupewa ngazi kwenye vipimo kuanzia I hadi IV. Kwenye ngazi ya III au IV, upasuaji unaweza kuhitajika.
Bawasiri ni Nini?
Fahamu kila kitu kuhusu bawasiri
Bawasiri ni mkusanyiko wa tishu zilizoumuka na kuvimba kwenye eneo la haja kubwa (mkundu).
Zinaweza kuwa na ukubwa tofauti tofauti, na zinaweza kuwa ndani au nje.
Bawasiri za ndani hupatikana kati ya sentimita(cm) 2 na 4 juu ya uwazi wa mkundu, na huwa ni za aina moja. Bawasiri ya nje ya ncha ya mkundu.
Dalili
Kwenye kesi nyingi, dalili za bawasiri hazina ugumu kuzitambua. Mara nyingi hujionesha baada ya siku chache.
Mtu mwenye bawasiri huweza kuwa na dalili zifuatazo:
Kuhisi uvimbe mgumu unaouma kuzunguka mkundu (njia ya haja kubwa). Uvimbe huo unaweza kuambata na damu. Bawasiri zinazoambatana na damu zinaitwa thrombosed external hemorrhoids.
Baada ya kinyesi kutoka, mtu mwenye bawasiri anaweza kuhisi bado kinyesi hakijaisha kwenye utumbo mkubwa.
Damu nyekundu hasa huonekana baada kinyesi kutoka.
Eneo kuzunguka mkundu huwasa, nyekundu, na kuuma.
Maumivu hutokea kipindi kinyesi kinapotoka.
Bawasiri inaweza kwenda na kuwa mbaya zaidi. Ikiwemo:
kutokwa na damu nyingi mkunduni, pia hupelekea kutokea kwa anemia.
maambukizi
Kutokuwa na uwezo wa kudhibiti mwendo wa njia ya chakula (bowel movements)
Fistula ya njia ya haja kubwa, ambapo mfereji hutengenezwa kati ya ngozi karibu na mkundu na ndani ya mkundu.
Bawasiri aina ya strangulated hemorrhoid, ambapo hukatisha usambaaji wa damu kwenye bawasiri, kusababisha matatizo yakiwemo maambukizi au damu kuganda.
Bawasiri imegawanyika kwenye ngazi nne:
Ngazi ya I: Kuna vivimbe vidogo, mara nyingi ndani ya kuta za mkundu. havionekani.
Ngazi ya II: Bawasiri ngazi ya II ni kubwa kuliko ngazi ya I, lakini pia ubakia ndani ya mkundu. Vinaweza kusukumwa nje kipindi kinyesi kinapopita, lakini hurudi bila kusaidiwa.
Ngazi ya III: Bawasiri hii pia hufahamika k**a pr*****ed hemorrhoids, na huonekana nje ya mkundu. Mtu huhisi vivimbe hivi kuning’inia kutoka kwenye puru, lakini vinaweza kurudishwa ndani.
Ngazi ya IV: Vivimbe hivi haviwezi kurudishwa ndani na huitaji matibabu. Ni vikubwa na hubakia nje ya mkundu.
Bawasiri ya nje hutengeneza vivimbe vidogo nje tu ya mkundu. Vinawasha sana na vinaweza kuuma sana k**a kukitokea kuganda kwa damu, kwani kuganda kwa damu kunaziba mzunguko wa damu. Bawasiri za nje (Thrombosed external piles), ambazo zimegandisha damu, zinahitaji matibabu.
Sababu
Bawasiri husababishwa na ongezeko la shinikizo kwenye puru.
Mishipa ya damu kuzunguka mkundu na ndani ya puru itajivuta kwa shinikizo na inaweza kututumka au kuumuka, kutengeneza bawasiri. Hali hii inaweza kutokana na:
Tatizo sugu la kuziba choo (chronic constipation)
Tatizo sugu la kuharisha (chronic diarrhea)
Kunyanyua vitu vizito
Ujauzito
Kujikamua kipindi unajisaidia haja kubwa.
Tabia ya kupatwa na bawasiri pia yaweza kuwa ni ya kurithi na huzidi kadri umri unavyoongezeka.