01/07/2025
Wiki iliyopita tulitembelea wakulima wetu, tukawapatia kamba mpya na kuwafundisha mbinu rafiki ya kufunga kamba kwa kamba (tie rope end to end) k**a njia bora ya sasa badala ya kutumia vijiti vya miti ambavyo vinachangia uharibifu wa mazingira. 🌍 Mbinu hii inasaidia kulinda mazingira na kuboresha kilimo cha mwani.
Hatua kubwa tuliyochukua ni kusaini mikataba mipya na wakulima wetu, ambapo sasa Afro Nature itakuwa inanunua mwani wao wote kwa uhakika – hatua inayowapa wakulima uhakika wa soko na kipato endelevu. 🤝
Zaidi ya hapo, tumewasaidia kwa kuongeza kichanja kingine cha kukausha mwani. Mbinu hii ni bora zaidi kuliko kuanika mwani chini kwani inasaidia kuhakikisha mwani unakuwa msafi, hauna uchafu, unakauka vizuri na unabaki na rangi yake ya asili – jambo ambalo linatufanya Afro Nature kusimama tofauti sokoni kwa kuwa na mwani safi na salama.
Pamoja tunajenga mustakabali safi, wa kijani, na jumuishi – kwa kila u*i wa mwani tunaozalisha. 💚🌊
🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿
Last week, we visited our farmers to deliver new ropes and trained them on the rope-to-rope method—a sustainable alternative to using tree pegs, which contributes to deforestation. 🌍 This simple shift helps protect the environment while improving farming practices.
We also took a major step forward by signing new contracts with our farmers, officially committing to buy all their seaweed harvests—ensuring them a reliable market and stronger income stability. 🤝
To support their production, we added another drying rack (kichanja). This method is a big improvement from drying seaweed on the ground. It helps maintain cleanliness, reduces contamination, and ensures the seaweed retains its natural color and quality—a key reason why Afro Nature seaweed stands out in the market.
Together, we are building a cleaner, greener, and more inclusive future—one seaweed strand at a time. 💚🌊