04/04/2025
𝗦𝗔𝗥𝗔𝗧𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜 (𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜):
Homa ya ini husababishwa na maambukizi ya virus vya Hepatitis lakini pia homa ya ini inaweza kusababishwa na mabadiliko ya mtindo wako wa maisha.
Virus vya hepatitis B vinasambazwa na kuambukizwa kupitia njia mbali mbali k**a vile:
𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗝𝗜𝗔 𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗔𝗠𝗕𝗨𝗞𝗜𝗭𝗔 𝗩𝗜𝗥𝗨𝗦 𝗩𝗬𝗔 𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜:
- kujamiana na mtu mwenye kuishi na maambukizi ya virusi vya homa ya in.
- Kushika maji maji yatokayo mwilini mwa mtu mwenye maambukizi k**a jasho, mkojo, mate manii na damu.
- Mama mjamzito anaweza kumuambukiza mtoto katika kipindi cha ujauzito au kujifungua.
- Kuchangia damu na mtu mwenye tatizo hili.
- kuchangia vifaa vyenye ncha kali.
- Kuvaliana nguo.
𝗟𝗜𝗩𝗘𝗥 𝗖𝗜𝗥𝗥𝗛𝗢𝗦𝗜𝗦 - 𝗦𝗔𝗥𝗔𝗧𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜:
Homa ya ini aina ya Hepatitis hupitia hatua kuu tano hadi ini kuacha kufanya kazi kutokana na uwepo wa maambukizi ya muda mlefu pasipo kutibiwa, na maranyingi sana tatizo hili hutibika moja kwa moja ikiwa katika 𝗵𝗮𝘁𝘂𝗮 𝘇𝗮 𝗮𝘄𝗮𝗹𝗶 𝘇𝗮 𝗹𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗶𝗻𝗳𝗹𝗮𝗺𝗺𝗮𝘁𝗶𝗼𝗻 𝗻𝗮 𝗵𝗮𝘁𝘂𝗮 𝘆𝗮 𝗽𝗶𝗹𝗶 𝘆𝗮 𝗟𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗙𝗶𝗯𝗿𝗼𝘀𝗶𝘀 kwasababu hatua hizi maranyingi sana ini linakuwa bado halijashambuliwa vizuri na kuchoka, Ini linakuwa bado lipo safi na salama na kazi zake.
Hatua ya kwanza na hatua ya pili mgonjwa hupitia dalili nyepesi nyepesi na sio za kudumu zinazo kuja na kupotea, mfano wa dalili hizi ambazo sio za moja kwa moja kwa hatua hii ya kwanza na hatua ya pili.
- Miwasho ya ngozi.
- Kupungua uzito.
- Kukojoa mkojo wa njano pindi mgonjwa asipo kunywa maji mengi.
- Maumivu ya tumbo upande wa kulia upande wa ini au upande wowote.
- Kupoteza hamu ya kula na kuhisi kichefuchefu.
- Kuwa na msongo mkubwa wa mawazo.
- Tumbo kujaa gesi na kuhisi kushiba mara kwa mara.
- kuwa na wasi wasi kwa mgonjwa.
Lakini 𝗵𝗮𝘁𝘂𝗮 𝘆𝗮 𝘁𝗮𝘁𝘂 𝘆𝗮 𝗹𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗰𝗶𝗿𝗿𝗵𝗼𝘀𝗶𝘀
na 𝗵𝗮𝘁𝘂𝗮 𝘆𝗮 𝗻𝗻𝗲 𝘆𝗮 𝗹𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗰𝗮𝗻𝗰𝗲𝗿 huwa hakuna matibabu ya moja kwa moja ya kumaliza tatizo hili, kwasababu kupitia hatua ya tatu maranyingi sana ini linakuwa tayari limeshakuwa na 𝗖𝗶𝗿𝗿𝗵𝗼𝘀𝗶𝘀 hatua hii huwa hakuna matibabu isipokuwa mgonjwa anahitajika kwenda kufanya 𝗹𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗧𝗿𝗮𝗻𝘀𝗽𝗹𝗮𝗻𝘁 𝗸𝘂𝗽𝗮𝗻𝗱𝗶𝗸𝗶𝘇𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗷𝗶𝗽𝘆𝗮.
Cirrhosis ni hatua ya tatu ya homa ya ini ambayo ndio chanzo kikuu cha saratani ya ini yani 𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗼𝗰𝗲𝗹𝗹𝘂𝗹𝗮𝗿 𝗰𝗮𝗿𝗰𝗶𝗻𝗼𝗺𝗮 saratani ya ini husababisha ini kusinyaa na kushindwa kufanya kazi (𝗟𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗳𝗮𝗶𝗹𝘂𝗿𝗲𝘀) ini lina sinyaa na kuacha kufanya kazi kabisa.
Kupitia hatua ya tatu ya homa ya ini mgonjwa anapata dalili kubwa kubwa na hatarishi k**a vile.
- Tumbo kujaa maji (Ascites).
- Miguu na sura kuvimba.
- Kukojoa mkojo wa njano au kahawiya iliyo kolea sana.
- Vidonda sugu vya tumbo na tumbo kujaa gesi.
- kupoteza hamu ya kula na kuhisi kichefuchefu cha mara kwa mara.
- Macho na ngozi hubadilika rangi na kuwa na rangi ya njano.
- Miwasho sugu ya ngozi hasa majira ya jioni.
𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲, 𝗸𝘄𝗮𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘇𝗮 𝘂𝘀𝗵𝗮𝘂𝗿𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗶𝗯𝗮𝗯𝘂.