Isaya Febu

Isaya Febu Tunawasaidia wanaume na wanawake kutatua changamoto za afya ya uzazi kwa kutumia virutubisho.

Je Unasumbuliwa Na Fangasi Ukeni Kwa Muda Mrefu? K**a Jibu Ni NDIYO Soma HapaUkeni ni makazi ya Bacteria...Ukeni kuna ba...
23/11/2025

Je Unasumbuliwa Na Fangasi Ukeni Kwa Muda Mrefu? K**a Jibu Ni NDIYO Soma Hapa

Ukeni ni makazi ya Bacteria...

Ukeni kuna bacteria wazuri wanaoitwa Lactobacillus

Lakini pia,

Kunabacteria wabaya k**a vile E-coli , mycetes na wengine wanaoweza kusababisha Maambukizi ukeni

Wote huishi pamoja bila madhara, wakiendelea kupambana kila siku na kubalance kiwango chao

Bacteria wote hao huwa hawaleti matatizo, mtu hupata Maambukizi baada ya haya kutokea...

1) Baada ya mabadiliko ya uke PH au acid ukeni yanayoweza kusababishwa na...

Kufanya mapenzi,

mbegu always ni alkaline hivyo hupelekea mabadiliko ya Bacteria

Ambapo mabadiliko ya PH ni sawa na kuharibu Mazingira yao

Hilo hufanya bacteria wabaya kumultiply au kuongezeka kwa haraka kiasi ambacho bacteria wazuri hushindwa kuwazuia

Kuosha uke kwa sabuni au marashi

Hedhi inavyotoka pia huharibu PH ya uke na kuongeza hatari

2) Kuvaa nguo za kubana

Uke unahitaji hewa safi k**a sehemu nyingine

Nguo za ndani zinazobana, majinsi hupelekea uke kushindwa kupumua na hali ya joto kuzidi

Hilo husaidia ukuaji na kuzaliana kwa kasi kwa Fangasi ukeni na kumdhuri mtu

3) Kujipangusa vibaya, kutoka nyuma kuja mbele na kuvaa nguo chafu

Huwafanya hata wale bacteria ambao wanaishi kwenye kinyesi kuja kwenye uke,

hapo huongeza hatari ya kupata Maambukizi

4) Njia za uzazi wa mpango na Dawa kila mara

Dawa za kuweka ukeni, hupelekea mabadiliko ya PH

Lakini pia antibiotics huua aina zote za bacteria, hivyo hata bacteria wazuri hufariki ambao ndio walinzi (Lactobacillus )ukeni

Njia za uzazi wa mpango hasa za uingizaji wa kifaa kwenye mji wa mimba

K**a usafi hautafanyika basi hutengeneza njia ya bacteria kuingia kwenye kizazi

5) Kutumia mate ukeni au kunyonya

Hupelekea bacteria wa mdomoni kuja ukeni, ambapo hupelekea mabadiliko ya tofauti

Hali inayoongeza udhaifu na mwanya wa bacteria kuingia kwenye kizazi

By the way, k**a wewe unachangamoto ya Maambukizi ukeni

Basi wasiliana nami kwa kubonyeza hii link: https://wa.me/+255625305487 ili kupata matibabu ambayo yatakufanya usiwe mtumwa wa dawa kila mara

Kumbuka: kupuuzia maambukizi ukeni ni kupuuzia uzazi wako, ni kupuzia ndoa yako na ni kupuzia uhai wako

Je Mwanaume Anaweza Kuugua PID?Mwanaume hawezi kupata PID… Lakini mzigo wa PID ya mwenzi wake mara nyingi humuangukia ki...
23/11/2025

Je Mwanaume Anaweza Kuugua PID?

Mwanaume hawezi kupata PID… Lakini mzigo wa PID ya mwenzi wake mara nyingi humuangukia kimya kimya.

Huu si uvumi—ni hali halisi katika mahusiano mengi ya sasa.

Jana usiku nilipokea ujumbe mzito kutoka kwa kijana mmoja aliyekuwa na hofu na mawazo mengi…

Ujumbe wake ulikuwa hivi…

“Daktari, nimekuwa na wasiwasi sana. Mpenzi wangu amekuwa na harufu mbaya ukeni na chupi yake ina ute wa rangi ya njano. Kila tukifanya tendo la ndoa nabaki nikiwa na hofu ya kuambukizwa.Nikipendekeza twende hospitali anachukia sana. Naomba unisaidie kuelewa huu ni ugonjwa gani.”

Hili ni tatizo linalomuumiza mwanamke kiafya na mwanaume kisaikolojia…

PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ni maambukizi yanayopanda kwenye kizazi cha mwanamke na kuathiri mfuko wa uzazi, mirija ya mayai na ovari.

Chanzo mara nyingi ni magonjwa ya zinaa k**a Chlamydia au Gonorrhea ambayo huingia kimya bila dalili za haraka.

Dalili ambazo mwanamke anaweza kupitia:

Ute wa njano au kijani

Harufu kali isiyo ya kawaida ukeni

Maumivu ya chini ya tumbo

Maumivu wakati wa tendo la ndoa

Kwa mwanaume:

Hawezi kuugua PID moja kwa moja, lakini anaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa kutoka kwa mwenzi aliyeathirika, na kuanza kupata dalili k**a:

Maumivu wakati wa kukojoa

Kuwashwa au kuungua sehemu za siri

Kuvimba korodani

Maambukizi ya njia ya mkojo

PID ni ugonjwa unaovunja mahusiano kisirisiri—mwanamke anaumia mwilini, mwanaume anaumia moyoni.

Ikiachiwa bila matibabu, PID husababisha:

Ugumba

Maumivu ya nyonga yasiyokoma

Hatari ya mimba nje ya kizazi

Kuongezeka kwa mimba kuharibika

Wito kwa wanaume:

Ukiona mabadiliko kwa mwenzi wako, mtoe hofu, sio lawama.

Mshawishi kwa upendo, si kwa hasira.

Mpendekeze kwenda kufanya vipimo mapema.

Wito kwa wanawake:

Usione aibu kutafuta matibabu.

PID hutibika kabisa ikigundulika mapema.

Afya yako ni muhimu kuliko kuhofia lawama.

Elimu, uaminifu, na hatua za haraka ndizo kinga ya kwanza ya mahusiano yenye afya.

Kwa msaada wa matibabu ya asili (kunywa+kunawia ukeni) ya ugonjwa wa pid kwa wanawake wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487

Hii Nayo Ni Miongoni Mwa Sababu Inayokufanya Mwanaume Unashindwa Kufurahia Tendo La Ndoa kwenye Mahusiano Yako.Miongoni ...
23/11/2025

Hii Nayo Ni Miongoni Mwa Sababu Inayokufanya Mwanaume Unashindwa Kufurahia Tendo La Ndoa kwenye Mahusiano Yako.

Miongoni mwa sababu inayopelekea baadhi ya wanaume kushindwa kufurahia tendo la ndoa kwenye mahusiano yao ni pamoja na ugonjwa wa pid kwa wenzi wao.

Kwa kawaida mwanaume haumwi PID..Lakini anaumia kimyakimya kwa sababu ya PID ya mpenzi wake.

Hii siyo hadithi ya mtu mmoja, ni ukweli unaoishi katika ndoa na mahusiano mengi ya sasa…

Jana jioni nilipokea ujumbe mzito kutoka kwa kijana mmoja aliyejaa hofu na sintofahamu…

Na Nukuu Ujumbe Wake…

“Doctor… kuna jambo linaninyima raha kabisa. Mpenzi wangu anatoa harufu mbaya sana ukeni, na kwenye chupi yake kuna uchafu wa njano, Kila tukishiriki tendo la ndoa, najikuta sina amani kabisa, Niko kwenye hofu kubwa ya kuambukizwa, Mbaya zaidi, nikimwambia, ananijia juu kwa hasira, Naomba msaada, ni ugonjwa gani huu?”

Hili si jambo la kupuuzia….

Ni ugonjwa hatari wa mfumo wa uzazi kwa mwanamke, lakini madhara yake huwatesa kimya wanaume pia…!

PID (Pelvic Inflammatory Disease)…

Ni maambukizi ya bakteria wanaoathiri kizazi cha mwanamke — Mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi (fallopian tubes), na mayai (ovaries)….

Become a member
Visababishi vikuu ni magonjwa ya zinaa k**a Gonorrhea na Chlamydia, yanayoingia bila dalili za haraka….

Matokeo yake…?

Mwanamke hupata uchafu wa njano au kijani, harufu kali ya uke, maumivu ya tumbo, na wakati mwingine maumivu wakati wa tendo la ndoa…

Mwanaume hawezi kuugua PID, lakini anaweza kuambukizwa madhara ya zinaa kutoka kwa mwanamke aliyeathirika na hata kupata maambukizi ya korodani au mkojo…

(PID ni miongoni mwa magonjwa yanayobomoa mahusiano kimya kimya)

Mwanamke anaumia ndani kwa ndani, lakini mwanamume huathirika kisaikolojia, kimwili, na kiakili…

Na ikiwa haitatibiwa mapema, PID…

Husababisha ugumba, maumivu ya kudumu ya nyonga, na hata mimba kuharibika na mimba za nje ya kizazi. (ectopic pregnancy) …

NB: Wito kwa wanaume, K**a unahisi mabadiliko haya kwa mwenzi wako, usinyamaze…

Ongea kwa upendo, mshauri mkafanye vipimo hospitalini…

Wito kwa wanawake, Usiogope, usione haya, PID hutibika mapema na kupona kabisa…

Pamoja tukemee magonjwa ya uzazi kwa elimu sahihi na uamuzi wa kwenda hospitali kwa wakati..

10/09/2025

I got over 10 reactions on one of my posts last week! Thanks everyone for your support! 🎉

Kitunguu Maji Na Nguvu Za Kiume.Kitunguu Maji:Kitunguu maji kimekuwa kikitumika kwa miaka mingi k**a tiba ya asili kwa k...
16/08/2025

Kitunguu Maji Na Nguvu Za Kiume.

Kitunguu Maji:

Kitunguu maji kimekuwa kikitumika kwa miaka mingi k**a tiba ya asili kwa kuongeza nguvu za kiume na afya ya uzazi kwa wanaume. Kinachofanya kitunguu kuwa na nguvu hii ni kwa sababu ya kemikali asilia na virutubisho vilivyomo ndani yake.

Faida Za Kitunguu Maji Kwa Nguvu Za Kiume:

Faida za kitunguu maji kwa nguvu za kiume ni pamoja na:

1) Huchochea Uzalishaji Wa Homoni Ya Testosteroni.

Tafiti zinaonyesha kitunguu maji huchochea ongezeko la homoni ya kiume iitwayo testosteroni inayohusiana moja kwa moja na hamu ya tendo la ndoa (libido) na nguvu za kiume.

2) Huboresha Mzunguko Wa Damu Mwilini.

Kitunguu maji kina viambato vinavyosaidia kupunguza msongamano wa damu kwenye mishipa na kuongeza mtiririko wake kuelekea sehemu za siri za mwanaume, jambo linalosaidia kusimama vizuri kwa uume.

3) Huongeza Stamina Na Nguvu Za Mwili.

Kwa kuwa kitunguu maji kina virutubisho k**a vitamin C, B6, madini ya chuma na foliki asidi (folate), husaidia kupunguza uchovu na kuongeza nguvu mwilini, hivyo mwanaume anapata uwezo wa kufanya tendo la ndoa bila kuchoka haraka.

4) Huimarisha Ubora Na Wingi Wa Shahawa.

Kitunguu maji kina madini ya zinki na antioxidants yanayosaidia kulinda mbegu za kiume dhidi ya uharibifu na kuongeza uwezo wa mwanaume kutungisha mimba.

Jinsi ya Kutumia Kitunguu Maji kuboresha Nguvu za Kiume:

Zifuatazo ni njia za kutumia kitunguu maji katika kuboresha kuboresha nguvu za kiume:

1) Juisi Ya Kitunguu Maji.

Chukua kitunguu maji 1–2, menya, saga kupata juisi yake.
Changanya na kijiko kimoja cha asali.
Kunywa mchanganyiko huo (juisi ya kitunguu maji+asali) mara moja kwa siku, hasa usiku kabla ya kulala.

2) Kuchanganya Na Asali.

Kata vipande vidogo vidogo vya kitunguu maji, weka kwenye glasi ya maji vuguvugu, ongeza asali kisha unywe mchanganyiko huo.

HITIMISHO:

Usitumie kupita kiasi (zaidi ya vitunguu 2 vikubwa kwa siku) kwani huweza kusababisha gesi tumboni na kiungulia.

Epuka k**a una vidonda vya tumbo au mzio wa kitunguu.

Epuka kutumia kitunguu maji kibichi sana ikiwa una tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni (halitosis).

Kwa matokeo mazuri, tumia kitunguu maji pamoja na kuishi mtindo bora wa maisha ikiwemo kula lishe bora, kufanya mazoezi na kuepuka matumizi ya pombe na sigara kupita kiasi.

Kwa kifupi, kitunguu maji ni chakula cha asili chenye mchango wa kweli kwenye kuimarisha nguvu za kiume na afya ya mfumo wa uzazi wa mwanaume.

Faida Za Kitunguu Maji Kwa Mwanaume.Kitunguu Maji:Kitunguu maji kwa kiingereza: Onion, ni kiungo ambacho kinatumika sana...
15/08/2025

Faida Za Kitunguu Maji Kwa Mwanaume.

Kitunguu Maji:
Kitunguu maji kwa kiingereza: Onion, ni kiungo ambacho kinatumika sana jikoni katika mapishi kwa karne nyingi. Lakini pia ni kiungo kinachojulikana sana duniani kwa ladha yake ya kipekee na faida nyingi kiafya kwa sababu kina virutubisho vingi na kemikali asilia zinazosaidia afya ya mwili wa mwanaume kwa ujumla.

Leo katika mada yetu ya ukurasa huu tutazungumzia baadhi ya faida za kitunguu maji kwa mwanaume Ungana nami katika kuchambua faida hizi.

1) Huimarisha Nguvu Za Kiume.

Kitunguu maji huboresha mzunguko wa damu kuelekea kwenye uume na kuchochea uzalishaji wa homoni ya kiume, testosteroni, ambayo ni muhimu kwa hamu (libido) na uwezo wa kufanya tendo la ndoa.

2) Huongeza Stamina Na Uwezo Wa Kudumu Kitandani.

Virutubisho vilivyomo kwenye kitunguu maji husaidia kuongeza nishati mwilini, hivyo kumruhusu mwanaume kushiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu bila kuchoka haraka.

3) Kuboresha Ubora Wa Shahawa.

Madini k**a vile zinki na antioxidants zilizopo kwenye kitunguu maji husaidia kuongeza wingi na ubora wa mbegu za kiume, jambo linaloongeza uwezo wa kupata mtoto.

4) Kuimarisha Kinga Ya Mwili.

Kitunguu maji kina vitamin C, ambayo inasaidia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili wa mwanaume na kuupa uwezo wa kupambana na magonjwa.

5) Kupunguza Hatari Ya Magonjwa Ya Moyo.

Kitunguu maji kina uwezo wa kusaidia kupunguza kiwango cha cholesterol mbaya (LDL) na kuongeza cholesterol nzuri (HDL), hivyo kuboresha mzunguko wa damu na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo kwa mwanaume.

6) Kusaidia Kudhibiti Kiwango Cha Sukari Mwilini.

Kwa mwanaume mwenye ugonjwa wa kisukari (type 2 diabetes), kitunguu maji kinaweza kusaidia kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu kutokana na uwezo wake wa kuongeza usikivu wa mwili kwa insulini (glucose tolerance).

7) Kuboresha Mfumo Wa Mmeng’enyo Wa Chakula.

Kitunguu maji kina nyuzinyuzi (dietary fibers) ambazo zinasaidia kuboresha mmeng’enyo wa chakula na kuzuia matatizo k**a vile kukosa choo (constipation) kwa mwanaume.

HITIMISHO:

Kwa hiyo, kitunguu maji ni kiungo muhimu ambacho kinaweza kusaidia katika kuboresha afya ya mwili wa mwanaume kwa ujumla. Kutumia kitunguu maji katika lishe yako ya kila siku kunaweza kuwa na manufaa mengi kwa mwili.

Faida Za Kitunguu Maji Kwa Mwanamke.Kitunguu Maji:Kitunguu maji kwa kiingereza: Onion, ni kiungo ambacho kinatumika sana...
15/08/2025

Faida Za Kitunguu Maji Kwa Mwanamke.

Kitunguu Maji:

Kitunguu maji kwa kiingereza: Onion, ni kiungo ambacho kinatumika sana jikoni katika mapishi kwa karne nyingi. Lakini pia ni kiungo kinachojulikana sana duniani kwa ladha yake ya kipekee na faida nyingi kiafya kwa sababu kina virutubisho vingi na kemikali asilia zinazosaidia afya ya mwili kwa ujumla.

Leo katika mada yetu ya ukurasa huu tutazungumzia baadhi ya faida za kitunguu maji kwa mwanamke. Ungana nami katika kuchambua faida hizi.

1) Kuimarisha Kinga Ya Mwili.

Kitunguu maji kina vitamin C, ambayo inasaidia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili wa mwanamke na kuupa uwezo wa kupambana na magonjwa.

2) Kupunguza Hatari Ya Magonjwa Ya Moyo.

Kitunguu maji kina uwezo wa kusaidia kupunguza kiwango cha cholesterol mbaya (LDL) na kuongeza cholesterol nzuri (HDL), hivyo kuboresha mzunguko wa damu na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo kwa mwanamke.

3) Kuzuia Saratani.

Baadhi ya utafiti unaonyesha kwamba viinilishe vilivyomo kwenye kitunguu maji k**a quercetin na sulfur compounds vinasaidia kupunguza hatari ya baadhi ya aina za saratani kwa wanawake k**a vile, saratani ya matiti, saratani ya ovari, saratani ya utumbo mpana (colon cancer).

4) Kusaidia Kudhibiti Kiwango Cha Sukari Mwilini.

Kwa mwanamke mwenye ugonjwa wa kisukari (type 2 diabetes), kitunguu maji kinaweza kusaidia kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu kutokana na uwezo wake wa kuongeza usikivu wa mwili kwa insulini (glucose tolerance).

5) Kuboresha Mfumo Wa Mmeng’enyo Wa Chakula.

Kitunguu maji kina nyuzinyuzi (dietary fibers) ambazo zinasaidia kuboresha mmeng’enyo wa chakula na kuzuia matatizo k**a vile kukosa choo (constipation) kwa mwanamke.

6) Faida Kwa Ngozi Na Nywele.

Kwa mwanamke, juisi ya kitunguu maji inaweza kutumika moja kwa moja kwenye nywele ili kuimarisha mizizi ya nywele na kupunguza upotevu wa nywele. Pia inaweza kusaidia katika afya ya ngozi kwa mwanamke kutokana na uwezo wake wa kuua bakteria na vimelea.

7) Kupunguza Uvimbe.

Kitunguu maji kina sifa za kupunguza uvimbe kutokana na viambato vyake k**a quercetin, ambavyo vinaweza kusaidia wanawake wanaougua magonjwa ya viungo au magonjwa sugu yenye kuambatana na uvimbe.

8) Husaidia Kudhibiti Usawa Wa Homoni Za Uzazi.

Baadhi ya tafiti zinaonyesha viambato vya kitunguu maji vinaweza kusaidia kuimarisha usawa wa homoni za uzazi, hivyo kusaidia mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida kwa mwanamke.

HITIMISHO:

Kwa hiyo, kitunguu maji ni kiungo muhimu ambacho kinaweza kusaidia katika kuboresha afya ya mwili wa mwanamke kwa ujumla. Kutumia kitunguu maji katika lishe yako ya kila siku kunaweza kuwa na manufaa mengi kwa mwili.

Mtoto Kuzaliwa Na Korodani Moja.Mtoto kuzaliwa na korodani moja ni hali ambapo mtoto ana korodani moja tu iliyoshuka kwe...
13/08/2025

Mtoto Kuzaliwa Na Korodani Moja.

Mtoto kuzaliwa na korodani moja ni hali ambapo mtoto ana korodani moja tu iliyoshuka kwenye mfuko wa korodani (sc***um), wakati korodani nyingine inaweza kuwa haijashuka (undescended), haipo, au imeondolewa. Hali hii inajulikana pia k**a monorchism.

Athari Za Kuzaliwa Na Korodani Moja:

Athari za kuzaliwa na korodani moja ni pamoja na:

1) Uwezo Wa Kupata Watoto.

Mwanaume mwenye korodani moja anakuwa na uwezo wa kupata watoto k**a kawaida, ikiwa korodani iliyopo ni yenye afya na inafanya kazi vizuri. Hii ni kwa sababu korodani moja hutoa mbegu za kiume na homoni ya kiume, testosteroni inayohitajika kwa uzazi na sifa za kiume.

2) Matatizo Yanayoweza Kuambatana.

Hali hii inaweza kuambatana na matatizo k**a vile:

Korodani nyingine kushindwa kushuka (cryptorchidism)
Kusokotwa kwa korodani (testicular torsion) ambayo ni hali ya mzunguko wa korodani na kusababisha maumivu makali
Upungufu wa homoni ya kiume au matatizo ya uzazi k**a vile mbegu kuwa chache sana au kufifia.

Ufuatiliaji wa afya: Ni muhimu kupimwa na kufuatiliwa na daktari wa uzazi au mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa uzazi ili kuhakikisha afya ya korodani iliyopo na uwezo wa uzazi.

Mfano Halisi:

Kuna watu wanaishi na korodani moja na waliweza kupata watoto wa kiume na wa k**e bila shida yoyote kubwa kiafya au ya uzazi.

Mambo Muhimu:

Hali hii haiathiri moja kwa moja uwezo wa kupata watoto ikiwa korodani iliyopo ina afya na inazalisha mbegu nzuri.
Hata hivyo, korodani moja ikiwa haifanyi kazi vizuri, inaweza kuathiri uwezo wa uzazi kwa mwanaume.
Kwa maumivu, uvimbe, au matatizo mengine yanayohusiana na korodani, ni muhimu kuonana na daktari kwa uchunguzi na matibabu.

Soma pia hii makala: https://isayafebu.com/korodani-moja-inazalisha/

HITIMISHO:

Kwa ujumla, mtoto kuzaliwa na korodani moja si tatizo kubwa kiafya k**a korodani hiyo ina afya na inatenda kazi vizuri. Ushauri wa daktari ni muhimu kwa uchunguzi wa kina na ufuatiliaji mzuri wa afya ya mfumo wa uzazi.

Jinsi Ya Kusafisha Uke Baada Ya Tendo La Ndoa.Baada ya tendo la ndoa, njia bora ya kusafisha uke ni kutumia maji safi ya...
11/08/2025

Jinsi Ya Kusafisha Uke Baada Ya Tendo La Ndoa.

Baada ya tendo la ndoa, njia bora ya kusafisha uke ni kutumia maji safi ya vuguvugu (running water) kusafisha sehemu za nje za uke kwa uangalifu.

Epuka kutumia sabuni au kemikali kali ndani ya uke kwani sehemu ya ndani ya uke huwa na uwezo wa kujisafisha yenyewe kwa asili (va**na is self cleansing).

Muhimu ni kujisafisha ukeni kutoka mbele kwenda nyuma (front to back) ili kuzuia bakteria k**a vile escherichia coli (E.coli) kutoka sehemu ya haja kubwa kuingia kwenye uke na kusababisha maambukizi k**a vile uti kwa wanawake.

Baada ya kujisafisha ukeni, jikaushe sehemu hiyo vizuri kwa kutumia taulo laini na kavu ili kuzuia unyevu unaodumu ambao unaweza kusababisha maambukizi zaidi k**a vile fangasi ukeni. Pia, kuvaa nguo za ndani (chupi) zenye pamba husaidia kupunguza unyevu na kuzuia ukuaji wa fangasi.

Zaidi ya hayo, ni vizuri kwenda haja ndogo baada ya tendo la ndoa kwani husaidia kusafisha njia ya mkojo na kuzuia bakteria kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo.

Vidokezo Muhimu Vya Kuzingatia:

Usitumie douches au sabuni zenye marashi au kemikali kali kujisafisha ndani ya uke.
Usijisafishe ukeni kupita kiasi kwani kunaweza kusababisha mabadiliko ya pH ya uke.
Fanya usafi wa sehemu za nje za uke tu kwa maji mara moja au mara mbili kwa siku au baada ya tendo la ndoa.

HITIMISHO:

Kwa ujumla, njia hii ni salama na inasaidia kuzuia maambukizi ukeni na matatizo ya afya ya uke. Ikiwa kuna dalili zisizo za kawaida k**a kuwashwa, maumivu, au kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni, wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487 kwa msaada wa ushauri na tiba ya uhakika.

Korodani Moja Inazalisha?Ndiyo, korodani moja bado inaweza kuzalisha mbegu za kiume za kutosha na kumwezesha mwanaume ku...
20/07/2025

Korodani Moja Inazalisha?

Ndiyo, korodani moja bado inaweza kuzalisha mbegu za kiume za kutosha na kumwezesha mwanaume kutungisha mimba. Hali ya kuwa na korodani moja kwa mwanaume hujulikana kwa kitaalamu k**a Monorchism.

Korodani ina jukumu la kuzalisha mbegu za kiume (sperms) na homoni ya kiume, testosteroni. Ingawa mwanaume wa kawaida ana korodani mbili, ikiwa moja imeondolewa au haifanyi kazi lakini nyingine ni yenye afya, mwanaume huyo anaweza kubaki na uwezo wa kuzalisha.

Mara nyingi, watu wenye korodani moja wanaendelea kuzalisha mbegu za kutosha k**a mwanaume aliye na korodani mbili.
Korodani moja inaweza kuchukua jukumu la korodani nyingine na kuzalisha kiasi cha kutosha cha mbegu na homoni za kiume zinazohitajika mwilini.

Hata hivyo, iwapo korodani pekee iliyobaki ina tatizo la kiafya k**a vile maambukizi, jeraha, au kasoro za kuzaliwa, inaweza kupunguza au kuondoa kabisa uwezo wa uzalishaji.

Kwa hiyo, uwepo wa korodani moja hauondoi uwezo wa uzazi, mradi tu korodani iliyobaki inafanya kazi vizuri kiafya.

Address

Majumba Sita
Dar Es Salaam
00255

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 20:00
Wednesday 09:00 - 20:00
Thursday 09:00 - 20:00
Friday 09:00 - 20:00
Saturday 09:00 - 20:00
Sunday 09:00 - 20:00

Telephone

+255625305487

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Isaya Febu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram