10/10/2025
Habari....mstaafu zingatia haya mambo 7 tafadhali kwa ustawi wako.....nawe ambae bado upo kazini jambo lako nakuletea punde tu....💃
MAMBO 7 HATARI KWA MAISHA YA USTAAFU
Habari za leo. Nimekuta hii habari Google nimeona niilete hapa, ili tuisome na kutoa mawazo yetu. Maisha ya ustaafu yapaswa kuwa bora zaidi, kwani unakuwa bosi wako mwenyewe 😂...basi uhondo wa ngoma usikunogee sana ukaharibu stepu za uchezaji🙆♀️
1. USIKUMBATIE MAMBO YA ZAMANI.
Ustaafu ni wakati wa kufurahia matunda ya kazi ya myaka iliyopita, wastaafu wengi hawafurahii kwa kukumbuka jana yao. Ni asili ya binadamu kuangalia jana. Jana yenye mafanikio, yenye ukuu, yenye kupendeza au kuchukiza na mengineyo. Iwapo jana hiyo tutaiwaza mara kwa mara, itatunyima kuangalia leo yetu tunayoiishi, ni hatari🤔. Inaweza kusababisha ushindwe kujaribu mambo mapya au kukutana na watu wapya. Acha tabia hii. Kumbatia siku uliyo nayo zaidi na karibisha fursa zote za siku hiyo kujifunza, jana na kesho zitajishughulikia zenyewe.
2. KUPUUZIA AFYA
Ni rahisi kupuuzia afya unapostaafu. Mhemko wa kustaafu, kutaka kila kitu ufanye, kutokuwa na ratiba ya mambo yako kwa masaa 12 ya mchana ni hatari kwa afya. Mwandishi anasema alikuwa anaangalia tv hadi masaa ya alfajiri🙄 akisikia njaa anakula vitafunwa akiwa kwenye tv duh....afya yake ilipozorota alijirudi na kuanza kulala masaa sahihi na kufuata sheria nyingine za afya. Tujiwekee ratiba sahihi ili tusitetereke kiafya.
3. KUJIEPUSHA NA JAMII
Wengi tunafikiri kujiondoa kwenye shughuli za jamii ni kupata muda wa kupumzika. Kujitenga ssna ni kukaribisha upweke. Tuwe na kiasi tuweke uwiano. Watafiti wanasema upweke ni hatari kwa afya, kwamba athari zake ni sawa na mtu aliyevuta sigara 15 kwa siku😯. Upweke unaambatanishwa na magonjwa ya moyo, kiharusi na hata kusababisha vifo vya ghafla. Ustaafu ni wakati unaofaa kufahamiana na wengine, kujiunga na clubs, kuanzisha hobby, kujitolea kwenye jamii, kufanya kazi part time nk...yote hayo yanawezekana kwa kiasi.
4. KUKATAA MABADILIKO
Ustaafu ni mabadiliko makubwa kimsisha, ni sawa kujisikia kukosa uhakika, lakini si sahihi kukataa kubadilika na kujaribu fursa ambazo zipo mbele yako. Kuwa na mawazo chanya na ubadilike kwa mazuri ili ukue upya katika phase hii ya ustaafu.
5.KUTUNZA VINYONGO
Maisha ni milima na mabonde, vikwazo na suluhu, mwisho wa siku kila mmoja wetu kabeba vinyongo.
Kuvikumbatia vinyongo ni hatari kwa mioyo yetu. Anza maisha ya ustaafu kwa kuamua kuvitupilia mbali....usimchukie mtu yeyote, usikumbuke mabaya...fanya ibada zaidi, samehe na sahau kwa ajili yako mwenyewe. Umri wako sasa ni wa kuishi kwa furaha na amani kuliko chochote, jifikirie wewe kwanza.
6.KUDHARAU VIPAUMBELE VYAKO
Hili ni kosa, usiache vipendaroho vyako eti kwa vile umestaafu ni maisha mapya...usiache uchoraji wako, kupiga piano kwako, kucheza ngoma, kuimba nk...furaha yako ni hivyo, viendeleze ukichanganya na vipya...wahenga walisema usiache mbachao kwa msala upitao, vipendaroho vya zamani visiachwe.
7.KUWAZA UCHUMI KUPITILIZA.
Ni kweli umestaafu kipato chako kitapungua. Sasa utaweka pesa zaidi kuliko kuzipokea. Utaogopa na kuingiwa na mashaka. Usiondoe amani yako kwa kuwaza sana utakaribisha magonjwa. Kuwa na kiasi, tumia hekima katika pesa zako matumizi yasizidi kipato unachopata wakati huu. Epuka matumizi yasiyo na tija. Kabla ya kununua kitu jiulize ukikikosa kitakuathiri?
Hisani:geediting.com, Google