Tabibu Fadhili Paulo

  • Home
  • Tabibu Fadhili Paulo

Tabibu Fadhili Paulo Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa tiba asili, nauza dawa za Asili. Nipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam Tanzania.

Simu|WhatsApp +255714800175

Ukiona umependezwa na huduma yangu usisahau kuniunganisha na ndugu, rafiki na jamaa zako wengine.

Je ungependa kuwa karibu na mimi kwa elimu ZAIDI kuhusu afya ya mwanaume na maisha ya mwanaume kwa ujumla?K**a jibu lako...
06/01/2026

Je ungependa kuwa karibu na mimi kwa elimu ZAIDI kuhusu afya ya mwanaume na maisha ya mwanaume kwa ujumla?

K**a jibu lako ni ndiyo, basi jiunge na group langu la WhatsApp linaitwa JANDO BILA GANZI kwa kubonyeza tu hapa 👇

https://chat.whatsapp.com/FbqtEPSyJSgBUWBVdwqrmC

Zingatia haya kabla hujajiunga na group langu

1. Nahitaji wanaume tu kwenye group langu, k**a wewe bado ni mvulana subiri kwanza utakapokuwa tayari mwanaume utajiunga

2. Ni group kwa ajili ya wanaume tu, Tafadhali wanawake msijiunge nikikugundua ni mwanamke umejiunga kwenye group letu nitakutoa haraka na viboko juu, ila k**a una mtoto wako wa kiume ungependa ajiunge kwenye group letu nijulishe kwenye WhatsApp tutamuunga kambini

WhatsApp Group Invite

VYAKULA AMBAVYO MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO HATAKIWI KULAMgonjwa wa vidonda vya tumbo ni lazima uwe makini sana na chak...
30/12/2025

VYAKULA AMBAVYO MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO HATAKIWI KULA

Mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni lazima uwe makini sana na chakula unachokula kila siku.

Chakula unachokula kila siku kitaamua ikiwa dawa unayotumia kutibu vidonda vya tumbo itakuponya na kukuacha huna vidonda tena milele au ndiyo utapata nafuu ya muda mfupi tu na baadaye utaendelea kuumwa vidonda tena na tena mpaka utakapokata tamaa.

Chakula unachokula kinapaswa kiwe ni dawa pia. Ulivyo ni kile unachokula kila siku.

Usile tu ili kushiba au kwa sababu unasikia njaa.

Lazima ujuwe hiki unachokula ni nini, kina kazi gani mwilini na je kinaweza kusaidia kupona au kupunguza makali ya vidonda vya tumbo?

Hiki unachokula ni nini?

Kina kazi gani mwilini?

Je kinaweza kusaidia japo kupunguza gesi au kupunguza asidi tumboni na kutibu vidonda au majeraha tumboni?.

Kanuni ya jumla ya chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo kwa siku ni kuwa asilimia 80 ya chakula unachokula katika siku iwe ni mboga za majani na matunda.

Hii ni kusema k**a jumla ya chakula unachokula kwa siku kina ujazo wa kilo 3 basi kilo 2 na nusu ziwe ni matunda na mboga za majani na nusu kilo iliyobaki ndiyo viwe vyakula vingine.

Cha kwanza kabisa unapoamka kitandani asubuhi, yaani ile unatua tu mguu kutoka kitandani ni maji ya kunywa.

Ukiamka tu kabla hata ya mswaki unapaswa unywe maji glasi moja (robo lita) au glasi 2 (nusu lita) ndiyo uendelee na maandalizi ya chai na kupiga mswaki na shughuli zingine.

Na hii ni kwa wote haijalishi unaishi sehemu zenye baridi au joto ni lazima kunywa maji.

Maji ya kawaida siyo ya kwenye friji wala siyo ya moto au ya uvuguvugu. Maji ya kawaida (room temperature).

VYAKULA AMBAVYO MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO HATAKIWI KULA:

1. Vyakula vya kusisimua

Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo.

Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua k**a vile ketchup, chill sauce, tomato sauce, achali, pilipili na vingine vingi vya jamii hii huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni.

Sababu ni kuwa, visisimuaji hivi huzichoma pia kuta za tumbo.

2. Vinywaji na vyakula vyenye kaffeina na asidi nyingi

Vinywaji vyenye kaffeina na asidi nyingi k**a vile chai ya rangi, kahawa, soya sauce, mayonnaise, jibini, Vyakula jamii ya Mkate, samaki wa kwenye makopo, pombe, soda na juisi za viwandani pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kutokea kwa vidonda vya tumbo.

3. MAZIWA Fresh

Kwa miaka mingi watu wenye vidonda vya tumbo wamekuwa wakihimizwa kunywa maziwa kwa wingi kwa matumaini kwamba yanaponyesha vidonda vya tumbo.

Utafiti wa karibuni umebaini maziwa si salama kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo.

Kwahiyo k**a umekuwa ukinywa vikombe na vikombe vya maziwa kwa matumaini unajiponya vidonda vya tumbo habari hii haikuachi salama

Ndiyo, ukinywa maziwa unaweza kusikia nafuu fulani kwa dakika kadhaa lakini baadaye hubadilika na kuwa mbaya zaidi

Ni vizuri zaidi kunywa maziwa mtindi kuliko maziwa fresh. Mtindi una bakteria wazuri mhimu kwa ajili ya tumbo na kinga ya mwili

Uchunguzi wangu umebaini watu wengi wanatumia dawa lakini hawajuwi wale nini na nini wasile, na hii ndiyo sababu kuu kwanini huponi vidonda vya tumbo hata baada ya kutumia dawa mbalimbali.

Vidonda vya tumbo ili upone siyo dawa peke yake, mhimu ni kujua nini ule na nini usile kwa kipindi kirefu kisichopungua miezi 6.

Ukiwa makini kwenye vyakula na vinywaji ninakuhakikishia kupona vidonda vya tumbo bila shida yoyote kwa asilimia 100

Kwa sehemu kubwa vidonda vya tumbo ni matokeo ya asidi kuzidi tumboni kwa muda mrefu mfululizo bila wewe kujua.

Kwa sababu hii kuendelea kunywa tena na tena maziwa katika siku kunapelekea kuundwa kwa hydrochloric acid ambayo ni chanzo pia cha vidonda vya tumbo.

Kuanzia leo punguza kabisa au ikiwezekana acha kabisa kunywa maziwa huku ukiendelea kutumia dawa na uone k**a hutaona tofauti

4. Chumvi NYINGI

Utafiti uliowahi kufanywa nchini marekani umeonyesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi nyingi na vidonda vya tumbo.

Angalia nimeandika chumvi nyingi, hii inamaanisha si kwamba hutakiwi kutumia chumvi, hapana unahitaji chumvi kila siku bali isiwe nyingi sana.

Mgonjwa wa vidonda vya tumbo anashauriwa kuepuka kula vyakula vyenye chumvi nyingi, HASA VYAKULA VYA KUSINDIKA AMBAVYO HUWEKWA CHUMVI NYINGI ili visiharibike haraka.

Pia jiupeshe na kuongeza chumvi mbichi kwenye chakula ambacho unakula.

Vitu vingine mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula au kunywa ni pamoja na sukari, vilevi vya aina yoyote, nanasi, karanga, maharage, dagaa, kuku wa kisasa, mayai ya kisasa, maandazi, nyama choma, wali wa pilau, wali mweupe, wali ulioungwa n**i nyingi unaweza kula mara 2 kwa wiki.

Orodha hii itaendelea kuboreshwa.

Pia ifahamike vyakula au vinywaji hivi haviruhusiwi kutumika kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo ili kumuongezea kasi ya uponyaji wa ugonjwa wake ila k**a wewe huumwi vidonda vya tumbo unaruhusiwa kuendelea kula na kunywa vinywaji hivi.

K**a unahitaji dawa ya asili inayotibu kabisa vidonda vya tumbo nipigie simu au niachie ujumbe kwenye WhatsApp 0714800175

Naitwa Fadhili Paulo ni tabibu wa tiba asili, nauza dawa za Asili, nipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.

Na ukinunua dawa kwangu ya kutibu kabisa vidonda vya tumbo nitakufundisha na vitu vingine vifuatavyo kuhusu vidonda vya tumbo BURE kabisa ;

1. Vyakula na vinywaji ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo anatakiwa kula kuanzia chakula cha asubuhi, cha mchana na cha jioni kwa siku 7 jtatu mpaka jpili.

2. Vyakula na vinywaji ambavyo havina asidi nyingi mwilini

3. Namna ya kuipunguza hydrokloriki asidi inayozarishwa tumboni wakati wa mmeng’enyo wa chakula isilete madhara ya kutoboa kuta za tumbo na kukuletea vidonda vya tumbo.

4. Mbinu nyingine nje ya vyakula na vinywaji za kupunguza asidi mwilini

5. Namna ya kumuua bakteria wa vidonda vya tumbo kwenye vyakula au vinywaji vya lazima unavyotumia kila siku.

6. Namna nzuri ya kudhibiti msongo wa mawazo (stress) kwenye maisha yako. Msongo wa mawazo ni moja ya sababu nyingine inayoongeza na kusababisha vidonda vya tumbo.

7. Madhara 9 ya kiafya yanayoletwa na vidonda vya tumbo na uhusiano wa vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo.

TAFADHALI SHARE POST HII KWA AJILI YA WENGINE

21/12/2025
JINSI YA KUACHA PUNYETOPunyeto ni tendo lolote la kujitafutia ashiki binafsi hasa kwa kuchochea viungo vya uzazi.Wanaoch...
07/12/2025

JINSI YA KUACHA PUNYETO

Punyeto ni tendo lolote la kujitafutia ashiki binafsi hasa kwa kuchochea viungo vya uzazi.

Wanaochukua hatua hiyo ili wajipatie kionjo cha kuridhisha kinachofanana na kile cha tendo la ndoa kwa kawaida wanasukumwa na msisimko uliowapata, pamoja na aibu ya kujitafutia mtu na hofu ya kuambukizwa maradhi ya zinaa.

Kufanya hivyo ni kupotosha maana ya jinsia kwa binadamu, ambayo ni kufanya wawili wawe kitu kimoja kwa nguvu ya upendo ambao huanzia rohoni na kukamilika katika muungano wa miili yao.

Upendo maana yake ni kujitoa kwa muungano na mpenzi unaoleta tunda lake katika mtoto, ambaye ni kwa pamoja wa baba na wa mama, akiwaunganisha upya ndani mwake.

Katika tendo la kujichua hakuna lolote kati ya hayo: hakuna upendo wala kujitoa kwa wengine, hakuna muungano wala uzazi, isipokuwa kujitafutia iwezekanavyo furaha ya kimwili (ashiki) iliyokusudiwa na Mungu kuwa sehemu ya furaha nzima ya muungano wa ndoa.

Katika tendo hilo la ubinafsi mtu yuko peke yake na kubaki peke yake: halengi chochote nje ya mwili wake, hivyo an**idi kuzama ndani mwake badala ya kustawi kwa kujiwekea malengo mema k**a vile ndoa, haki, huduma kwa wenye shida, utume n.k.

Matokeo yake ni kupoteza nguvu za mwili na hasa kuvuruga msimamo wa nafsi kwa kujisikia mnyonge, mwenye kosa na mtumwa wa tendo ambalo analikinai mara tu baada ya kulitenda. Hatimaye anaweza kupata matatizo katika tendo la ndoa.

Kwa msingi huo punyeto inahesabika kuwa dhambi kubwa, tena upande mmoja ni kubwa kuliko uasherati (kuzini kati ya msichana na mvulana), kwa sababu linakwenda kinyume cha maumbile na kuandaa njia kwa dhambi nyingine k**a vile ushoga.

Ushoga kwa asilimia fulani ni matokeo ya juu ya madhara ya kupiga punyeto.

Mtu anajiona uume wake hauinuki na hauna nguvu yoyote tena sasa mwisho wa siku anaona bora awe shoga tu.

Hata hivyo elimu nafsi inatueleza pia urahisi kwa mtu asiyekomaa kimapendo kufuata njia hiyo danganyifu, tena ngumu kuachwa baada ya kuzoeleka.

Punyeto ni uteja (Addiction) k**a ulivyo uteja mwingine wa vilevi k**a sigara, bangi, pombe, madawa ya kulevya na kadharika.

Uteja wowote ikiwemo na uteja wa kujichua husababishwa na kumikali mbili zilizopo kwenye ubongo zijulikanazo k**a ‘Dopamine’ na ‘endorphin’.

Dopamine ni transimita nyurolojia ambayo hukusaidia kujisikia raha.

Wakati endorphins ni homoni inayotolewa ukiwa una mfadhaiko wa akili (stress) na wakati unafanya kazi yoyote inayohitaji nguvu.

Endorphin pia hukusaidia wakati unaporudi kwenye hali yako ya kawaida ya utulivu baada ya misukosuko ya maisha.

Wakati unapiga punyeto mwili wako huitoa homoni hii dopamine kemikali ambayo hukufanya ujisikie raha za kimapenzi na kisha mwili huitoa tena endorphin baada ya kuwa umemaliza tendo hilo.

Kadri unavyoendelea kuwa teja wa punyeto ndivyo na ubongo wako unavyozidi kuzalisha na kuzitoa hizi homoni kwenye mwili wako.

Endorphins na dopamine ni homoni zinazohusika na kupunguza au kushusha kiwango cha stress kwenye akili yako.

Kwahiyo wale wote wanaosumbuliwa sana na stress au wenye matatizo yoyote ya kuvurugika kwa akili wanakabiliwa zaidi na hamu ya kutaka kupiga punyeto kuliko watu wengine wenye utulivu wa akili zao.

Hivyo punyeto kwa sehemu kubwa ni matokeo ya kutokuwa na namna nzuri za kushughurika na mihemko yako katika maisha.

Punyeto inakufanya wewe ulikimbie tatizo kwa muda mfupi badala ya kushughulika na tatizo uso kwa uso.

Wakati punyeto ya mara 1 au 2 kwa mwezi inaweza isilete shida yoyote kwenye afya yako, ukizidisha ina madhara makubwa kiafya kuliko hata sigara. Wapo baadhi hufanya punyeto karibu kila siku.

Shida hii miaka ya sasa ni kubwa sana kwa vijana wa miaka 15 mpaka 25 na wengi wao wanakuwa bado wapo shule na vyuoni na wengi hawajuwi k**a baadaye inaweza kuwaletea madhara.

Wazazi wanawanunulia watoto wao simu janja (smartphone) ili waweze kupata masomo kirahisi mtandaoni na mawasiliano kati yao na wazazi lakini vijana hao kwa ujinga wao wanajaza picha na video za ngono na huzitazama kila mara na k**a matokeo yake hujikuta watumwa wa punyeto na mwisho wa yote ni kufeli masomo yao.

Wakati mwili unatoa hizi homoni mbili mwili wako unajisikia kuwa na hisia au stimu sawa sawa na za yule aliyetumia dawa ya kulevya ijulikanayo k**a ‘heroin’.

Kuacha punyeto siyo jambo rahisi k**a mtu anavyoweza kukuaminisha.

Hili ni swali ninalokutana nalo karibu kila siku niwasilianapo na watu hasa wanaume.

Ni ngumu kuacha punyeto kuliko hata sigara.

Hata hivyo penye nia pana njia na hakuna lisilowezekana k**a umeamua.

Inaweza kuchukua muda lakini ukiwa na malengo na afya yako mwishowe utafanikiwa kuacha.

K**a ilivyo kwa tabia zingine zozote mbaya, kuacha punyeto kunahitaji mikakati na kuepuka chochote kinachoweza kukupelekea kuwaza kujichua.

Kitu pekee kinachoharibu afya, nguvu na ubunifu kwa mwanaume ni punyeto.

Siwezi kukueleza kwa namna inayoeleweka madhara ya punyeto hata ukaamini.

Ni somo zito na wengi wanalichukulia juu juu tu.

K**a wewe ni mwanaume na unataka kuepukana na ujinga, unataka kuepukana na hali ya kukosa hamasa ya kuwa mbunifu au kufanya kazi kwa bidii basi acha punyeto.

Kuna uwezekano kuna baadhi ya watu pengine hata wataalamu kabisa wamewahi kukuambia kuwa punyeto ni ngono salama na ni jambo la kawaida na ukaamini.

Ukweli ni kuwa punyeto ni mbaya kiwango ambacho siwezi kukueleza ukaamini.

Nguvu ya mwanaume ipo kwenye mbegu zake (semen).

Kila mara mbegu zake zinapotoka nguvu zake hupungua pia.

Sasa unapofanya punyeto maana yake unapoteza nguvu bila sababu na bila uumbaji wowote kutokea tofauti na vile ungeshiriki na mwanamke.

Mara tu unapoacha kujichua utaona nguvu zako za mwili na ubongo zinaongezeka kiwango ambacho hukuwahi kufikiri.

K**a unajiona ni mnyonge, huna nguvu, mjinga au unajiona ni mpumbavu hivi mara nyingi ujuwe ni matokeo ya kuzoea kujichua.

Mwanaume aliyezoea kujichua hata kutongoza kwake huwa ni shida sana kwani amejawa na aibu zisizoelezeka na wengi wao hupenda mambo ya bahati nasibu na ya mikato mikato (shortcut).

Punyeto ikikuzoea unakuwa huna tofauti sana na teja wa madawa yoyote ya kulevya.

Hata k**a huvuti sigara, huvuti bangi, hutumii dawa za kulevya au hunywi pombe kupitiliza lakini ukiwa tu ni mtumwa wa punyeto mwili wako na ubongo hauna tofauti na hao wanaoutumia hivyo vilevi kila siku.

Kila wakati unapopiga punyeto unajiuwa mwenyewe pole pole kimya kimya bila hata kujuwa.

Siri ya mafanikio k**a mwanaume au k**a wewe ni mwanaume na unataka kuwa mtu mwenye mafanikio kwenye maisha yako, nakuonya leo kwa upole, acha kujichua na hutakaa unisahau maishani mwako.

Kuna mambo mengi yataanza kutokea kwenye ubongo wako na kwenye mwili wako mara tu unapoanza kuacha tabia hii ya kujichua.

Uwezo wako wa kujiamini na kujitambua utaongezeka kwa haraka sana na wala hutaamini k**a kumbe ni punyeto tu ndiyo ilikuwa inachelewesha maisha yako namna hiyo hata ukawa unajiona hufai, siyo mzuri, ukawa hujiamini hata kuzungumza mbele ya watu.

Jinsi ya kuacha kujichua

1. Tafuta Daktari na uongee naye juu ya tatizo lako

Wakati unapokuwa tayari kuacha tabia yako mbaya ya kujichua hatua ya kwanza ni kumtafuta daktari na ikiwezekana uonane naye uso kwa uso siyo kwenye simu kwa msaada na maelekezo zaidi.

Usitafute msaada mtandaoni kwani unaweza kukutana na habari za kukukatisha tama au kukuhamasisha kuendelea kushiriki zaidi punyeto.

Daktari au Tabibu amefundishwa namna ya kushughulika na matatizo ya kitabia ya kiakili na namna ya kukupa mbinu nzuri za kuachana na tatizo hilo kutokana na umri wako na mazingira unayoishi.

Siyo gharama sana wapo matabibu unaweza kuonana nao bure na wengine hawachaji pesa nyingi k**a unavyoweza kudhani.

2. KUWA BIZE

Akili isiyojishughulisha na lolote ni makao makuu ya shetani na kila aina ya ujinga.

Kuwa bize na kazi, mazoezi, masomo kutakusaidia kupunguza hamu yako ya kutaka kujichua kirahisi zaidi kuliko ukiwa ni mtu wa kula na kulala.

Tembelea ndugu jamaa na marafiki kila mara unapokuwa huna kazi yoyote ya kufanya. Tafuta kitu kingine tofauti na punyeto unachopenda kukifanya mara kwa mara na uwe bize na hicho.

Ukiwa bize na kazi au mazoezi ya viungo au hata masomo kutakusaidia kuichosha akili yako na mwili kwa ujumla na hivyo hutapata tena nguvu za kutaka kujichua.

Kuna namna nyingi za kukufanya uwe bize. Nenda hata shambani kulima k**a huna shughuli yoyote maalumu ya kufanya.

Kuwa bize, endelea kufanya kazi, endelea na mazoezi ya viungo kila siku.

3. KUWA NA MKE AU MCHUMBA

Namna pekee nay a uhakika ya kuacha punyeto ni kuoa au kuwa na mchumba. Hii ndiyo njia pekee yenye uhakika wa asilimia 100 ya kuacha punyeto.

Tofauti na hii ni kuomba tu neema ya Mungu.

Mungu siyo mjinga hata akatuumba watu wa jinsia mbili tofauti. Ingawa bado nimekutana mara kadhaa na wanaume ambao tayari wameoa lakini bado wanajihusisha na kupiga punyeto.

Ukimuuliza inakuwaje unapiga punyeto na una mke majibu ni kuwa ameshazoea mchezo huo anashindwa kuacha!

Kwa wenzetu wazungu kuanzia shule ya msingi kijana wa kiume hata binti wa k**e anaweza kuwa na mchumba na akampeleka mpaka nyumbani kwa wazazi na isilete shida yoyote.

Shida ni huku kwetu Afrika ambako kijana huruhusiwi kuwa na mchumba wala mpenzi mpaka umalize shule au chuo na siyo kumaliza tu shule labda mpaka upate kazi inayoeleweka ndiyo unaweza kuwa na mchumba na ukampeleka mpaka kwa wazazi na wasipige sana kelele.

Kwahiyo kwa vijana waliopo shule ya msingi, sekondari na hata vyuo wengi wao sababu ya maadili yetu ya kiafrika wanajikuta hawana namna zaidi ya kupiga punyeto.

Hivi karibuni tulisikia huko Kenya wabunge walitaka kupitishwa mswaada wa sheria kuruhusu vijana waweze kuanza kushiriki tendo la ndoa wakiwa na miaka 16 na siyo mpaka 18, sijajuwa wameishia wapi k**a wamefanikiwa au la

K**a husomi shule au chuo na umeshakuwa mkubwa namna pekee ya kuacha punyeto ni kuoa au kuwa na mchumba karibu.

Kwa mwanaume tendo la ndoa ni moja ya mahitaji yake ya lazima k**a ilivyo kwa chakula au malazi ingawa hili wengi hawajuwi na wanaweza kupinga ila ukweli unabaki pale pale mwanaume ili awe na akili yenye utulivu na iliyotulia lazima awe anashiriki tendo la ndoa na siyo kupiga punyeto.

Ni kweli mapenzi yana madhara yake hasa k**a unasoma na upo bize masaa yote na mapenzi.

Mapenzi pia yanahitaji muda, nguvu na hela, k**a bado hali yako kiuchumi haieleweki au huna muda wa kumhudumia mwenza wako basi tumia mbinu zingine za kuacha punyeto kwa sasa mpaka utakapokuwa tayari kwa mahusiano.

Wanaoathirika zaidi na punyeto kati ya wanawake na wanaume ni wanaume.

Hivyo wanaume tuache kuwadharau wanawake na tutambuwe bila wao sisi hatujakamilika.

4. ACHA KUTAZAMA PICHA ZA X

K**a kuna kitu kimehamasisha tabia hii ya kujichua kwa kasi sana miaka ya sasa basi kitu hicho si kingine zaidi ya picha za X.

Yaani picha hizo na punyeto ni kulwa na doto, huwezi kuvitenganisha.

Ni ngumu sana sawa sawa na haiwezekani kwamba uangalie picha za x halafu usiishie kwenda kujichua k**a huna mke wala mchumba.

Hizi nazo zina uteja wake (addiction) k**a ilivyo kwa punyeto yenyewe. Ukishazoea kuziangalia nazo kuziacha inahitaji neema ya Mungu.

Ni k**a madawa ya kulevya hivi.

Sasa k**a unataka kuacha kujichua au kupiga punyeto, hakikisha unasahau kuziangalia hizi picha kuanzia sasa.

Popote ulipozihifadhi iwe kwenye simu au kwenye computer hatua ya kwanza zifute kabisa kote zisionekane.

K**a huwa un**iangalia kwenye mtandao futa anuani ya blog au tovuti ambazo huwa un**itembelea kuangalia uchafu huo futa na historia yake kwenye browser yako ya simu au computer.

K**a upo kwenye magroup labda huko facebook au WhatsApp na kuna wenzako wanaweka picha za namna hiyo jitowe kwenye hayo magroup haraka dakika hii hii.

Ukiweza kukaa mbali na hizi picha una uwezekano wa kuacha punyeto kwa zaidi ya asilimia 98.

Tofauti na hapo sahau wewe kuacha punyeto na utaendelea kuwa mtumwa wa wa punyeto mpaka utakapokufa.

Na hizi picha za X ni mpango mkakati wa kishetani wa kukizubaisha na kukiangamiza hiki kizazi cha sasa pasipo wao kujitambua.

Picha hizi zinaharibu afya yako ya ubongo, zinasababisha wewe kuwa teja wa punyeto, zinakuletea tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa, zinaharibu utu wako wa ndani na uhusiano wako na Mungu.

Baada ya njia ya kuacha punyeto ya kuwa na mke au mchumba, njia nyingine ya uhakika ya kukuwezesha wewe kuacha punyeto ni hii ya kuacha kutazama picha za X.

Huo muda unaotazama hizo picha au hizo video kwanini usiingie youtube au google ukatafuta notisi za masomo ya ujasiriamali au ubunifu wowote na ukaboresha afya yako ya akili badala ya kuharibu akili yako kwa kutazama ujinga huo wa picha za X?.

Kingine ni kuondoa chumbani kwako vifaa vyote vinavyotumika wakati wa kujichua au kupiga punyeto.

Hivi vinajulikana k**a ‘sex toys’, ni k**a mamidoli ambayo watu waume kwa wake wamekuwa wakiitumia wakati wa kujichua.

Uamuzi unabaki kuwa kwako.

Ikiwa unatafuta dawa ya kutibu madhara yatokanayo na punyeto, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Hizi ni baadhi tu ya faida chache zitakazokutokea mwilini unapoanza kuacha punyeto:

1. Hofu zitakuisha – Wakati unapoacha uteja wa kujichua mara moja utaanza kuona uwezo wako wa kujiamini unaanza kuongezeka.

Itakuwa ngumu sana wewe kupatwa na wasiwasi au kutetemeka hata mbele ya vitu ulivyokuwa ukitishika kirahisi hapo kabla.

Kwenye hali za hatari utakuwa unaelewa matokeo ya hatari hizo lakini utakuwa na uwezo wa kushughurika nazo kwa umakini na uangalifu mkubwa mpaka un**ishinda tofauti na kabla ulipokuwa mtu wa kupaniki hata kwa vitu vidogo tu

Utaanza kuona wazi nini maana hasa ya kuwa mwanaume kwenye maisha yako.

2. Macho yataongezeka uwezo wa kuona – Uwezo wa macho kuona huongezeka mara dufu mara tu unapoacha tabia hii ya kujichua.

Na siyo uwezo wa macho tu kuona ndiyo unaoongezeka bali hata uwezo wake wa uvumulivu wa kufanya kazi masaa mengi utaongezeka.

Utaona unaweza kufanya kazi kwenye computer yako au simu yako masaa mengi bila kuhisi kuchoka haraka tofauti na mwanzo ulipokuwa teja wa punyeto.

Punyeto inasababisha upofu k**a ikizidi.

3. Utaanza kujisikia vizuri – Utaanza kujisikia vizuri, utaanza kujiona ni mwenye furaha. Utajiona unafaa sana pengine ukaanza hata kuwasahau na watu wengine karibu yako.

4. Uwezo wa kukukumbuka vitu utaongezeka – Utaona ni rahisi kwako kukumbuka vitu na pia utakumbuka kumbukizi za nyuma ambazo ulikuwa umezisahau siku nyingi.

Usijali sana kuhusu kukumbuka mambo ya zamani, utaanza pia kukumbuka ndoto zako ulizokuwa umejipangia maishani miaka mingi iliyopita.

Akili yako itakuwa ni nyepesi na yenye nguvu zaidi.

5. Kinga ya mwili wako itaongezeka – Mwili wako sasa utakuwa na akiba ya kutosha ya nguvu hivyo kuwa rahisi kuyashughulikia magonjwa.

Inawezekana mwanzoni wakati unaacha kujichua kukajitokeza magonjwa au maradhi mengine kwa sababu mwili unakuwa upo bize kujitibu wenyewe lakini pole pole mwili wote utakaa sawa hivyo usivunjike moyo mapema.

6. Woga wako utaisha – Kiasi chako cha kuwa muoga kitapungua kwa asilimia kubwa sana mara uachapo kujichua.

Utaanza kujisikia vibaya kuwa mtu muoga au mwenye wasiwasi kwani utakuwa unajiona unakaribia kuwa ni mtu mkamilifu.

Hii itakupa hali ya kuona una ulinzi wa kutosha na hivyo kuweza kushughulika na hali ngumu bila kuwa na wasiwasi wowote.

7. Uelewa kuhusu vitu na watu utaongezeka – Uwezo wako wa akili utaongezeka mara dufu.

K**a ni mwanafunzi hata uwezo wako darasani unaweza kuanza kuwashangaza walimu, wazazi hata rafiki zako.

Utaanza kuvielewa vitu bila kutumia nguvu nyingi na majibu yatakuwa yanakuja kwako kirahisi zaidi kuliko wakati ule ulipokuwa teja wa punyeto.

8. Mwili utakuwa mnyumbufu – Yaani mwili wako utakuwa mwepesi, utaweza kufanya kazi au hata mazoezi muda mrefu bila kuhisi kuchoka sana.

Ni k**a unavyowaona watoto na vijana wadogo miili yao ilivyo shapu sababu bado hawajaipoteza hiyo nguvu mhimu zaidi kwa mwili wa mwanaume, ndivyo mwili wako utakavyoanza kuwa.

Utaonekana ni kijana zaidi tofauti na umri wako.

9. Utulivu utakuongezeka – Utakuwa na amani na utulivu usioelezeka kirahisi rahisi.

Utakuwa na uwezo mkubwa wa asili wa kuvumilia mambo na changamoto mbalimbali maishani mwako.

10. Utajiamini zaidi – Utakuwa hodari zaidi, aibu zako zote zitakuisha. Utakuwa na uwezo wa kuongea na yoyote, utaweza kumtongoza hata yule mdada ulihisi haiwezekani hata kusalimiana naye tu siku za huko nyuma ulipokuwa teja wa punyeto.

Faida za kuacha punyeto ni nyingi na siwezi kuandika zote hapa maana muda nao ni mali. Bali faida zingine kwa uchache ni pamoja na zifuatazo;

*Utakuwa na nidhamu
*Utaacha kuwa mtu wa kupaniki
*Unaweza kuacha uteja au ulevi mwingine wowote kirahisi
*Ngozi yako itakuwa nzuri na ya kupendeza
*Afya yako ya uzazi itarudi
*Utakuwa msafi
*Utakuwa unapangilia mambo yako
*Uwezo wako na nia zako vitaongezeka
*Msongo wa mawazo (stress) utaisha
*Utakuwa na mwili unaovutia
*Utakuwa huru, mwenye afya na mwenye furaha utadhani ni mtoto
*Uwezo wako wa kufanya kazi na kutengeneza pesa utaongezeka
*Hutakuwa mtu aliyetawaliwa na mihemko
*Utakuwa ni mtu wa kuaminiwa na wengine
*Utajiheshimu
Bado utaendelea kupiga punyeto au utaamua kuacha sasa na kuwa na afya bora na mpya ya mwili na akili kuanzia leo au utaendelea kuwa teja wa kujichua?

Uamuzi unabaki kuwa kwako.

Ikiwa unatafuta dawa ya kutibu madhara yatokanayo na punyeto, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Naitwa Fadhili Paulo ni Tabibu wa tiba asili, nauza dawa za Asili, nipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.

SHARE post hii na wengine uwapendao

DAWA YA KUTOA SUMU MWILINI SUMU ni kitu chochote ambacho kinaweza kuingia mwilini na kusababisha mifumo ya mwili ishindw...
27/11/2025

DAWA YA KUTOA SUMU MWILINI

SUMU ni kitu chochote ambacho kinaweza kuingia mwilini na kusababisha mifumo ya mwili ishindwe kufanya kazi ipasavyo.

Unafikiria kuwa una afya njema, lakini haujisikii vyema. Unapuuza, unaona ni vitu vidogo vidogo.

Hivyo, haushughuliki kwenda hospitali au kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Hatimaye tatizo linakuwa kubwa. Unafika hospitali unaambiwa una saratani, unapata mshtuko mkubwa! Unaambiwa chanzo cha ugonjwa hakifahamiki, ila unaelezwa chakula na mtindo wa maisha kwa ujumla ni sababu kubwa.

Hii ina maana kuna uwezekano umeingiza sumu nyingi mwilini. Kinga ni bora kuliko tiba. K**a ungeelewa mapema, ungejikinga na saratani.

Sizungumzii sumu za kung’atwa na nyoka, wala sizungumzii sumu zinazohitaji matibabu ya dharura.

Nazungumzia sumu ambazo zinatuua pole pole na kimya kimya bila ya sisi kujua wala kutambua chochote. Nazungumzia sumu ambazo kila kuchapo tuko kwenye mlango wa daktari.

Kila kuchapo afya zetu hizidi kuzorota zaidi. Hizi ni sumu ambazo ziko kwenye vyakula vyetu.

Ni sumu tunazozivuta katika hewa kila siku kutokana na mioshi ya magari, viwanda n.k.

Sumu ambazo zinaweza kutokana na madawa mbalimbali tunayojitibia afya zetu, sumu zinazotokana na vipodozi mbalimbali tunavyotumia kila siku kwa ajili ya urembo na kupendeza.

Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tuvute hewa, hata kwa sekunde kadhaa tusipopata hewa ya oksijeni tunakufa.

Lakini tunavuta hewa iliyochafuliwa na mioshi ya viwanda na magari ambayo imetamalaki kila kona.

Hivyo lazima tufe polepole na kimya kimya!

Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tule na tunywe. Lakini kwa bahati mbaya, vyakula vingi tunavyokula siyo salama, vimesheheni kemikali.

Tunapata sumu kwa sababu lazima tujipodoe, lazima tujipambe tupambike, na lazima tung’are tupendeze.

Kwa bahati mbaya sana, vipodozi vingi vimekuwa siyo vipodozi, ni vipopozi. Vimejaa kemikali ambazo huleta madhara mengi ya kiafya.

Tunapongeza mamlaka ya chakula na dawa, TFDA, kwa kuviteketeza baadhi ya vipodozi na kutoa orodha ya vipodozi visivyofaa, lakini hata hivyo juhudi kubwa lazima ifanyike.

Ishara zitakazokuonyesha mwili wako una sumu nyingi:

1. Uchovu sugu
2. Maumivu ya maungio
3. Msongamano puani
4. Kuumwa kichwa kila mara
5. Tumbo kujaa gesi
6. Kufunga choo au kupata choo kigumu
7. Kukosa utulivu
8. Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi
9. Pumzi mbaya
10. Mzunguko wa hedhi usio sawa
11. Kuishiwa nguvu
12. Kushindwa kupungua uzito
13. Kupenda kula kula kila mara
14. Kupatwa na ganzi sehemu mbalimbali mwilini

Kinachosababisha mwili kuwa na sumu au taka taka

Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku.

Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali.

Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako.

1. Kutokula matunda na mboga za majani

Matunda na mboga za majani ni vitu viwili mhimu sana ili kusafisha mwili wako na kukukinga dhidi ya sumu na taka taka mbalimbali.

K**a huna tabia ya kula matunda na mboga za majani kila siku ni wazi mwili wako utatengeneza sumu za kutosha.

2. Kula vyakula vya viwandani

K**a unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia katika mwili wako basi pendelea zaidi kula vyakula vya asili vinavyopikwa nyumbani kuliko kula vya kwenye makopo au vya dukani au vya kwenye migahawa (fast foods).

3. Kutokunywa maji mengi kila siku

Sababu kubwa ya watu wengi kutengeneza sumu au taka mwilini mwao ni kutokunywa maji mengi kila siku. Maji ni uhai, bila kunywa maji mengi kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.

Haijalishi upo mazingira gani k**a ni ya baridi au ni ya joto ni LAZIMA UNYWE MAJI YA KUTOSHA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU.

Unahitaji maji glasi 8 mpaka 10 kila siku. Watu wengi wanahangaika namna ya kuondoa sumu kusafisha miili yao bila kujua kuwa maji pekee ya kunywa yanatosha kwa kazi hiyo.

Kumbuka asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 za ubongo wako ni maji, hivyo k**a huna mazoea ya kupenda kunywa maji kila siku ni rahisi mwili wako kutengeneza sumu. .

4. Vinywaji vyenye kaffeina

K**a tayari imethibitika una sumu au takataka nyingi mwilini nakushauri uache kunywa chai ya rangi na kahawa.

Badala yake hamia kutumia chai yenye tangawizi au mdalasini au mchaichai.

Chai ya rangi na kahawa vina kaffeina ambayo kwanza huyasukuma maji nje ya mwili kwa haraka na kuuacha mwili bila kuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya kazi zake.

Kaffeina pia ni madawa ya kulevya kundi la madawa yanayosisimua mwili (stimulants drugs).

5. Kutopata usingizi wa kutosha kila siku

Moja ya vitu vinaweza kukupelekea kuwa na sumu mwilini au takataka nyingi ni pamoja na kutokulala muda wa kutosha kila siku. Usingizi haukopwi na huwezi kuwa na ufanisi katika kazi zako k**a hupati usingizi wa kutosha kila siku.

Usingizi siyo jambo la starehe tu, ni sehemu mhimu sana katika afya yako ya kila siku.

Bila kupata usingizi wa kutosha unaweza kuwa karibu na matatizo k**a kuongezeka uzito, kushuka kwa kinga ya mwili na nguvu zako za mwili kwa ujumla zinaweza kushuka.

Unapopata muda wa kutosha wa kulala masaa 7 mpaka 8 kwa siku unaupa mwili wako nafasi ya kutosha ya kupumzika na kujiripea upya na hivyo ndivyo sumu na takataka nyingine zinavyoweza kukutoka kirahisi.

Ingia kulala mapema walau saa tatu usiku ingia kulala siyo unakaa unaangalia tamthiliya au mpira mpaka saa sita za usiku!

6. Mazingira tunayoishi

Kuna mazingira yanajulikana wazi kuwa ni vyanzo vya sumu mwilini. Maeneo ya migodi ya madini, maeneo yenye viwanda vingi, maduka yanayouza dawa za kilimo nk

Maeneo haya yanafaa kukaa mbali na makazi ya binadamu kwa usalama wa afya zetu.

7. Vyakula vilivyokobolewa

Ili kuwa na mwili msafi kabisa epuka kula mkate mweupe, sukari na vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi k**a vile chipsi, maandazi na vingine vyote vinavyochomwa katikati ya mafuta mengi.

Mkate upo mkate mweusi (brown bread), sukari ipo asali mbichi, vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi unaweza kuamua kuwa unavioka (bake) au uvichemshe (boiling). Uchaguzi ni wako.

8. Mfadhaiko (stress)

Kile tayari unajuwa ni kuwa mfadhaiko au stress ni jambo baya kwa afya yako. Kile unatakiwa kujua kuanzia sasa ni kuwa ili kubaki na afya bora kabisa yenye TBS basi ukae mbali na stress.

K**a utaruhusu stress kutawala maisha yako basi ujuwe mwili wako hauwezi kufanya kazi zake vizuri ikiwemo ya kuondoa taka au sumu mbalimbali mwilini.

Stress peke yake inaweza kupelekea magonjwa mbalimbali mwilini zaidi ya 50. Unapokuwa na mfadhaiko mwili wako hauwezi kutoa taka nje kirahisi na kinga yako ya mwili inashuka matokeo yake unakuwa karibu na magonjwa mengine mengi.

Watu wengine wenye uelewa mdogo wakiwa na stress hukimbilia kutumia vilevi wakidhani zitapungua kumbe ndiyo wan**idi kuongeza tatizo bila kujua.

9. Dawa za kizungu

Dawa nyingi za hospitali huwa zina matokeo chanya (positive) na matokeo hasi (negative) pia ambayo ndiyo matokeo mabaya.

K**a unalazimika kutumia antibiotic kila mara au unameza dawa za kuondoa maumivu kila mara unaweza kuwa unaongeza sumu na taka mwilini bila kujua na bila sababu yoyote ya lazima.

Kuepuka hilo jaribu kutumia mitishamba au mimea ya asili kwa baadhi ya magonjwa ambayo si lazima uende hospitali. Siyo mafua tu mtu ameenda kuchoma sindano!

10. Vilevi

Moja ya vitu vinavyoweza kuleta sumu au taka mwilini moja kwa moja ni vilevi. Vilevi k**a pombe, madawa ya kulevya, sigara, bangi na vinginevyo ni vitu vinavyopelekea mwili kuwa na taka moja kwa moja.

Namna pekee ya kuondoa sumu kutokana na vilevi ni kuviacha hivyo vilevi, ndiyo kuviacha.

Usitegemee asubuhi utumie dawa kuondoa sumu mwilini halafu jioni ukanywe pombe au ukavute sigara utegemee tu ile dawa uliyotumia asubuhi kwamba itafanya kazi, hapana unajidanganya, dawa ni kuacha vilevi moja kwa moja.

Vingine vya kuacha k**a tayari imegundulika una sumu nyingi mwilini ni pamoja na vinywaji baridi vyote, juisi zote za dukani, chai ya rangi na kahawa.

DAWA YA KUTOA SUMU MWILINI > UNGA WA MAJANI YA MLONGE

Unga wa majani ya mlonge ndiyo dawa pekee ya asili ya uhakika ya kuondoa sumu mwilini.

Mti wa mlonge umekuwa ukijulikana k**a mti wa miujuza (miracle tree) kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu maradhi mengi mbalimbali mwilini kuanzia kwenye kufunga choo mpaka kwenye saratani.

Kwa sababu hiyo Mlonge unakuja kuwa msaada mkubwa kwenye ogani yetu kubwa kuliko zote katika kazi za kusafisha mwilini ambayo ni INI.

Kwa kawaida Ini letu ndiyo ogani inayohusika na utoaji sumu na taka mbalimbali mwilini.

Ini huchuja kila kinachouingia mwili ili kuchambua na kuondoa vitu visivyohitajika na mwili yaani sumu na taka mbalimbali.

Ini lipo kwenye mawasiliano wakati wote na ogani zingine za mwili hasa zile zinazohusika na umeng’enyaji wa chakula.

Ini zuri lenye afya husaidia kuweka sawa mzunguko na mgawanyo wa damu mwilini.

Ini huihifadhi damu ili kwamba liweze kuupa mwili damu mpya na safi yenye afya wakati mwili unapokuwa umepatwa na majeraha na kuripea au kuziondoa seli za damu zilizodhurika ambazo zinapita kupitia Ini.

Ini ndiyo linahusika na kuganda kwa damu kazi ambayo ni mhimu sana inayosaidia miili yetu kujitibu tunapopatwa na majeraha.

Ini husaidia pia kuondoa damu sukari iliyozidi katika damu na kufanya kazi kwa karibu na kongosho kwa kudhibiti matendo na kazi za insulin.

Ini huzalisha nyongo ambayo kisha huhifadhiwa katika kibofu nyongo (gall bladder). Nyongo husaidia mmeng’enyo wa chakula na uondoaji wa sumu au taka mwilini.

Mlonge unalisaidia ini katika kazi zake

Yote katika yote Ini ni ogani mhimu sana kwa kazi za mwili kwa ujumla. Jambo lolote linaloathiri utendaji kazi wa Ini linaweza kusababisha shida nyingi mwilini ikiwemo matatizo kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, homoni, kudumaa kwa ubongo na hata kudhuru afya yako ya akili kwa pamoja.

Kwa bahati nzuri mlonge unaweza kulirudishia Ini afya yake na hivyo kuliwezesha kufany akazi kwa kiwango chake cha juu kabisa katika kuondoa sumu na taka mbalimbali mwilini kwa njia 3 zifuatazo:

1. Mlonge unapunguza uharibifu uliojitokeza katika ini

Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa mlonge unasaidia kutibu na kuzuia madhara katika Ini.

Tafiti kadhaa zimeonyesha mlonge kuwa na uwezo wa kupunguza madhara ambayo tayari yamejitokeza katika Ini.

Mlonge unao uwezo wa kuzuia Ini dhidi ya ugonjwa wa Ini (hepatitis) na tafiti zinahitimisha kwa pamoja kuwa unga wa majani ya mlonge husaidia pia kuzuia uharibifu katika Ini.

2. Mlonge Unavirudisha Vimeng’enya vya ini

Mlonge unasaidia kuvirudisha vimeng’enya (enzymes) kwenye Ini lililodhurika.

Ini ni ogani katika mwili inayohusika na kusafisha damu, uzalishaji wa nyongo, kumeng’enya mafuta na umeng’enywaji wa jumla wa viinilishe katika vyakula tunavyokula.

Kazi hizo zote za Ini zinawezekana kwa msaada wa vimeng’enya vyake. Inapotokea Ini lina uchovu au limezidiwa na wingi wa kazi vimeng’enya vyake vyaweza kupungua na hivyo kulifanya Ini kutokuwa na msaada wowote katika kazi ya kutoa sumu na taka mwilini.

Mlonge unasaidia kuvirudisha vimeng’enya (enzymes) vyote kwenye Ini katika hali yake ya kawaida na kufanya kazi k**a vinavyopaswa kuwa vinafanya katika ini zuri lenye afya.

3. Mlonge unasaidia kuondoa msongo wa mawazo (stress)

Nimeandika pale juu kwamba moja ya vitu vinavyosababisha sumu au taka taka mwilini ni msongo wa mawazo yaani stress.

Tafiti nyingi zimekuwa zikionyesha kuwa moja ya kisababishi kikubwa cha msongo wa mawazo (stress) ni kukosekana kwa viinilishe mhimu katika chakula.

Kukosekana huku kwa viinilishe mhimu katika chakula kunasababisha usawa usio sawa wa homoni mwilini (hormonal imbalance) jambo linalopelekea kutokea kwa msongo wa mawazo.

Msongo wa mawazo umeendelea kuwa tatizo kubwa kwa watu miaka ya sasa na wengi wao wakipatwa na tatizo la kukosa pia usingizi.

Hata hivyo, tatizo hilo linaweza kutibika kirahisi kwa kuongeza viinilishe sahihi kwenye mwili wako

Kwa bahati nzuri unga wa majani ya mlonge una viinilishe vingi kuliko mmea au mtishamba wowote chini ya jua ukiwa na viinilishe 92 ndani yake!

Unga wa majani ya mlonge una kiasi cha kutosha cha vitamini A, B, C, E, Potasiamu, Kalsiamu na viinilishe vingine vingi.

Kwahiyo k**a utaweka mazoea ya kutumia mlonge kila siku itakuwa ni vigumu kwako kupata tatizo la msongo wa mawazo huku ukipata faida nyingine nyingi za mti huu wa ajabu

Kiasi kingi cha madini ya magnesiamu kwenye mlonge ni mhimu kutibu matatizo ya mifupa kwa wamama wanaofika ukomo wa siku zao (miaka 40 hivi kwenda juu).

Magnesiamu madini yapatikanayo kwenye mlonge ni dawa maarufu ya kutuliza akili (Tranquillizer) na kutibu matatizo k**a msongo wa mawazo, sononeko, huzuni, hamaki na matatizo mengine ya mvurugiko wa akili.

Hii ni orodha ya viondoa sumu (antioxidants) 46 na zaidi vipatikanavyo katika mlonge:

Antioxidants (9, 11, 12, 13, 14, 15)

1. β-carotene
2. calcium
3. potassium
4. quercetin
5. chlorogenic acid
6. hydroxyanisole (BHA)
7. butylated hydroxytoluene (BHT)
8. tertiary-butylhydroquinones
9. propyl gallate
10. vitamin E (tocopherols)
11. ascorbic acid (vitamin C)
12. glucose oxidase
13. reduced glutathione
14. citric acid
15. polyphospages
16. aminopolycarboxylic acids
17. vanillin
18. moringine
19. strophantidin
20. 4-(α-l-rhamnosyloxy)
21. benzyl isothiocyanate
22. 4-(4’-O-acetyl-α-l-rhamnosyloxy)
23. benzyl isothioyanate
24. catechin
25. 4-(β-d-glucopyranosyl-1→4-α-l-rhamnopyranosyloxy)
26. benzyl thiocarboxamide
27. epicatechin
28. 4-O-(α-l-rhamnosyloxy)
29. benzyl glucosinolate
30. 4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)-benzylglucosinolate
31. Kaempferol
32. Niazimicin
33. 4-(α-l-rhamnosyloxy)
34. benzyl acetonitrile (niazirin)
35. O-ethyl-4-(α-l-rhamnosyloxy)
36. benzyl carmate
37. Gallic acid
38. Glycerol-1-1-(9-octadecanoate)
39. p-Coumaric acid
40. 3-O-(6’-O-oleoyl-β-d-glucopyranosyl)-β-sitosterol
41. Ferulic acid
42. β-sitosterol-3-O-β-d-glucopyranoside
43. Caffeic acid
44. 3-Hydroxy-4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)
45. benzyl glucosinolate
46. Protocatechuic acid
47. 4-(2/3/4′-O-acetyl-α-l-rhamnopyranosyloxy)
48. benzyl glucosinolate
49. cinnamic acid
50. glucosinalbin
51. ellagic acid
52. glucoraphanin
53. glucoiber

Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele.

Mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe. Mlonge UNA MADINI YA CHUMA MARA 25 ZAIDI YA ILE ILIYOMO KWENYE SPINACHI

Changanya matunda yote na mboga za majani zote bado viinilishe vyake kwa pamoja haviwezi kuvifikia vile vilivyomo kwenye mlonge!

Ni kusema mtu aliyekula matunda na mboga za majani zote bado hatakuwa na afya bora k**a yule atakayetumia mlonge tu.

Kwahiyo tunaweza kuhitimisha kuwa unga wa majani ya mlonge ni dawa nzuri na ya uhakika kwa kuondoa sumu mwilini na kulinda afya ya INI kwa ujumla.

*Usitumie dawa hii bila uangallizi wa karibu wa Tabibu.

K**a unahitaji maelezo zaidi ya jinsi gani ya kutumia pamoja na jinsi ya kuweza kuupata ambao umeandaliwa maalumu Kwa ajili ya matumizi ya dawa na lishe kwa familia, wasiliana na mimi kwa simu ya kawaida au WhatsApp 0714800175

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Address

Kibugumo Mji Mwema Kigamboni

Telephone

+255714800175

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tabibu Fadhili Paulo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram