12/06/2025
VIDONDA VYA TUMBO(PEPTIC ULCERS),
VIDONDA VYA TUMBO
Hivi ni vidonda ambavyo vinapatikana kwenye kuta za tumbo (stomach) na utumbo mwembamba (duodenum).
▪️FAIDA
_Kwenye kuta za tumbo kunazalishwa utando mzito wa k**asi (protective mucous coating) kwaajili ya kulilinda tumbo na utumbo mwembamba. Pia huzalishwa asidi (Hydrochloric acid) kwaajili ya kusaidia kumeng'enywa chakula na kuua vijidudu (bacteria) wanaongia tumboni kupitia chakula, maji au kugusana midomo kati ya m/Maambukizi na mzima mfano kissing ._
SABABU ZA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo husababishwa na sababu kuu mbili.:
1.▶️ Maambukizi ya bacteria (Helicobacter Pylori i.e H.Pylori infections)
H.pylori mara baada ya kuingia tumboni hudhoofisha ute mzito wa k**asi ndani ya tumbo na utumbo mwembamba, hivyo huruhusu asidi kupenya na kuingia ndani zaidi ya kuta za tumbo. Asidi na bacteria husababisha maumivu na kidonda kwenye kuta za tumbo na utumbo mwembamba. Umbile la mnyongoroto la huyu bacteria pia huchangia kuchimba zaidi kuta za tumbo na utumbo mwembamba.
_FAIDA_
Nilisema ndani ya tumbo kunazalishwa asidi kwaajili ya kuua vijidudu (bacteria).
_*Swali*_: Kwanini bacteria huyu hauliwi(hadhuriki) na hiyo asidi?.
_*Jibu*_: H.pylori anaweza kuishi tumboni bila kuuliwa na hiyo asidi kwasababu anajizalishia kemikali (enzymes) iitwayo *UREASE ENZYMES*, ambayo inabadili urea kuwa ammonia (basic compound) ambayo inapambana na asidi (neutralization) na kufanya mazingira yawe ya kawaida kwake.
2.▶️ Matumizi ya muda mrefu madawa ya kuondosha maumivu (Nonsteroidal anti-inflammatory drugs i.e NSAIDS)
Ndani ya tumbo na utumbo mwembamba kunazalishwa kemikali iitwayo *Cyclo -oxygenase (COX-1)* isoenzymes inayobadili asidi iitwayo *arachidonic acid* kuwa kemikali iitwayo *prostaglandins*. Hii prostaglandin huupa ukuta wa tumbo na utumbo mwembamba ulinzi. Madawa haya ya kuondosha maumivu mfano Aspirin,Ibuprofen Diclofenac n.k yanapotumika kwa muda mrefu huleta madhara ya kuzuia kuzalishwa kwa COX-1 ambapo husababisha prostaglandin iwe finyu tumboni mwishowe kuta za tumbo hupata michubuko na vidonda vya tumbo hutokea.
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO⤵️
1.🧷 Kupata maumivu ya tumbo ya kuwaka moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
2.🧷 Kupatwa na kiungulia(heartburn) karibu na chembe ya moyo
3.🧷 Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
4🧷 Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
5.🧷 Kupata haja kubwa ya rangi ya kahawia au nyeusi cheenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
6.🧷 Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
7.🧷 Kushindwa kupumua vizuri.
8.🧷Kuharisha hasa unapokula vyakula vinavyochochea vidonda vya TUMBO.
9.🧷Kupata choo kigumu k**a cha mbuzi
10.🧷 Maumivu ya mgongo
11.🧷 Tumbo kuwaka moto.
12.🧷 Kupungukiwa damu na kupelekea kupata kizunguzungu.
13.🧷 Mwili kudhoofika na kupungukiwa kilo
14.🧷 Dhakari(Uume) kulegea/kusinyaa na kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
15.🧷Mapigo ya moyo kwenda mbio.
16.🧷 Macho kupunguza nguvu ya
VICHOCHEZI VYA TATIZO
Unaweza kuongeza ukubwa wa tatizo la vidonda vya tumbo au kuchelewa kupona hata K**a unatumia dawa ikiwa utafanya yafuatayo:
1. 🧷Uvutaji sigara (smoking)
2.🧷Unywaji wa pombe (alcohol drinking)
3.🧷 Kuwa na msongo wa mawazo kupitiliza (untreated stress)
4.🧷Kula vyakula vyenye viungo vingi
5.🧷 Kunywa kahawa
6.🧷Kula vyakula vyenye kuleta gesi.
7.🧷Kula vyakula vyenye asidi mfano jamii ya ndimu au nyanya.
8.🧷 Kula kupita kiasi
9.🧷 Kutokua na ratiba maalum ya kula mfano kukaa na njaa kwa muda mrefu n.k
_Itambulike hizi sio visababishi vya vidonda bali huchochea vidonda kutopona na kuchimbika zaidi._
DALILI HATARISHI ZA VIDONDA VYA TUMBO (COMPLICATIONS)
Vidonda vya tumbo vikiiachwa bila kutibiwa kwa muda mrefu au mgonjwa akijiweka kwenye vichochezi, hujiweka kwenye dalili hatarishi k**a zifuatazo:
1.◾ Damu kuvujia ndani ya tumbo (internal bleeding)
2.◾ Kupatikana tundu ndani ya tumbo au utumbo mwembamba(percolation)
3.◾ Kuziba kwa njia ya chakula kitokacho tumboni kwenda kwenye utumbo mwembamba(obstruction).
4.◾ Kupata saratani ya tumbo(gastric cancer)
5.◾ Kupoteza maisha(death)
TIBA ZA VIDONDA VYA TUMBO
Tunatoa tiba sahihi na salama kabisa ya Vidonda vya tumbo ambazo zimeshafanyiwa vipimo na zipo kisheria zimethibitishwa na taasisi kubwa za kiafya duniani pamoja na tanzania.
Muhimu.
⚫ Ni vyema kutambua kuwa dalili hizi pia zinaweza kusababishwa na magonjwa mengine, na kwamba uwepo wa moja au zaidi ya dalili hizi haimaanishi kwamba mtu ana tatizo la vidonda vya tumbo. Ikiwa una wasiwasi kuhusu dalili yoyote, ni muhimu kwenda hospital kwanza kufanya vipimo kujua tatizo ni nini hasaa kabla ya kutumia dawa.
+25564699353
+255745680156
DR MSUYA HERBAL CLINIC
-----------------------------------------------------------