19/01/2022
MAUMIVU YA NYAYO NA KISIGINO
Plantar Fasciitis ni hali ya kusikia maumivu kwenye unyayo wako. Plantar Fascia ni tissue nyembamba/ligament ambayo huunganisha sehemu ya mbele ya unyao na kisigino chako. Hufanya kazi sawa shock up za gari au pikipiki ili kuhimili mgandamizo wa uzito wa kiwiliwili/ mwili wako kwa ujumla na kuuwezesha mguu wako kutembea bila maumivu.
Maumivu ya visigino na unyayo ni tatizo miongoni mwa watu wengi. Nyayo zetu zinakutana na mikiki mingi katika shughuli zeu za kila siku hasa ukizingatia shughuli zetu za kujikimu zinatofautiana miongoni mwetu. Hii hupelekea kuchakaa na kuisha nguvu kwa ligaments za unyayo husasani sehemu ya kisigino. Mgandamizo mkubwa husababisha nyayo kupata joto na kupelekea maumivu ya kisigino na kukaza kwa seli za eneo hilo.
Dalili za Plantar fasciitis
Watu wengi hulalamika kuhusu maumivu ya unyayo hasa kwenye kisigino na mbele kidogo kuelekea katikati ya unyayo, hii hutokea kwa mguu mmoja au miguu yote.
Maumivu ya unyayo huanza kidogo kidogo na kushamiri kadri muda unavyozidi kwenda. Maumivu huweza kuwa ya kusambaa au kuchoma mithili ya mwiba kwenye kisigino. Maumivu hayo husambaa kutoka kwenye kisigino kuelekea mbele ya unyayo.
Mauumivu huwa makali zaidi wakati wa asubuhi pale unapotaka kupiga hatua ya kwanza kutokea kitandani, maumivu haya huwa sawa na kukanyaga mwiba wa moto katika kisigino chako.
Pia maumivu huja pindi mtu anapoketi au kulala kwa muda mrefu, pia maumivu huja saa ya kupanda ngazi maana kisigino huwa kigumu na kukaza.
Maumivu hupungua kadri unavyopiga hatua na kuendelea na shughuli zako. Mara nyingi watu wenye changamoto hizi za miguu hawapati maumivu wakati wakiwa wamezongwa kwenye shughuli zao bali maumivu huwapata wakikata kuanza upya au kuendelea na shughuli zao baada ya Mapumziko.
Nini Husababisha plantar fasciitis
Kwa kawaida watu waliokuwa kwenye hatari zaidi ya kupata maumivu ya seli za nyayo ni wanaume na wanawake wenye umri wa miaka 40 hadi 70 ambao miili yao inajishughulisha zaidi.
Maumivu huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume, wanawake wajawazito hukumbwa na changamoto hii hususan kipindi cha mwishoni cha ujauzito wao.
Watu wenye uzito mkubwa pia hukubwa na changamoto ya maumivu ya visigino na nyayo kwa ujumla, uzito uliokithiri husababisha misuli kushindwa kuhimili hivyo kusababisha athari hususan kwa watu walionenepa ghafla na kupata ongezeko kubwa la mwili ndani ya muda mfupi.
Pia ukiwa ni mkiambiaji wa mbio ndefu au mtu wa michezo kuna uwezekano mkubwa wa kupata changamoto hizi, na aina ya kazi unayoifanya yaweza pelekea kupata changamoto hii mfano ikiwa ni mtu wa kusimama muda mrefu au kuzunguka na kutembea k**a mhudumu wa mgahawa n.k.
Wenye Miguu iliyokosa uvungu, au kuwa na uvungu mkubwa kupiliza nao pia hupata changamoto hii ya maumivu ya visigino na nyayo.
Uvaaji wa viatu vyenye kuumiza kisigino au visivyo upa unyayo wako ahueni, visivyofata asili ya umbile la mguu wako au vilivyokuwa Flat kabisaa na vyenye soli au vikanyagio laini..
Japo awali madaktari walihusisha changamoto ya maumivu haya ya nyayo na Heel spurs lakini si hivyo tena japo heel spurs huweza pelekea plantar fasciitis.
Ugunduzi wa Tatizo na Matibabu.
Tabibu/daktari atafanya uchunguzi wan je kupima hali ya unyayo wako ili kujua kina hasa cha maumivu kipo wapi ili kujirisha kwamba maumivu hayo hayasabishwi na kitu kingine.
Matibabu
Sindano au vidonge pamoja na mazoezi na vifaa tiba kulingana na hali ya mgonjwa na kina cha tatizo.
Gharama za Matibabu.
Gharama za Matibabu huanzia Tsh 45,000/- Hadi Tsh 65,000/- Kulingana na Vifaa Tiba na Huduma za kupatiwa Mhusika.
Tunapatikana Tandika Magorofani. - Dar Es Salaam.
Call/ Text/ WhatsApp 0624 7400 12.