07/08/2025
Nisikilize mwanangu,
Usikubali mwanamke akuchezee kihisia. Akikuomba kitu na kwa kweli huna uwezo nacho, mtazame usoni umwambie:
"Hapana. Siwezi kukusaidia kwa sasa."
Akipigwa na butwaa au kuanza kukutusi kwa maneno k**a:
"Dah! Sikujuaga wewe ni maskini hivi!"
Mjibu kwa utulivu:
"Sasa umeshajua. Na tafadhali usiniombe tena."
Wanawake wengi wa leo wanacheza na ego ya mwanaume, ile hamu ya kutaka kuwavutia, na hofu ya kuachwa — ili kuwanyonya hadi tone la mwisho. Hawaanzi kwa kukutaka pesa moja kwa moja. Wanaanza kwa akili zako, hisia zako, na uanaume wako.
Simama imara.
K**a hawezi kujinunulia mwenyewe, hana haki ya kimaadili kukutaka wewe umnunulie. Wala hana haki ya kukufanya ujihisi vibaya ukimkatalia.
Mwanamke si jukumu lako la kifedha. Ni mtu mzima. Kila mtu mzima anapaswa kujibeba. Tunachotoa ni msaada — si utumwa. Tunatoa kwa upendo, si kwa mashinikizo.
Usijiuwe kwa kujaribu kumpendezesha mtu.
Mwanamke akikuomba pesa mara kwa mara ilhali anajua jinsi unavyohangaika na majukumu yako yote — huyo si tu mwenye roho ngumu. Ni mwizi.
Mwanamke mwenye busara hatakukamua. Atajisimamia mwenyewe huku ukijenga. Atakupunguzia mzigo, si kuongeza.
Wewe si mradi wa kuchangishwa pesa. Pokea akili!
Umenielewa vizuri?