30/10/2016
MENDE
Somo lililopita tuliona japo kwa uchache sana madhara yaletwayo na mdudu msumbufu Mende, nikukaribishe tena kwenye safu hili ya leo kuhusu hatua za maisha ya Mende na jinsi ya kumzuia au kumwondoa ndani kwako bila kutumia sumu kali wala kemikali.
B: HATUA ZA UKUAJI WA MENDE
K**a ilivyo kwa wadudu wengi Mende huanzia hatua ya yai, na hupita hatua tatu hadi kifikia hatua ya mwisho ya ukuaji mende mzima (adult). Hatua hizo ni Yai;
Ni Muhimu ifahamike kuwa kuna jamii nyingi sana za mende zaidi ya 4000 ambao huwa na tofauti ndogondogo za maendeleo ya UKUAJI NA TOFAUTI ZINGINE ila kati ya aina hizi kuna aina tatu wanaoishi majumbani mwa watu. Hapa naenda kuzungumzia zaidi wale mende ambao wamekuwa ni tatizo kubwa kwa Watanzania na kwingineko duniani majumbani.
1. Yai
Mayai ya mende yanakaa ndani ya mfuko wa mayai wa rangi ya kahawia unaobeba wastani ya mayai 35 ujulikanao kitaalamu k**a Ootheca (Fuko la mayai). Ukubwa wa ootheca moja inakaridiwa kuwa mm 7 urefu na mm 2 upana japo hutofautiana sana ukumbwa kati ya jamii moja ya mende na nyingine.
Kwa jamii nyingi za Mende, dume huyarutumbisha viyai ndani ya jike na huendelea kujitengeneza ndani ya ootheca. Jamii zingine za mende hubaki na mayai hayo na hukomaaa hadi kuanguliwa ndani ya mwili na vifaranga huwa k**a wanazaliwa; mfano k**a vile Madagascar hissing cockroach.
Jike hutaga mayai mfululizo anapofikia hatua ya mwisho ya ukuaji na kwa maisha yake yote ya watani wa siku 100 kutegemeana na jamii ya mende. Mende mmoja anauwezo wa kutaga mayai kwa makadirio k**a 4oo hivi. Kwa aina ya mende waliozoeleka na wanaopatikana kwa wingi nchini Tanzania hubeba mayai (ootheca) mwilini mwao hadi linapobakiza siku mbili au siku chache kuanguliwa kisha hulitagia sehemu salama na ngumu kufikika na binadamu. Mara nyingi mende jike mzima(adult) huonekana akiwa na fuko la mayai mwilini mwake kila aendapo.
2. Vifaranga (Nymph)
Vifaranga huanguliwa vikiwa vidogo sana, rangi nyeupe, vilaini na hawana mabawa ambao hukua huku wakibadili rangi hadi kufikia mende mzima. Vifaranga mara nyingi huanguliwa ndani ya siku 24 hadi 38 na idadi ya vifaranga vitakavyoanguliwa hutofautiana kutokana na aina (Spicies) ya mende.
Vifaranga hupitia hatua mbalimbali za kujibadili (molting) mpaka kufikia kuwa mende mzima. Vifaranga (Nymph) na mwisho mende mzima na mara zote vifaranga (Nymph) ni mara tatu ya mende wazima yaani Vifaranga (nymph) 75% na Wakubwa (adult) ni 25% ya mende wote waliopo kwenye makazi ya binadamu.
3. Mende Mzima (Adult)
Japo kuna jamii za mende ambazo hazina mabawa jamii nyingi wana mabawa, jamii hizi ambazo ni wasumbufu sana ndani ya makazi ya watu nchini mwetu Tanzania na Africa mashariki wana mabawa na huweza kuruka japo kwa umbali mfupi na hii huwa saidia sana kusambaa kutoka kwa jirani mmoja hadi kwa mwingine. Mende hujifisha mchana na usiku hula na kutembea.
Japokuwa mende ana uwezo wa kukaa bila kula kwa muda wa miezi mitatu hawezi kuishi bila kunywa maji, Mende huishi kwa kula mabaki ya vyakula, kunywa maji hula pia kwenye njia ya maji machafu na pia chooni na wanaweza kuziba masinki k**a wapo wengi sana kwenye nyumba.
Kwa asilimia kubwa mende husambaa kupitia wasafiri hukaa kwenye mabegi, redio na viafaa vingine vinavyosafirishwa na ukifika unako kwenda huhamia ndani ya nyumba.
Hotel nyingi zinapata mende kupitia wateja wao wanaokuja kulala huleta mende bila kujijua
C) JINSI YA KUWAONDOA NA KUWAZUIA WASIJE NYUMBANI BILA KUTUMIA WATAALAMU WALA
Kuna njia mbali mbali za kupambana na mende nyumbani kwako bila kutumia wataalamu wa kupulizia sumu au chemikali za kununua.
1. Majani ya Bei (Laurus nobilis); mende hawaupendi mmea huu na hivyo ukikatakata na kuweka sehemu sehemu za mende kucheza na kula mende huondoka
2. Sumu ya mende ya kujitengenezea;
Chukua kijiko kimoja cha chakula ya asidi ya boric changanya na vijiko viwili vya unga wa mahindi na kijiko kimoja cha kokoa changanganya vizuri na nyunyiza sehemu ambazo mende hupenda.
NB mchanganyiko huu ni sumu hivyo weka mbali na watoto
3. Mtego wa mende;
Vaselini uliotandazwa vyema kwenye kiboksi hunasa mende na hawataweza kutembea juu ya vaselini. Ni vizuri kuweka chakula cha kuwavutia Mende ili waje kwenye mtego.
4. Mchanganyiko wa sabuni na Maji;
Changanya sabuni ya maji na maji iwe nyepesi kiasi cha kuweza kupuliza kwa kutumia chupa ya kupulizia. Kwa kutumia chupa ya kupulizia ama bomba ya kuogeshea mifugo hakikisha unamdondokea mende, ikimdondokea tumboni ni vizuri zaidi. Matone madogo mawili yakimpata mende tumbuni hufa baada ya muda mfupi
5. Amira (Baking Powder) and sugar;
Changanya kwa uwiyano sawa sukari na amira (Baking Powder) kasha nyunyiza seheme mende wanapenda kukaa sukari itawavutia kula na Amira itawauwa kwa kuwa fanya wavimbiwe.
6. Sprei ya Nywele (Hair Spray);
Wapulizie mende sprei ya nywele watakufa mara moja
7. Wanyime maji na chakula;
Kumbuka mende wanahitaji maji kuliko wanavyohitaji chakula; hapa unashauriwa mabomba yote yafungwe vyema yasiwe yanavuja maji, maji yakimwagika hakikisha unayakausha kwa kudeki na kuacha nyumba yote kavu na sinki zote zifunikwe vyema usiku na mchana pia kwa kutumia kizibo cha sinki; jokofu pia zisivuje.
Jitahidi mabaki ya chakula yasibaki popote jikoni na chumba cha kulia chakula (dinning) pia, vyakula vinavyobakizwa vivunikwe vyema kwenye bakuli mbalimbali na kuwekwa kwenye jokofu au mahali pakuhifadhi chakula, vyombo vioshwe mara tu baada ya kula. Kumbuka kipunje kidogo cha chakula kinawashibisha mende wengi hivyo umakini kwenye hili unatakiwa.
8. Mchanganyiko wa Matango, pilipili na Limao
Koroga mchanganyiko huu kisha weka sehemu ambazo mende hupendelea kikaa/kuishi na mende watakimbia ndani kwako hawatakaa.
Safisha nyumba yako sana;
Anzia jikoni pawe pasafi sana bila mrundikano wa vitu na vyombo visivyosafishwa. Vyakula vilivyobaki vifunikwe vyema na kuwekwa kwenye jokofu.
9. Ficha chakula;
Chakula chochote ambacho mende hula kitunzwe vyema sehemu ambapo mende hafiki kwenye jokofu pia matumda huwapatia chakula na maji pia yatunzwe vyema
10. Safisha Sakafu;
Nasisitiza kuwa Mende anahitaji maji ili kuishi jitahidi kuhakikisha hawapati maji kwa kusafisha na kukausha sakafu; ondoa pia mabaki ya chakula, michirizi ya chakula na matone ya chakula kwenye sakafu na ukutani au popote pale.
11. Ondoa chombo/debe la taka kila siku
Hii itawanyima chakula mende ambao mara ngingi hujilisha ndani ya chombo cha taka pia nashauri chombo taka cha nje kisikae sana karibu na nyumbu ili kuepusha mende wasiende kujilisha huko usiku na kurudi ndani.
12. Maji ya Moto
Hii nimeshudia sehemu/jamii nyingi za nchi yetu, maji huchemshwa na yanabaki yakiendelea kuchemka na huchotwa kwa kutumia chombo na kuyarushia kwenye mikusanyiko wa mende vifaranga na wakubwa haraka kabla ya kupoa. Hii ikifanyiki kila siku mende huisha. Njia hii ni vizuri ikaendana na 9 hadi 12 kwa pamoja hizi zitamaliza tatizo lamende bila kutumia sumu ama kemikali ambazo huitaji mtaalamu ama garama kubwa.
D) KUZUIA MENDE WASIRUDI
i. Ziba Nyufa
Nyufa za kuta za nyumba pamoja na fenicha huwa makazi mazuri ya mende hivyo wanyime makazi hayo kwa kuziba nyufa za fenicha na kuta za nyumba
Ziba nafasi k**a vile zile zilizopo kati ya kabati ya kujengea na ukuta kwa kutumia simenti au gundi maalum ya mbao waweza kumshauri fundi afanye hivyo wakati wa kutengeneza kabati na k**a umepanga ama unaishi kwenye nyumba ya mwajiri basi jitahidi kuhahakiosha hili linafanyika.
ii. Wazuie mende wasiingine ndani
Weka nyavu kwenye madirisha na sehemu za kupitishia hewa kwenye nyumba pia milango iwekewe visuia wadudu kwa chini na zibaki zimefungwa wakati wa usiku. Tundu lolote lisilo (kioo, mbao, Ukuta nk) la lazima lizibwe.
iii. Epuka marundo ya mazao ya miti karibu na nyumba
Marundo ya mbao, kuni, mabanzi, nk huwa ni kivutio cha mende hivyo yakiwa karibu na nyumba hupelekea mende kuhamia ndani, hivyo nashauri zikae mbali na nyumba ya makazi.