27/10/2025
UGONJWA WA GAUT NI NINI?
Gauti (Gout) ni aina ya ugonjwa unaoathiri viungo vya mwili unaosababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya Urea (uric acid) katika damu.
Ongezeko la uric acid husababisha madhara katika jointi (joint) (joint ni sehemu ya mwili inapokutana/ inapoungana mifupa miwili). Gauti inaweza kutokea ghafla (acute gout) au ikawa sugu (chronic gout). Gauti inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri jointi moja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri jointi zaidi ya moja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye jointi.
Visababishi vya Gaut
Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha uric acid katika damu. Hali hutokea iwapo mwili wa mgonjwa unatengeneza uric acid nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa uric acid mwilini k**a inavyotakiwa.
Ongezeko hili husababisha mrundikano wa uric acid katika maji maji yanayozunguka jointi yanayoitwa synovial fluid na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogo vidogo vya tindikali ya urea yaani uric acid crystals ambavyo husababisha jointi kuvimba na hatimaye kuathirika.
Vihatarishi (risk factors)
Ingawa chanzo hakieleweki vema, ugonjwa wa gauti hutokea kuwapata baadhi ya watu walio katika familia moja. Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi kuliko wale wanaoendelea kupata hedhi.
1. Unywaji wa pombe na uvutaji wa sugars.
Unywaji pombe na sigara unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu.
2. Matumizi makubwa ya baadhi ya madawa k**a vile dawa za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uric acid katika damu.
3. Magonjwa k**a kisukari, magonjwa ya figo, unene uliopitiliza, ugonjwa wa sickle cell anemia au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia)
Dalili
Dalili za gauti kwa kawaida uhusisha jointi moja au joint chache. Jointi zinazoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa ha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu.
Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla hususani nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali k**a kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana.
Jointi hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe). Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye jointi yenye matatizo.
Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu, lakini pia laweza kujirudia mara kwa mara.
Pia mgonjwa anaweza kujihisi homa.
Baadhi ya wagonjwa hupata gauti sugu ambayo huwaletea madhara sugu katika jointi (chronic arthritis) hali ambayo husababisha mgonjwa kujihisi maumivu na muda mwingi kushindwa vizuri kutumia jointi zake. Wagonjwa wenye gauti kwa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka jointi zilizoathirika. Vinundu hivi kwa kitaalamu huitwa trophy na ni ishara ya muhimu kwa madaktari.
Vipimo
1. Vipimo vya damu
Kiwango cha uric acid katika damu. Hata hivyo, si kila aliye na kiwango kikubwa cha uric acid katika damu huwa na gauti.
Kiwango cha uric acid katika mkojo
Uchunguzi wa maji maji yanayozunguka jointi (synovial fluid) kuchunguza vijiwe katika jointi
2. X- ray ya jointi iliyoathirika
3. Synovial biopsy chunguzi wa utando unaozunguka jointi
Matibabu
Matibabu ya gauti hujumuisha matumizi ya dawa mbali mbali za maumivu, virutubisho lishe pamoja na mabadiliko katika mfumo wa maisha ya mgonjwa.
Lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha husaidia pia kuthibiti na kumuepusha mgonjwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya gauti. Njia hizi ni pamoja na:
Kuacha kunywa pombe
Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye viasili vya purine (aina ya protini) k**a vile nyama ya mbuzi, samaki jamii ya sardines na herring, nyama ya maini au figo, mkate mtamu, maharage yaliyokaushwa, njegere, baadhi ya aina za uyoga, spinachi, n.k.
Thibiti pia ulaji wa nyama kwa kila mlo unaokula
Jiepushe na matumizi ya vyakula vya mafuta k**a vile ice creams, mayonise au vyakula vya kuokwa
Kula kiasi kikubwa cha wanga
Iwapo utaamua kupunguza uzito, hakikisha unapunguza kidogo kidogo kwa sababu upunguzaji wa kasi unaweza kusababisha vijiwe vya uric kujitengeneza katika figo
Matarajio
Madhara ya gauti
Gauti inaweza kusababisha matatizo sugu kwenye jointi (chronic gouty arthritis)
Vijiwe katika figo
Mrundikano wa uric acid unaoweza kusababisha ugonjwa sugu wa figo
Ili kupunguza kiwango cha uric acid katika damu,na kuondoa maumivu katika Viungo kwa njia ya ASILI pasipokuongeza sumu mwilini wasiliana nasi 0718105628