12/12/2025
Leo mapema Taasisi ya Saratani Ocean Road imepokea msaada wa vifaa tiba kutoka BMG Group International Limited.
Vifaa hivyo vimepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya saratani ocean road Dkt. Diwani Msemo.
Dkt. Msemo amesema Taasisi imepata faraja kubwa pamoja na wagonjwa watafarijika kwa msaada huo kwa kuwa msaada huo utarahisisha moja kwa moja huduma kwa wagonjwa.
Dkt. Diwani ameongeza kwa kusema kitendo hicho kilichofanywa na BMG Group International ni kitendo kilichotukuka na Taasisi itahakikisha vifaa vyote vitatumika kwa ajili ya wagonjwa husika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa BMG Group International Bw. Amani Temu amesema msaada huo waliotoa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii na Ili kuifikia jamii kwa ufanisi ni kutoa msaada huo kwa Taasisi ya saratani ocean road.
Bw. Temu amesema msaada huo waliotoa utaongeza zaidi ufanisi wa watumishi wa Taasisi ya saratani ocean road katika kurudisha afya njema kwa wagonjwa wa Saratani.