20/10/2023
weza kuota ni kwenye ovari, mirija ya uzazi (fallopian tubes), kuta za nje za nyumba ya uzazi, utumbo, pelvis, kuma , cervix, kibofu na mara chache kwenye maini, mapafu na ubongo.
Endometriosis imegundulika zaidi kwenye kundi la wanawake wenye umri kati miaka 25 na 35, ingawa mara chache
imeonekana kwa wasichana wadogo wa miaka k**a 11. Endometriosis ni nadra kuonekana kwa wanawake waliokoma hedhi. Wanawake warefu , wembamba wenye uzito mdogo huonekana zaidi na tatizo hili. Kupata ujauzito katika umri mkubwa sana, kutozaa na kukoma siku mapema huongeza uwezekan wa kutokea endometriosis.
Kuota kwa seli hizi za ziada – na tendo la kuziondoa kwa operesheni – huweza kusababisha makovu ambayo huweza kuzuia yai la mwanamke lisiungane na mbegu ya mwanamme. Kuathirika kwa utando huu juu ya uterus huweza kuzuia kutungwa kwa yai lililopevushwa.
SABABU NYINGINEZO
(i). SABABU Za KITABIA
Baadhi ya tabia zetu huathiri afya zetu ikiwa ni pamoja na afya ya viungo vya uzazi na kupunguza au kuondoa uwezo wetu wa kuzaa watoto. Bahati nzuri tabia hizi zinaweza kudhibitika.
Chakula Na Mazoezi: Ili tuwe na uwezo mzuri wa kuzaa watoto tunahitaji kupata chakula kizuri na kuipa miili yetu mazoezi ya kutosha. Wanawake wenye unene wa kupindukia au uzito mdogo sana wanapata shida kushika mimba.
Uvutaji Wa Sigara: Uvutaji wa sigara umethibitika kupunguza kiwango cha mbegu (low s***m count) kwa wanaume, kuongeza uwezekano wa mimba kutoka, kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo au kabla ya wakati (njiti) kwa wanawake.
Pombe: Unywaji wa pombe huongeza uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye matatizo na unywaji uliozidi huweza kuleta ugonjwa, Fetal Alcohol Syndrome. Kwa mwanaume, pombe hupunguza kiwango chake cha mbegu.
Madawa: Madawa k**a bangi (ma*****na) hupunguza kiwango cha mbegu kwa wanaume. Utumiaji wa co***ne kwa wanawake huathiri figo za watoto watakaozaliwa.
(ii). MAZINGIRA
Uwezo wa mwanamke kutunga mimba unaweza unaweza kuathiriwa na uwepo wake kwenye mazingira yenye sumu au kemika