16/10/2023
Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya TANZANIA Paralympic Committee ndugu Ernest Nyabalale alikuwa ni miongoni mwa wachezaji walioiwakilisha timu ya kuogelea ya TPC. TPC imeshiriki ikiwa ni miongoni mwa timu 11 zilizoshiriki Mashindano ya kuogelea ya kwanza ya Taifa kwa watu wenye ulemavu Tanzania 🇹🇿. Ernest ameshika nafasi ya tatu baada ya kutanguliwa na wachezaji wawili wa timu ya ZANZIBAR Talent Swimming CLUB kutoka Zanzibar katika mtindo wa freestyle katika bwawa la GYMKHANA CLUB DAR ES SALAAM.