14/01/2024
Ili kusaidia mifumo yetu ya kusaga chakula iwe na hali nzuri lazima kuzingatia yafuatayo:
1. Epekaneni na ulaji vyakula vya baridi
2. Pendeleeni zaidi matumizi ya ngano ambayo haijakobolewa
3. Unga wa Dona muhimu kuliko sembe. Wenye afya migogoro tumieni Mchele wa brown zaidi ya ule mweupe, Ulezi na mtama pia ni nzuri
4. Matumizi ya vyakula vilivyokaangwa iwe kwa nadra sana
5. Matumizi ya Samuli yana manufaa kwenye chakula
6. Tafuneni chakula vizuri kabla ya kumeza
7. Miloo ipishane kwa masaa yasiyo chini ya matano
8. Chakula lazima kiwe na ladha nzuri
9. Usilale bada tu ya kula. Angarau chukuwa lisaa limoja au hata mawili ili kuruhusu mfumo wa kusaga chakula ufanye kazi. Isipokuwa k**a ni mwenye kuumwa njaa mara kwa mara, unaweza kula matunda. Lakini pia unywaji chai kupunguza hamu ya kula ya mara kwa mara
10. Chakula cha asubuhi ni kabla ya saa mbili, chakula cha mchana ni kuanzia saa sita hadi nane kasorobo, kitafunwa saa tisa na nusu hadi kumi. Chakula cha usiku kabla ya saa mbili usiku. Ukipitiwa mida hii bila kula, unaweza kula matunda
11. Kunyweni chai hata mara mbili kwa siku. Zingatieni matumizi ya mimea niliyo zungumzia kwenye message za mwanzo. Hata watoto wapeni chai: Majani ya molonge, Majani ya Kashwagara (wild or holy Basil), mchai chai, au tangawizi kiasi, au mdalasini, na majani ya wild sage; mimea yote hii unaweza kuipata bure kabisa maana ipo kila sehemu. Chai yako ikiwa na mimea k**a hii miwili hadi mitatu kinga itakuwa ngangari
12. Nyama nyekundu siyo sawa kwa kila mtu. Ukiona ukiila unakaa siku mbili bila kupata choo, au ukawa unapata choo ngumu achana nayo, usiimeze hata kakipande, ila supu yake unaweza kunywa
Wanaokunywa damu mbichi kumbukeni hata wanyama wana magonjwa ya mambukizi. Lakini pia kuna watu ambao mifumo yao ya kusaga chakula imesha haribika na haiwezi kusaga damu mbichi
13. Maziwa fresh yachanganywe na maji kwa wenye afya migogoro na hata watoto.
14. Kukeni matunda na mboga mboga
15. Niombeeni Mungu atubariki mimi na wanagu