Chakula na Tiba

Chakula na Tiba Karibuni wote mpate kujua chakula safi na namna kinavyotibu miili yetu na akili zetu.

21/10/2025

Siri Tiba ya Ukwaju Wengi Hawaijui Soma kwa makini Elimu hii...🩺

Usiuchukulie powa ukwaju —Ndani ya ganda lake la kawaida kumefichwa tiba asilia yenye nguvu zaidi kwa mwili wako....

Kitaalamu, ukwaju una asidi ya tartaric, potassium, magnesium, na polyphenols —Mchanganyiko unaosaidia...👇

↳ Kupunguza uchovu na kusafisha damu kwa kuondoa taka za metabolic waste...

↳ Kurekebisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa kusisimua bile secretion na kupunguza gesi, kujaa, au choo kigumu....

↳ Kushusha cholesterol na sukari ya damu kupitia fiber yake inayodhibiti absorption ya glucose.

↳ Kusafisha ini (liver detox) kwa kuongeza ufanisi wa enzymes za kuondoa sumu.

↳ Kupunguza uvimbe mwilini (inflammation) — chanzo kikuu cha magonjwa sugu k**a pressure, kisukari, na uzito kupita kiasi.....

↳ Kwa wanaume, ukwaju huamsha mzunguko wa damu na kusaidia kurejesha stamina asilia bila dawa za kuongeza nguvu.

↳ Kwa wanawake, husaidia kusawazisha homoni na kupunguza bloating hasa kipindi cha hedhi....

NB: Anza Tiba ya kutumia Ukwaju leo, Chemsha kijiko 1 cha ukwaju mbichi (au kavu) katika glasi 1 ya maji ya uvuguvugu, Ongeza asali kidogo, Kunywa asubuhi kabla ya chakula kwa siku 14.

Matokeo yake hayachelewi— Utahisi mwili wako unaamka, tumbo linatulia, ngozi inang’aa, na nguvu zinarejea...💪

Ukwaju sio ladha tu, Ni tiba ya mfumo mzima wa mwili wako.

Kumbuka hili: Daima tiba huanzia kwenye sahani yako ya chakula, sio kwenye maduka ya dawa....🫵

21/10/2025

🍌UKIMALIZA KULA NDIZI USITUPE MAGANDA YAKE (BANANA PEELS) .

1️⃣ KWA AJILI YA NGOZI
sugulia ile nyamanyama ya maganda kwenye ngozi ili utibu chunusi,na madoamadoa ya ngozi na uso wako.Usioshe hadi ipite nusu saa au saa nzima.

2️⃣ KWA AJILI YA VIDONDA
Weka au valisha ganda la ndizi ligusane na kidonda utapona.

3️⃣ KWA AFYA YA MOYO
Chemsha kwa dakika15-20 kisha kunywa glasi asubuhi na jioni .

4️⃣ KWA AFYANYA MENO NA FIZI
Sugulia meno yako na maganda hayo kwa dakika 2 hadi 3 .Hufanya pia meno kuwa meupe.

5️⃣ KWA AJILI YA KUSUUZA MWILI ULIOCHOKA NA KUPATA USINGIZI MZURI.
Chemsha kwa dakika15-20 kisha kunywa glasi moja kabla ya kulala ,utalala k**a mtoto mchanga.

Maandalizi ya dawa :

Osha maganda yawe masafi, katakata vipande vidogovidogo kisha chemsha kwenye chombo kwa dakika15-20.
Chuja na kunywa glasi moja. Ongezea na asali kwa ajili ya ladha kijiko kimoja cha chakula cha asali.

Kunywa sasa

Danieli 1:8-20

Dawa ya vidonda vya tumbo
19/10/2025

Dawa ya vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo ni nini?Vidonda vya tumbo hufahamika kwa kiingereza k**a Peptic Ulcer ni hali ambayo kuna kidonda kwen...
19/10/2025

Vidonda vya tumbo ni nini?

Vidonda vya tumbo hufahamika kwa kiingereza k**a Peptic Ulcer ni hali ambayo kuna kidonda kwenye tabaka la tumbo au sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo. Dalili kuu ni hisia ya kuungua katika sehemu ya juu ya tumbo baada ya kula. Dalili nyingine ni kiungulia, kubeua, tumbo kujaa gesi na kichefuchefu. Dalili za vidonda vya tumbo huongezeka kadiri muda unavyoenda.Vidonda vya tumbo vinaweza kusababisha madhara ambayo huhitaji huduma ya dharura. Haya hujumuisha kutokwa damu au kuchimbika shimo katika tumbo la chakula. Madhara haya huweza kusababisha dalili kuanza kwa ghafla. Matibabu ya vidonda vya tumbo hutegemea sababu ya hali hii kutokea. Sababu hiyo ikishatambuliwa na kutibiwa, huwa na matokeo mazuri.

Mara nyingi mtindo mbaya wa ulaji na unywaji husababisha vidonda vya tumbo.

Pata dawa inayotibu kabisa na pia badilisha mtindo wa maisha ili kuepuka kuumwa tena baada ya kupona.

Mawasiliano: call/sms/WhatsApp +255760209793

FAIDA YA KULALA MASAA 8 kuanzia saa 3 mpaka saa 11 au saa 4 mpaka saa 121. Hukusaidia kuwa na kumbukumbu nzuri2. Huupa m...
01/10/2025

FAIDA YA KULALA MASAA 8 kuanzia saa 3 mpaka saa 11 au saa 4 mpaka saa 12

1. Hukusaidia kuwa na kumbukumbu nzuri

2. Huupa mwili na akili nafasi ya kujikarabati upya(restoring)

3. Unapata nafasi nzuri ya ubongo kupangilia taarifa kichwani na kuepusha hitilafu katika akili yako

4. Kwa mtu ambaye bado umri wake uko katika hatua za makuzi inamsaidia kukua kwa haraka

5. Hupunguza msongo wa mawazo

6. Huondoa uchovu

7. Huruhusu upumzishwaji wa kichwa(saa 3 mpaka 6) upumzishwaji wa tumbo(saa 6 mpaka 9) na kisha miguu(saa 9 mpaka 11)

Mungu awabariki na kuwapa afya njema

27/12/2023

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Nafy Wa Ray, Zubely Haruna, Lucy Wangari, أبو حذافة, Rehema Bint Ally

07/08/2023

Afya yako ni uzima wako.

16/01/2023

MAMBO MUHIMU KATIKA ULAJI

1. Usinywe maji unapokula au baada tu ya kula ili kuepuka kuvuruga mfumo wa umeng'enywaji na kulipa tumbo tabu

2. Epuka vinywaji vyenye baridi au vilivyogandishwa katika friji ili mishipa laini ya ndani isiharibike

3. Kunywa maji nusu saa kabla ya kula chakula

4. Epuka kuongea na simu au kutazama televisheni ili ubongo ujikite kupeleka nguvu nyingi kwenye umeng'enyaji

5. Epuka matumizi ya vyakula na vinywaji vya viwandani ili afya yako iwe katika ubora.

6. Tumia mimea ya mboga mboga,nafaka na matunda zaidi ili kuwa na afya bora kuliko vitu vinavyotokana na wanyama k**a mayai, maziwa, nyama kwa aina zote n.k

23/12/2022

FAIDA ZA JUISI YA TANGAWIZI

PART II

1. Hutibu shinikizo la juu la damu
2. Husafisha utumbo mpana
3. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma
4. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI
5. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
6. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu
7. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu
8. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa
9. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula
10. Husaidia kuzuia kuharisha
11. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu
12. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto
13. Hutibu homa ya kichwa
14. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
15. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito
16. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)
17. Huimarisha afya ya figo
18. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi
19. Ina madini ya potassium ya kutosha
20. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita
21. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha
22. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium
23. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene
24. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

BLEND K**A UNAVYO TENGENEZA JUICE YA KAWAIDA KISHA KUNYWA GLASS MOJA KWA SIKU.

AU UNAWEZA KUJENGA MAZOEA YA KUTAFUNA VIPANDE KADHAA KILA SIKU ASUBUHI KABLA HUJALA KITU

23/12/2022

FAIDA ZA JUISI YA TANGAWIZI

PART 1

1. Huondoa sumu mwilini haraka sana.

2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi.

3. Kuna viua vijisumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi.

4. Huondoa uvimbe mwilini.

5. Huondoa msongamano mapafuni.

6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake.

7. Huondoa maumivu ya koo.

8. Huua virusi wa homa.

9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini.

10. Huondoa homa, hata homa ya baridi.

11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.

12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu k**a ‘gingerol'
13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-related cancer)

14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)

15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)

16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kansa mbalimbali za tumbo.

17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya t**i
18. Hutibu kansa za kwenye kizazi na kansa za kwenye mirija ya uzazi.

19. Huongeza msukumo wa damu.

20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo.

21. Huzuia damu kuganda

22. Hushusha lehemu(cholesterol)

23. Husafisha damu

24. Husaidia watu wenye kukak**aa kwa mishipa.

ASANTE KWA KUFATILIA MAKALA ZA AFYA. MUNGU AKUBARIKI.

Chakula kwa afya yako.
01/03/2022

Chakula kwa afya yako.

KITUNGUU SAUMU (GARLIC)

Ni mmea ambao una uwezo wa kutibu magonjwa mengi sana kutokana na kuwa na virutubisho vinavyopatikana katika mmea huo. Ni miongoni mwa mimeatiba ambayo imetumika zamani katika nchi k**a China, Rumi, Ugiriki, Misri na Babeli kwa tiba dhidi ya maradhi mbalimbali. Kitunguu saumu ni mmea jamii ya kitunguu maji.

FAIDA ZA KITUNGUU SAUMU

-Husaidia kuondoa mafuta machafu mwilini na kufanya damu ipite vizuri bila shida
-Hutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume
-HUamsha misuli iliyosinyaa
-HUkinga dhidi ya saratani ya ubongo na uvimbe katika seli za ubongo
-Hukinga dhidi ya saratani ya mapafu
-Hukinga dhidi ya bacteria na maradhi ya ngozi na pia fangasi wanaoshambulia ngozi
-Hushusha presha katika damu
-Hulinda mifupa isiharibike
-Huzuia magonjwa ya moyo
-Vitamin C na B6 hupatikana ndani yake na ni muhimu kwa ajili ya mwili
-Huzuia saratani ya kibofu cha mkojo
-Huzuia saratani ya mat**i na tatizo la kujfungua kabla ya wakati

MATUMIZI YA KITUNGUU SAUMU

-Tumia k**a dawa kwa kutafuna vipande vidogo vidogo ikiwa imekatwa
-Paka sehemu ya ngozi iliyoathirika na fangasi au bacteria
-Kula ikiwa imechanganywa na tangawizi pamoja na asali mbichi au katika kachumbari

ZINGATIA: Usile vitunguu saumu bila kuvikatakata ili kuepuka kudhurika na gesi iliyo ndani yake

Mungu akubariki na kukuwezesha kutumia vitu vya asili kwa ajili ya kuboresha afya ya akili na mwili.

Address

Segerea
Dar Es Salaam
12105

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chakula na Tiba posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Chakula na Tiba:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram