WikiElimu

WikiElimu WikiElimu ni tovuti ya wazi inayoruhusu jumuiya ya kimataifa ya wataalamu wa afya kuongeza na kuhariri maudhui ya kitabibu au kutoa elimu ya afya kwa jamii

UGONJWA WA RUBELAUgonjwa wa rubella unaojulikana pia k**a surua ya ujerumani ‘’German measles’’ ni ugonjwa wa kuambukiza...
20/03/2025

UGONJWA WA RUBELA
Ugonjwa wa rubella unaojulikana pia k**a surua ya ujerumani ‘’German measles’’ ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi. Ugonjwa huu umekua adimu sana siku hizi kwa sababu ya chanjo inayotolewa kukinga ugonjwa huu utotoni. Kwa kawaida husababisha upele mwekundu unaosambaa usoni na kisha kuenea mwili mzima.

Mara nyingi  ugonjwa huu hausababishi dalili yoyote. Mtoto anaweza kuanza kupata homa ya kawaida, kuvimba kwa tezi na kutokwa na mak**asi siku 2 – 3 baada ya kuambukizwa. Watu wazima wanaweza kupata maumivu ya kichwa na maumivu ya viungo.

Tatizo kubwa zaidi linaloweza kusababishwa na ugonjwa wa huu ni kwa mama mjamzito. Ugonjwa huu unaweza kuleta athari mbaya kwa mtoto aliye tumboni, hasa akiambukizwa katika kipindi  cha mwanzo cha ujauzito.

JIFUNZE ZAIDI HAPA 👉
https://wikielimu.org/ugonjwa-wa-rubella-surua-ya-ujerumani/

KUAMBUKIZWA UGONJWA - UKIOGELEAKuogelea kwa kawaida ni shughuli nzuri na salama. Unaweza kupata ugonjwa k**a maji unayoo...
20/03/2025

KUAMBUKIZWA UGONJWA - UKIOGELEA
Kuogelea kwa kawaida ni shughuli nzuri na salama. Unaweza kupata ugonjwa k**a maji unayoogelea yana vimelea na ukayanywa au wakaingia kupitia kwenye jeraha. Unaweza pia kupata maambukizi kwenye mabwawa ya kuogelea, hata k**a maji yametibiwa vizuri kwa dawa ya chlorine. Kuna baadhi ya bakteria, virusi na vimelea kwenye mabwawa ya kuogelea wanaoweza kuendelea kuishi hata baada ya maji kutibiwa.

Watu wengi wanougua baada ya kuogelea wana harisha. Mara nyingi mtu hupona bila matibabu yoyote. Unaweza pia kupata ugonjwa wa homa ya mapafu (nyumonia) na magonjwa mabaya ya ngozi kutokana na maji yaliyochafuliwa

Ongea na daktari k**a una harisha damu, unaharisha kwa zaidi ya wiki moja , au k**a unakohoa na una homa. Onana na daktari haraka sana k**a una dalili nyingine kali, k**a vile homa na kukak**aa kwa shingo baada ya kuogelea kwenye mabwawa ya mtaani, au k**a una ugonjwa mbaya wa ngozi na una homa. Hakikisha unamwambia daktari kuwa uliogelea kwenye maji hayo.

JIFUNZE ZAIDI 👉 https://wikielimu.org/kuambukizwa-kupata-ugonjwa-wakati-wa-kuogelea/

KUVIMBA KILIMI/KIMEOKuvimba kilimi / Kuvimba kimeo ni hali inaweza kukera sana . Kuvimba kilimi (uvulitis) mara nyingi h...
20/03/2025

KUVIMBA KILIMI/KIMEO
Kuvimba kilimi / Kuvimba kimeo ni hali inaweza kukera sana . Kuvimba kilimi (uvulitis) mara nyingi huambatana na kuvimba kwa eneo la koromeo (phyrinx), mafindofindo (tonsilitis), kidaka tonge (epiglotis)  au kaakaa la mdomo (palate). Kilimi ni tishu ndogo yenye umbo k**a ulimi inayoning’inia kwenye sehemu ya nyuma ya mdomo.

SABABU ZA KUVIMBA KILIMI/KIMEO

Kuvimba kwa kilimi mara nyingi husababishwa na maambukizi ya bakteria – Bakteria ambao husababisha tatizo la kilimi, ndio hao hao husababisha ugonjwa wa homa ya mapafu ”pneumonia”, homa ya uti wa mgongo “Meningitis” na maambukizi katika Mfumo wa damu.
Sababu nyingine ni pamoja na:
▪︎Kuunguzwa na vinywaji vya moto
▪︎Kuumia eneo la koo
▪︎Mzio ”allergy” unaotokana na kizio k**a vile chamvua za mimea, vumbi, chakula k**a vile njugu au mayai au manyoya ya wanyama
▪︎Kuvuta au kumeza aina fulani za kemikali
▪︎Uvutaji wa sigara

JIFUNZE ZAIDI HAPA 👉 https://wikielimu.org/kuvimba-kimeo-kilimi/

KUINGILIWA NA KITU SIKIONIKuingiliwa na kitu sikioni ni tatizo. K**a kitu kitaingia na kung’ang’ania ndani ya sikio  kin...
20/03/2025

KUINGILIWA NA KITU SIKIONI
Kuingiliwa na kitu sikioni ni tatizo. K**a kitu kitaingia na kung’ang’ania ndani ya sikio  kinaweza kusababisha usumbufu na kusababisha ushindwe kusikia kwa kitambo k**a kitaziba njia nya sikio. K**a ni kitu chenye ncha kali kinaweza kutoboa ngoma ya sikio.

Watoto wadogo wakati fulani wanaweza kuweka vitu masikioni. Vitu k**a mbegu, vidude vya kuchezea au vipande vya karatasi. K**a hujaona wakiweka masikioni, inaweza kuwa ngumu kujua kuwa wameweka mpaka utakapoona wakilalamika maumivu sikioni, uchafu unatoka sikioni au wanashindwa kusikia vizuri.

Watu wazima hubakiza vipande vya pamba kwenye sikio wakati wa kusafisha. Utaratibu huu wa kusafisha masikio kwa kutumia vijiti vyenye pamba haushauriwi na madaktari, kwa sababu unaweza kuleta madhara. Kwa mara chache wadudu wanaweza kuingia na kukwama ndani ya sikio, hii inaweza kushtua, hasa kwa mtoto.

JIFUNZE ZAIDI 👉 https://wikielimu.org/kuingiliwa-na-kitu-sikioni-na-jinsi-ya-kukitoa/

KUSIKIA KELELE MASIKIONI AU KICHWANIK**a unatatizo la kusikia kelele masikioni au kichwani (tinnitus), unahisi k**a keng...
20/03/2025

KUSIKIA KELELE MASIKIONI AU KICHWANI
K**a unatatizo la kusikia kelele masikioni au kichwani (tinnitus), unahisi k**a kengele inapigiwa masikioni, sauti ”buzzz” k**a mdudu anayeruka au sauti ”hissss” k**a nyoka. Unasikia sauti k**a zinaanzia masikioni au kichwani na ukitafuta chanzo cha kelele hizi kwenye mazingira uliyopo hakipo. Kelele hizi zinaweza kuwepo muda wote au zinaweza kuwa zinakuja na kuondoka. Zinaweza kusababisha ukashindwa kupata usingizi, ukashindwa kufanya vitu kwa umakini, na ukapatwa na ugonjwa wa sonona.

Kadri muda unavyokwenda ukiwa na tatizo la kusikia kelele masikioni, unaweza kuanza kuwa mtu wa wasiwasi mwingi. Watu wanaopatwa na tatizo hili, mara nyingi hupoteza uwezo wa kusikia wanapofika uzeeni. Wengi wa waathirika huwa na historia ya kufanya kazi au kuishi maeneo yenye kelele nyingi. Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuchangia mtu kupata tatizo la kelele masikioni ni pamoja na:

▪︎kusafiri kwa ndege
▪︎Ongezeko la shinikizo la damu
▪︎ kujaa kwa nta kwenye masikio
▪︎Matatizo kadhaa ya sehemu ya ndani ya sikio ‘’inner ear’’ na
▪︎Baadhi ya madawa

JIFUNZE ZAIDI HAPA 👉 https://wikielimu.org/tatizo-la-kusikia-kelele-masikioni-kichwani/

KUSHINDWA KUZUIA MKOJOWanawake wengi wana tatizo la kushindwa kuzuia mkojo, yaani wanajikojolea /kuvuja mkojo kwa sababu...
19/03/2025

KUSHINDWA KUZUIA MKOJO
Wanawake wengi wana tatizo la kushindwa kuzuia mkojo, yaani wanajikojolea /kuvuja mkojo kwa sababu ya kushindwa kudhibiti kibofu. Tatizo hili linazidi zaidi kunapoongezeka mgandamizo kwenye kibofu, kwa mfano unaweza kujikojolea/ kushindwa kuzuia mkojo unapokohoa, kupiga chafya, kufanya mazoezi, au kuinua kitu kizito.

Hali hii inaweza kusababishwa na kulegea kwa misuli ya nyonga, misuli hii inategemeza kibofu, mji wa mimba (uterasi) na puru/rektamu. Ni kawaida kulegea kwa misuli ya nyonga kwa wanawake waliojifungua watoto. Sababu nyingine za kushindwa kuzuia mkojo ni pamoja na kufunga choo, maambukizi kwenye kibofu, mabadiliko ya homoni baada ya ukomo wa hedhi, na baadhi ya dawa k**a vile ‘’diuretics’’ (dawa hizi zinatumika kudhibiti shinikizo la juu la damu).

Baadhi ya wanawake wanatatizo la kushindwa kuusubirisha mkojo, akihisi kukojoa inabidi akakojoe haraka, la sivyo anaweza kujikojolea au wengine mkojo unapita bila hata kujijua. Tatizo hili wakati mwingine linaweza kutokana na matatizo kwenye neva zinazodhibiti kibofu.

JIFUNZE ZAIDI 👉 https://wikielimu.org/kushindwa-kuzuia-mkojo/

KUCHA ZENYE MWONEKANO MBAYASababu kubwa zaidi inayosababisha kucha zenye mwonekano mbaya ni mambukizi ya fangasi. Mara n...
19/03/2025

KUCHA ZENYE MWONEKANO MBAYA
Sababu kubwa zaidi inayosababisha kucha zenye mwonekano mbaya ni mambukizi ya fangasi. Mara nyingi fangasi wanathiri zaidi kucha za miguu, hasa miguu inayotokwa jasho au k**a haikauki vizuri baada ya kuiosha. lakini pia , kucha zinaweza kupata maambukizi kwa sababu ya unyevunyevu unaojificha chini ya kucha za kubandika.

Ukucha unakuwa mnene, unamomonyoka kwa urahisi na unabadilika rangi na kuwa mweupe /manjano.  Ukucha unakua ukiwa na sura mbaya au umbo ambalo halipendezi au unakua ukiwa umenyanyuka na haugusi sakafu ya ukucha.

Matatizo mengine ni k**a vile kuwa na kucha kavu, ngumu na zinazokatika au kuchanika kwa urahisi, baadhi huwa na madoadoa meupe kwenye kucha ambayo hutokea baada ya kuumia kucha. Wengine huwa na kucha zenye mikunjo mikunjo, hii utaipata zaidi kwa wazee. Kwa baadhi ya nyakati, mabadiliko kwenye kucha yanaweza kuashiria kuwa una ugonjwa mwingine ndani ya mwili.

JIFUNZE ZAIDI 👉 https://wikielimu.org/kucha-zenye-mwonekano-mbaya-na-zinazokatika-katika/

UUME KUSHINDWA KUSIMAMAWanaume wengi huwa wanapata shida hii ya kushindwa kusimamisha uume kwa wakati fulani au wengine ...
19/03/2025

UUME KUSHINDWA KUSIMAMA
Wanaume wengi huwa wanapata shida hii ya kushindwa kusimamisha uume kwa wakati fulani au wengine wanaweza kusimamisha ila baada ya muda uume unalala na hausimami tena.

Sababu kubwa huwa ni msongo, uchovu, matumizi ya pombe kupita kiasi au ugonjwa wa hivi karibuni. K**a ukiamka asubuhi unakuta uume umesimama, basi kushindwa kusimamisha kwa siku moja sio swala linalopaswa kukutia wasiwasi.

Tatizo la kudumu la kushindwa kusimamisha uume linaweza kusababishwa na ugonjwa k**a vile kisukari na magonjwa mengine yanayoathiri mfumo wa kuzungusha damu mwilini au madawa, k**a vile madawa ya kudhibiti shinikizo la juu la damu au madawa ya kudhibiti sonona.

Tatizo hili pia linaweza kusababishwa na wasiwasi uliozidi kipimo au matatizo kwenye mahusiano. Kadri unavyoendelea kuzeeka, inaweza kuchukua muda mrefu zaidi uume kusimama na ukishasimama unakuwa hauna nguvu sana.

JIFUNZE ZAIDI HAPA 👉 https://wikielimu.org/kushindwa-kusimamisha-uume/

KUWASHWA SEHEMU YA HAJA KUBWAKuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa (mk*ndu), ni hali inayoleta karaha sana na inaweza ku...
18/03/2025

KUWASHWA SEHEMU YA HAJA KUBWA
Kuwashwa sehemu ya kutolea haja kubwa (mk*ndu), ni hali inayoleta karaha sana na inaweza kuaibisha kwa sababu unapata hamu kubwa ya kutaka kujikuna.

Ngozi inayozunguka mk*ndu inaweza kuwa nyekundu na inayouma, na inaweza kuvuja damu na hata kupata maambukizi k**a utapakuna sana. Kuwashwa mara nyingi huwa kunazidi baada ya kujisaidia na usiku.

Mtu anaweza kuwashwa mk*ndu kwa sababu ya harara inayotokana na bidhaa za kujitawadhia au marashi anayotumia, jasho, unyevu unyezi au vipande vya mavi vinavyobakia kwenye ngozi kuzunguka eneo la kutolea haja kubwa.

Watu ambao wana uzito mkubwa, wanaotokwa jasho jingi sana au wanaovaa chupi zinazobana sana wako kwenye hatari zaidi ya kuwashwa. Wakati mwingine aina fulani za vyakula, zinaweza kuchangia tatizo hili. 

Bawasiri na minyoo inayoitwa ‘’pinworm’’ ni sababu pia za tatizo hili.

JIFUNZE ZAIDI HAPA 👉 https://wikielimu.org/kuwashwa-sehemu-ya-kutolea-haja-kubwa/

MAUMIVU YA UUME Maumivu ya uume – ngozi inayoufunika uume ni nyepesi na ni rahisi kuumia. Mikwaruzo midogo midogo inawez...
18/03/2025

MAUMIVU YA UUME
Maumivu ya uume – ngozi inayoufunika uume ni nyepesi na ni rahisi kuumia. Mikwaruzo midogo midogo inaweza kutokea wakati wa michezo au wakati wa ngono.

Maumivu kwenye kichwa cha uume yanaweza kusababishwa na usafi duni au kwa sababu ya harara inayosababishwa na sabuni au maambukizi, hii ni pamoja na maambukizi ya magonjwa ya ngono.

Dalili nyingine za magonjwa ya ngono ni pamoja na upele, uchafu kutoka kwenye uume na maumivu wakati wa kukojoa. Kwa wale ambao hawajatahiriwa, wanaweza kupata maumivu uume ukisimama au wakati wa ngono kwa sababu ya govi kubana sana ‘’overtight’’.

JIFUNZE ZAIDI 👉 https://wikielimu.org/maumivu-ya-uume/

MAPIGO YA MOYO KWENDA MBIOMapigo ya moyo kwenda mbio – kwa kawaida moyo unapopiga huwa hatuna ufahamu au kuhisi kuwa una...
18/03/2025

MAPIGO YA MOYO KWENDA MBIO
Mapigo ya moyo kwenda mbio – kwa kawaida moyo unapopiga huwa hatuna ufahamu au kuhisi kuwa unapiga, lakini unapoanza kwenda mbio au kupiga isivyo kawaida unahisi unaenda kwa kasi au unapiga isivyo kawaida. Kwa wakati mwingi hali hii ni ya kawaida. Sababu za hali hii ni pamoja na mazoezi, furaha, msongo, wasiwasi na kutumia viamsha mwili k**a vile kahawa yenye kafeini au sigara yenye nikotini.

Katika hali ya kawaida mapigo ya moyo huenda mbio kwa sekunde au dakika kadhaa na baadae hupungua na hutokea bila kuwepo kwa dalili nyingine yoyote. Mapigo ya moyo yanapoenda mbio sio tatizo la kutia wasiwasi, lakini k**a yakianza kwenda mbio bila sababu ya msingi au yakitokea sambamba na dalili nyingine au k**a yataendelea kupiga kwa muda mrefu, yanaweza kuwa yanashiria kuwa kuna tatizo.

JIFUNZE ZAIDI HAPA 👉 https://wikielimu.org/mapigo-ya-moyo-kwenda-mbio/

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when WikiElimu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to WikiElimu:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram