03/10/2025
K**a ni kweli… basi soka la Africa bado lina maswali mengi kuliko majibu!
Leo tumeshuhudia mchezaji wa zamani wa Yanga, Jesus Moloko, akiomba jezi na hata kupewa pesa na Fiston Mayele, aliyewahi kung’aa naye pale Jangwani na sasa anakipiga Pyramid.
👉 Swali gumu: Hivi wachezaji wanaoimba na kupigiwa makofi makubwa pale Taifa leo tunawapa thanani kubwa ila baadae wanasahaulika kiasi hiki?
Je, hii ni ishara kwamba:
1. Klabu haziwalipi vizuri wachezaji wake k**a tunavyosikia? 🤔
2. Au ni kwamba wachezaji wenyewe hawana mpango wa maisha baada ya soka?
Kwa macho ya wengi, kitendo cha Mayele kumpa Moloko jezi na pesa kinaonekana cha utu na urafiki… lakini kwa macho ya wachache, ni aibu kubwa kwa klabu kubwa k**a Yanga na mchezaji mwenyewe kufikia hatua ya kuomba msaada hadharani. 😬
⚽ Sasa nauliza nyie mashabiki:
Ni heshima kwa Mayele kumpa msaada mwenzake hadharani tena mbele ya kamera?
Au ni doa linaloonyesha namna mfumo wa soka la Afrika Mashariki ulivyo dhaifu kwa wachezaji wake?