20/02/2023
VIJANA CHANGAMKIENI FURSA ZA KILIMO ZILIZOTOLEWA NA MHE RAIS SAMIA
20 Februari, Tanga
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ccm Taifa Sophia Mjema Imeiagiza Halimashuri zote hapa nchini kuweka mfumo rafiki wa vijana kuweza kujiunga kwenye mtandao ili kuweza kunufaika na fursa ya kilimo iliyo tolewa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika ziara ya Sektetariet ya CCM Taifa wilayani Lushoto mkoani Tanga katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Sophia Mjema amesema kuwa Mhe.Rais ametoa zaidia ya Bilioni miatisa kwaajili ya mashamba ya umwagiliaji,mashamba yatakayo kuwa na dhana bora za kilimo na yatakayo letewa viwatilifu kwaajili ya vijana kuweza kujiondoa na umasikini na ikiwa ni mkakati wake wa kupambana na wimbi la ukosefu wa ajira hapa nchini.
"Lengo la Rais wetu ni kuwawezesha vijana kunufaika katika sekta ya kilimo ndomana ametoa fedha nyingi ili kuwawezesha vijana hapan nchinikuweza kujikwamua na umasikini na kwenda kwenye uchumi wa kati"Alisema Mjema
Aidha amemwagiza mkuu wa mkoa wa Tanga Omary Mgumba kuendelea kutemga maeneo kwaajili ya mashamba ambapo amesema kuwa baada ya kutengwa maeneo hayo nilazima vijana wausishwe jinsi ya kujaza fomu katika mtandao ili kuweza kuwa na uelewa wa namna ya kuweza kupata mashamba hayo.
"Mkuu wa mkoa wenu ambaye ni kamisaa wa Chama Cha Mapinduzi nime muelekeza na amesema ataleta wataalamu ambao watazunguka kwenye Halimashauri mbalimbali ndani ya Mkoa wa Tanga ili kuwasaidia vijana jinsi ya kujaza fomu kwaajili ya kupata nafasi ya kumiliki mashamba hayo kwani wengi wao hawana ulewa juu ya kujaza kwamba wanahitaji mashamba hayo"Alisema Mjema
Hata hivyo amewataka vijana kuchangamkia furasa hiyo ya kupata maeneo ya kilimo ili kuweza kujiajiri kwani hizo ni moja ya jitihada za Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayo ongozwa na Mhe.Rais Samia Suluh Hassan katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana hivyo amewataka vijana kuchangamkia fursa hiyo.