18/10/2025
Story Yangu / My Story
Ndoto isiyowahi kufa
A dream that never faded
Mwaka 2013, nilikuwa na ndoto ya kuanzisha ukurasa ambao mama anaweza kujifunza, kuuliza maswali na kupata taarifa sahihi kuhusu ujauzito na malezi, kwa Kiswahili. Hapo ndipo Mamas & Totos ilipozaliwa.
Sikuwa na rasilimali nyingi, lakini nilikuwa na hamasa kubwa. Nilikuwa natumia muda wangu kutafsiri taarifa nzuri, kuziweka Facebook, na kujibu maswali ya kina mama waliokuwa wananitumia ujumbe kila siku. Wengine walidhani mimi ni daktari 😅 lakini ukweli ni kwamba nilikuwa najitahidi kusoma na kutafuta majibu sahihi, kwa upendo tu wa kusaidia.
Miaka ikaenda, maisha yakawa na harakati, na ukurasa ukaanza kimya... lakini ndoto haikufa.
Miaka ikaenda, nikawa na majukumu mengi na muda wa kupost ukawa mdogo, hivyo niliacha ukurasa kwa muda. Lakini moyoni nilijua hii ndoto haijafa ilikuwa imenipa mwito wa kusaidia kina mama, na nilijua siku moja nitarudi.
Leo, mwaka 2025, nimeamua kuirudisha Mamas & Totos nikiwa na maono mapya, uzoefu zaidi, na moyo ule ule wa awali.
Sasa si ukurasa tu wa ushauri, bali ni jamii ya kina mama mahali pa kujifunza, kusimuliwa hadithi, na kuhimizana kupitia safari halisi za ujauzito, uzazi, na malezi.
Imekuwa safari ndefu, lakini nimejifunza kuwa kila mama ana hadithi yake ya kipekee.
Ndiyo maana tunaanza Story Yangu / My Story, sehemu ya kushiriki uzoefu halisi wa ujauzito, uzazi, na maisha ya umama kwa ujumla.
Asante kwa wote mlioamini Mamas & Totos tangu mwanzon, na karibuni sana wote mnaojiunga nasi sasa.
Kwa sababu ndoto zingine haziishi, bali zinangoja muda sahihi wa kuchanua.
Je ungependa kushiriki hadithi yako pia?
Bonyeza link iliyopo kwenye bio yetu au andika Story Yangu kwenye comment, tutakutumia fomu ya kushiriki.