22/06/2022
Faida za Tende
1. Ukila tende mara kwa mara mwili wako utapata aina mbalimbali za madini na
vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili maarufu duniani.Katika
tende kuna kiasi kidogo tu cha mafuta (fat )na haina lehemu ( kolestrol).
2. Ukila tende, utajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B,
A na C ,virutubisho ambavyo ni muhimu
kwa ustawi wa afya ya mwili wako kwa ujumla .
3. Ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni , hivyo
utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu
kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids ’ ambavyo ni muhimu mwilini.
4. Ukila tende, mwili utapata nguvu na kukuondolea uchovu ndani ya nusu saa tu,kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia k**a vile ‘glucose’ , ‘ sucrose’na ‘ fructose’ . Ili kupata faida zaidi za tende,changanya na maziwa fresh kisha kula.Unapojisikia mchovu ,badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu,kula tende , hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa wafunga saumu ,ndiyo maana inashauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili wako nguvu iliyopotea siku nzima .
5. Tende ina madini pia aina ya
‘potassium ’ na kiasi kidogo cha chumvi(sodium) . Madini haya husaidia uimarishaji
wa mishipa ya fahamu. Watafiti
wamegundua kwamba ulaji kiasi wa ‘potassium ’ huweza kumuepusha mtu na
kupatwa na kiharusi (stroke ). Pia tende husaidia kupunguza lehemu (cholesterol )mwilini ( LDL Cholesterol ).
6. Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kuishiwa damu mwilini (anemia) ,wanaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini .Wakati vitu vitamu vingine huozesha meno,utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.
7. Husaidia tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo.
Kwa Maelezo na ushauri zaidi kuhusu Afya ya uzazi(Nguvu za kiume). Tuma Neno RIJALI Kwenda WhatsApp namba +255 742 216 182.