22/06/2025
Unajua Haya yoteee... Siku Moja Itakuwa Hadithi tu??
Ila kwa leo... Acha Mpambano uendelee
K**a wewe ni hustler..
Ukweli ni kwamba,
Hakuna hadithi ya mafanikio ya kweli isiyoanzia na challenges, maumivu....
..na imani kali ilioonekana k**a uwendawazimu kwa muda huo.
Ila ukiendelea kukaza. Ipo Siku moja…
Utakaa chini, utamwambia mtu:
> “Nilikuwa na ndoto kubwa, nilikuwa sina kitu… lakini nilianza Na bila kuchoka niliamua kupambana.”
Na huyo mtu atakutazama kwa mshangao mkubwa sana.
Kwa challenges na uzito wa hadithi yako....
Atashindwa kuamini k**a mtu k**a wewe umeweza kuvuka yote hayo.
Atashindwa kuamini k**a ulipitia misukosuko yote hiyo (Ambayo pengine kiuhalisia ndiyo unapitia kwa sasa)
Na bado... ulisimama imara. Hukuyumba wala kukata tamaa.
Naamini hii inaweza kuwa hadithi yako ya baadae.
Lakini, leo bado hujawa hadithi hiyo.
Leo bado uko kwenye uwanja wa mapambano makali sana.
Basi usikate tamaa, mana mwisho wako unaweza kuwa mzuri sana.
Na Leo ndiyo siku ya kujitolea na kufanya kazi kwa bidii... Bila kukata tamaa.
Watakuona chizi... Umepotea... Au umevurugwa.
Watataka ushindwe ... Ili wakuambie, "SI TULISEMA SISI..."
Watasema, "Tuone atafika wapi na jeuri yake!?"
But, Don't worry 😁😊...
Hawaoni unachokiona.
Hawawazi unachokiwaza.
Leo... mambo yanaweza kuwa magumu. Ni ruksa kuchoka na kupumzika lakini usikate tamaa.
Leo na muda huu wa maisha yako Inaweza ikawa siku ya kuumia lakini tunakua kwa maumivu na changamoto hivyo inabidi tu uendelee kutembea.
Leo Inaweza kuwa siku ya kuanguka lakini kamwe usibaki chini.
Kila tone la jasho leo,
kila kukataliwa leo,
kila kukosa usingizi kwa ajili ya ndoto zako...
Hayo yote ni maneno na chapters unazoandika ili kukamilisha hadithi yako ya baadaye.
Usisubiri mazingira yakupe nafasi kuwa perfect.
Usingoje support ya kila mtu. Anza.... Wakiona wataku support tu.
Usikae tu ukiishia kuota na kutamani — amka ufanye kweli... Anza hata kidogo.
Kumbuka tu...:
Hakuna mtu aliyewahi kuandika hadithi ya kweli ya mafanikio akikaa tu na ndoto na kusubiri.
Hadithi zinatengenezwa na watu wanaojua kuwa leo ni vita na wakaamua kupambana kweli.
Kwa hiyo,
Chagua kupambana leo.
Kwa sababu naamini ipo siku kesho, utaangalia nyuma na kusema:
> “Nilifanya nilichopaswa kufanya… ndiyo maana leo nina hadithi ya mafanikio ya kusimulia na kuwa inspiration kwa wengine.”
Leo sio mwisho. Ni mwanzo tu wa hadithi yako ya kipekee ya mafanikio.
Siku moja itakuwa hadithi. Lakini lazima ukubali leo iwe mapambano ya kweli.
Naamini, HATA SISI TUNAWEZA🔥🔥✍️