14/09/2025
Niko njia panda, moyo wangu unauma sana kwasababu ya huyu mwanaume. Nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa muda sasa kwa kweli mwanzo alionyesha upendo usio na kifani kwangu pamoja na familia yangu
Nilikuwa na amani nikiwa na yeye, lakini furaha hiyo haikudumu. Mana anachokitaka ni kigumu sana kwenye maisha yangu. Ety anataka mimi na mdogo wangu, wote tuwe wapenzi wake na anasema anatupenda wote jamani hivii hii inawezekana kwelii๐ญ๐ญ
Mimi na mdogo angu ndio tuliobakia katika familia yetu, na tumetoka mbali sana. Tumepigana vita nyingi za maisha, na kwa sasa tunaweza kujivunia maisha mazuri kwa sababu ya bidii yetu.
Mpenzi wangu ni mfanyabiashara tajiri na maarufu, anamiliki maduka mengi, nyumba, na magari. Alikuwa hajawai kumwona mdogo wangu sababu alikuwa chuo ila mambo yalianza kubadilika baada ya yeye kumwona mdogo wangu kwa mara ya kwanza
Alianza kumsifia sana mdogo wangu, akasema ni mpole ana heshima na anaonekana kuwa na roho nzuri k**a nilivyo mimi na akaniomba nijitahidi kumfanya mdogo wangu awe karibu na yeye. Mhhhh! Nikaanza kupata mashaka
Sikufanya hilo kosa nilimuonya mdogo wangu asiwe na mazoea na shemeji yake na kwakuwa mdogo wangu alinipenda sana alinielewa, japo bado nina wasi wasi mkubwa
Siku moja, aliniambia kuwa ananipenda lakini pia anamtaka mdogo wangu. Alisema, "Nyinyi wote ni wazuri sana na wote mmenivutia. Nina uhakika mnaweza kufurahia maisha yangu, na nina uwezo wa kuwafanyia nyinyi wote mambo makubwa. Akasema anaamini kuwa yeye ndiye mwanaume pekee anayeweza kutupenda zaidi kuliko mtu yeyote, na ana uhakika anaweza kutimiza ndoto zenu."
Siku hiyo nilihisi dunia imegeuzwa juu chini, yaani nilihisi bado sijaamka ilikuwa ni ndoto ambayo utaisha lakini siku zinakatika tumwgombana hatuongei. Nilianza kujiuliza mambo mengi sana hivi huyu mwanaume kweli ananipenda au ananitumia tu
Nimeshamwambia mdogo wangu kinachoendelea japo nina wasiwasi mana sisi watoto wa k**e kudanganyika ni rahisi hasa ukizingatia mdogo wangu alinambia shemeji ake kamuahidi kumwajiri dukani kwake na atamlipa mshahara mzuri
Ninahofia mdogo wangu, anaweza kuangukia kwenye mtego huu. Najua nikimwambia mama, hatanielewa, kwa sababu mpenzi wangu amekuwa akiwapa pesa na zawadi kibao nyumbani. Kwa hiyo, mama anamwona wa thamani sana, ambaye najituma sana kwa ajili ya kuilea familia yetu. Najiona niko peke yangu katika hili, na ninaumia sana. Naomba ushauri wenu Nifanyeje?๐ญ๐ญ
FOLLOW #๐ ๐๐ฃ๐๐ก๐ญ๐ +255 KUJIFUNZA ZAIDI
https://whatsapp.com/channel/0029VaqfCfjK0IBcdfHhhh2I