11/11/2025
Facebook Huangalia Nini Kabla ya Kulipa (Monetization Criteria)
Facebook hatoi malipo tu kwa sababu ya views au followers bali inachunguza vitu vinne vikubwa👇👇
1️⃣ Kiwango cha uhalisia wa akaunti (Authenticity & Originality). Facebook hulipa wale wanaotengeneza content halisi (original content) si waliyochukua kutoka kwa watu wengine.
Mfano mtu ana followers 3.5k anaweza kuwa anaweka video zake mwenyewe (si repost), anatumia sauti yake mwenyewe au AI voice, ana captions na maudhui ya kipekee.
Lakini wakati huo huo kuna mtu mwingine ana 1M views lakini video ni repost au kachukua vitu alivyoandika mtu mwingine basi Facebook haihesabu k**a eligible kwa malipo.
2️⃣ Uhalisia wa engagement (Meaningful Interactions). Facebook haangalii tu idadi ya views, bali je, watu wanacomment kweli? Je, wanatazama video hadi mwisho? je, wanashare au ku-save?
Mtu anaweza kuwa na 3.5k followers lakini k**a ana community hai (active audience) engagement zake zina quality kubwa zaidi na algorithm inampendelea.
3️⃣ Kuwasha & kutimiza Vigezo vya Monetization. Kuna aina kadhaa za monetization, na kila moja ina masharti tofauti mfano angalia hapa 👇👇👇
a) In-stream ads (kwa video ndefu) Angalau account iwe na 5,000 followers.
b) Dakika 60,000 za kuangaliwa video (watched minutes) ndani ya siku 60. Je huwa unaangalia k**a video zako zinafikisha dakika 60,000 za utazamwaji? Na ni lazima video ziwe original na watu waziangalie hadi mwisho
c) Reels Bonus / Ads on Reels. Facebook huchagua kwa invitation program kigezo kikubwa ni reels zako kupata consistency ya engagement
Hata k**a una 3.5k followers, unaweza kuingizwa kwenye reels bonus k**a Facebook inaona content zako zinawashirikisha watu vizuri.
d) Stars Followers wanakutumia zawadi. Unahitaji kufikisha 500 followers na Video 5 zilizotengenezwa binafsi ndani ya siku 30
Kwa hiyo mtu mwenye 3.5k followers anaweza kuwa anapokea pesa kupitia stars au reels ads si lazima awe na milioni za views.
4️⃣ Uzingatiaji wa sheria za monetization. Facebook hukagua mambo kadhaa mfano hakuna copyright issues.
Hakuna community violations k**a hate speech, nudity, etc.
Akaunti imeunganishwa na professional mode
Wengi wana views nyingi lakini wanashindwa kulipwa kwa sababu ya haya makosa madogo madogo. Wakati mwingine mtu mwenye 50k followers hawezi kulipwa kwa sababu page yake imejaa reposts au haijakamilisha vigezo vya Professional Mode.
゚