06/10/2025
Nafahamu furaha mliyo nayo ni kubwa mno, Baada ya miaka mingi na kushirikiana kwenye maombi,
Kupitia safari ya changamoto ya kukosa mtoto— Hatimaye majibu ya kipimo yamekuja POSITIVU..
*Ipo hivi.....*
Safari ya kiafya haimaliziki kwenye kicheko cha majibu...MSIJISAHAU....
Hapa ndipo familia nyingi hukose wanasimama kusherehekea bila kujua kuwa hatua ya kwanza ndiyo imeanza...
*Jiulizeni maswali haya....👇*
Je, lishe ya ujauzito itandaliwa kuhakikisha mtoto anakua bila hatari za upungufu wa damu, shinikizo la juu au kisukari cha mimba...?
Je, kliniki ya kwanza mtahudhuria kwa pamoja ili kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu wa awali...?
*NB:* Ujauzito ni zawadi, lakini pia ni jukumu, Ni kipindi kinachohitaji ufuatiliaji, lishe bora, mazoezi mepesi ya usalama, na uchunguzi wa kitaalamu wa mara kwa mara...
Miujiza ya kushika mimba ni hatua ya kwanza… Lakini kupokea mtoto mwenye afya njema mikononi mwako— Ndiyo ushindi wa kweli....
Usiishie kufurahi tu, anza safari ya kliniki mapema, Jipatie elimu ya lishe na afya ya uzazi kutoka kwa mtaalamu, kwa sababu afya ya kesho inaanza na hatua unazochukua leo.....
*By Dr kilatenga | Jifunze na chukua hatu kuboresha afya yako...🩺🫡*