Weaset Epilepsy

  • Home
  • Weaset Epilepsy

Weaset Epilepsy Epilepsy often is an hidden disease in Tanzania,this rises stigma and discrimination! We want to fight it with educational contents! By ComSol NGO

Tusiwanyanyapae wenye kifafa! Kifafa si uchawi wala laana, ni hali ya kiafya inayohitaji uelewa na msaada wa jamii. Tuun...
29/11/2024

Tusiwanyanyapae wenye kifafa! Kifafa si uchawi wala laana, ni hali ya kiafya inayohitaji uelewa na msaada wa jamii. Tuungane kubadilisha fikra na kusaidia walio na kifafa kuishi maisha yenye furaha.

Kifafa ni hali ya kiafya inayosababishwa na shughuli zisizo za kawaida kwenye ubongo, na husababisha degedege (seizures)...
26/11/2024

Kifafa ni hali ya kiafya inayosababishwa na shughuli zisizo za kawaida kwenye ubongo, na husababisha degedege (seizures). Zaidi ya watu milioni 50 duniani wanaishi na kifafa, lakini bado kuna unyanyapaa mwingi kuhusu hali hii.

📌 Kifafa hakihusiani na uchawi au laana – ni tatizo la kiafya.
📌 Kifafa hakiambukizwi
📌 Tiba na msaada sahihi vinaweza kusaidia mtu kuishi maisha ya kawaida.

Picha za matukio mbalimbali kutoka kwenye Tamasha letu la leo. Tumeshuhudia mshikamano, burudani, na elimu kuhusu ugonjw...
23/11/2024

Picha za matukio mbalimbali kutoka kwenye Tamasha letu la leo. Tumeshuhudia mshikamano, burudani, na elimu kuhusu ugonjwa wa kifafa. Asante kwa wote mliojitokeza kushirikiana nasi katika kuleta mabadiliko ya kijamii kupitia uelewa sahihi wa afya.

22/11/2024

Leo timu yetu imeendelea kutoa elimu kwa wakazi wa Mbeya kupitia matangazo ya barabarani (PA) kuhusu Tamasha letu maalum la uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa kifafa.

Kesho, Jumamosi tarehe 23 Novemba 2024, ndio siku ya Tamasha letu maalum hapa Mbeya! Tunakukaribisha kujiunga nasi uwanja wa Ruanda Nzovwe (eneo la CCM) kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi 7:30 mchana.

Tamasha litakuwa na burudani za muziki, maigizo, na elimu muhimu kutoka kwa madaktari kuhusu ugonjwa wa kifafa – sababu zake, matibabu, na ukweli kwamba hakihusiani na ushirikina.

Usikose fursa hii ya kujifunza na kufurahia! Karibu tushirikiane kwa mabadiliko chanya.

Kifafa hakiambukizwi na kinatibika! Tufikie kwenye kliniki zetu kwa matibabu bora. Morogoro: Hospitali ya Rufaa ya Mt. F...
29/10/2024

Kifafa hakiambukizwi na kinatibika! Tufikie kwenye kliniki zetu kwa matibabu bora.
Morogoro: Hospitali ya Rufaa ya Mt. Francis Ifakara
☎️ 0784 402 899 (Dr. Winifrid Gingo)

Njombe: Hospitali ya Utengamao ya Inuka Wanging’ombe
☎️ 0759 750 497 (Reception)

Mbeya: Kituo cha Huduma za Afya cha Waroma, Iyunga
☎️ 0789 643 786, 0754 069 233 (Dr. Joshua Mwakyelu)

Leo ni Kumbukizi ya  Baba wetu wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,  Tunamuenzi kwa mchango wake mkubwa katika ku...
14/10/2024

Leo ni Kumbukizi ya Baba wetu wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Tunamuenzi kwa mchango wake mkubwa katika kujenga umoja na amani ya Tanzania. Heri ya Siku ya Nyerere kwa Watanzania wote 🇹🇿

Tunapenda kuwakaribisha kutembelea Kliniki yetu ya Kifafa iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Francis, Ifakar...
11/10/2024

Tunapenda kuwakaribisha kutembelea Kliniki yetu ya Kifafa iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Francis, Ifakara. Tunatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya kifafa.

Vipimo vinafanywa kwa kutumia mashine ya EEG, ambayo husaidia kuchunguza kwa kina afya ya ubongo na kuwezesha utambuzi sahihi wa aina ya kifafa.

Tunapenda kuwakaribisha kutembelea Kliniki yetu ya Kifafa iliyopo katika Hospitali ya utengamao ya Inuka Wanging’ombe, N...
08/10/2024

Tunapenda kuwakaribisha kutembelea Kliniki yetu ya Kifafa iliyopo katika Hospitali ya utengamao ya Inuka Wanging’ombe, Njombe. Tunatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya Kifafa.

Vipimo vinafanywa kwa kutumia EEG machine, ambayo husaidia kuchunguza afya ya ubongo kwa kina na kuwezesha utambuzi sahihi ya aina ya Kifafa.

Tunapenda kuwakaribisha kutembelea Kliniki yetu ya Kifafa iliyopo katika Kituo cha Afya cha Waroma, Iyunga, Mbeya. Tunat...
04/10/2024

Tunapenda kuwakaribisha kutembelea Kliniki yetu ya Kifafa iliyopo katika Kituo cha Afya cha Waroma, Iyunga, Mbeya. Tunatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya Kifafa.

Vipimo vinafanywa kwa kutumia EEG machine, ambayo husaidia kuchunguza afya ya ubongo kwa kina na kuwezesha utambuzi sahihi ya aina ya Kifafa.

Kifafa hakiambukizwi na kinatibika! Tufikie kwenye kliniki zetu kwa matibabu bora. Morogoro: Hospitali ya Rufaa ya Mt. F...
27/09/2024

Kifafa hakiambukizwi na kinatibika! Tufikie kwenye kliniki zetu kwa matibabu bora.
Morogoro: Hospitali ya Rufaa ya Mt. Francis Ifakara
☎️ 0784 402 899 (Dr. Winifrid Gingo)

Njombe: Hospitali ya Utengamao ya Inuka Wanging’ombe
☎️ 0759 750 497 (Reception)

Mbeya: Kituo cha Huduma za Afya cha Waroma, Iyunga
☎️ 0789 643 786, 0754 069 233 (Dr. Joshua Mwakyelu)

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Weaset Epilepsy posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram