20/01/2026
𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜 - 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨 𝗡𝗔 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢:
𝗛𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 (𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀) ni ugonjwa unaosababisha 𝗞𝘂𝘃𝗶𝗺𝗯𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶, 𝗦𝗮𝗿𝗮𝘁𝗮𝗻𝗶 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗻𝗮 𝗜𝗻𝗶 𝗸𝘂𝗮𝗰𝗵𝗮 𝗸𝘂𝗳𝗮𝗻𝘆𝗮 𝗸𝗮𝘇𝗶.
+255 0750 969 698
Mara nyingi ugonjwa huu wa ini unatokana na 𝗠𝗮𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶 𝘆𝗮 𝗺𝘂𝗱𝗮 𝗺𝗿𝗲𝗳𝘂 𝘆𝗮 𝘃𝗶𝗿𝘂𝘀𝗶, 𝗨𝗻𝘆𝘄𝗮𝗷𝗶 𝗣𝗼𝗺𝗯𝗲 𝗸𝘂𝗽𝗶𝘁𝗮 𝗸𝗶𝗮𝘀𝗶, 𝗠𝗮𝘁𝘂𝗺𝗶𝘇𝗶 𝗺𝗮𝗸𝘂𝗯𝘄𝗮 𝘆𝗮 𝗱𝗮𝘄𝗮 𝘇𝗮 𝗺𝗮𝘂𝗺𝗶𝘃𝘂, 𝗽𝗮𝗺𝗼𝗷𝗮 𝗻𝗮 𝗦𝘂𝗺𝘂.
𝗔𝗜𝗡𝗔 𝗞𝗨𝗨 𝗭𝗔 𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜 (𝗛𝗘𝗣𝗔𝗧𝗜𝗧𝗜𝗦)
1️⃣ 𝗩𝗶𝗿𝘂𝘀 𝘃𝘆𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗮𝗶𝗻𝗮 𝗔 𝘆𝗮𝗻𝗶 (𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗔)
✔️ Homa ya ini inaweza kusababishwa na virus vya homa ya ini aina ya Hepatitis
✔️ Virus hivi vya hepatitis A husambazwa au kuenezwa kupitia maji machafu /Chakula kichafu
2️⃣ 𝗩𝗶𝗿𝘂𝘀 𝘃𝘆𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗮𝗶𝗻𝗮 𝗕 𝘆𝗮𝗻𝗶 𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗕 (𝗛𝗕𝗩)
✔️ Virus vya homa ya ini B husambazwa kupitia kushika Damu yenye maambukizi,
✔️ Kushiliki vifaa vyenye ncha kali k**a vile sindano, wembe, mikasi au visu
✔️ Kushiliki ngono isiyo salama na mtu mwenye maambukizi,
✔️ Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto katika kipindi cha kujifungua
✔️ Kugusa maji maji yatokayo mwilini mwa mtu mwenye maambukizi ya virus vya homa ya ini k**a vile Jasho, mate au maji maji yatokayo sehemu za siri k**a manii au ukeni
✔️ Husambazwa kupitia njia ya kuongezewa damu yenye maambukizi
3️⃣ 𝗩𝗶𝗿𝘂𝘀 𝘃𝘆𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗮𝗶𝗻𝗮 𝗖 𝘆𝗮𝗻𝗶 𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗖 (𝗛𝗖𝗩)
✔️ Virus vya homa ya ini C inasambazwa kupitia kugusa Damu yenye maambukizi
✔️ Kushiliki vifaa vyenye ncha kali k**a vile sindano, wembe, mikasi au visu
✔️ Hepatitis C inasambazwa kupitia ngono isiyo salama na mtu mwenye maambukizi
✔️ Hepatitis C inasambazwa pia kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto katika kipindi cha kujifungua
✔️ Husambazwa kupitia njia ya kuongezewa damu yenye maambukizi
4️⃣ 𝗩𝗶𝗿𝘂𝘀 𝘃𝘆𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗗 𝘆𝗮𝗻𝗶 𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗗
✔️ Virus D hutokana na virus vya hepatitis B kwaiyo kwa wenye HBV huongeza madhara zaidi
5️⃣ 𝗩𝗶𝗿𝘂𝘀 𝘃𝘆𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗘 𝘆𝗮𝗻𝗶 𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗘
✔️ Virus E huenezwa kupitia kushika au kunywa Maji machafu
𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗗𝗔𝗟𝗜𝗟𝗜 𝗭𝗔 𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗧𝗜𝗭𝗢 𝗟𝗜𝗦𝗜𝗟𝗢 𝗧𝗜𝗕𝗜𝗪𝗔 𝗠𝗨𝗗𝗔 𝗠𝗥𝗘𝗙𝗨
Dalili za homa ya ini mara nyingi huanza polepole, na dalili hizi huwakuta baadhi ya watu kwa hatua za mwanzoni mwa ugonjwa na baadhi yao huendelea kuishi kwa miaka mingi bila kuona dalili yoyote.
Dalili huja kuonekana baada ya miaka mingi kupita inaweza kuwa miaka miwili, miaka mitatu na hata miaka kumi, Dalili za homa ya ini hufanana kabisa na dalili za magonjwa mengine ya mfumo wa chakula ivyo ni ngumu kutambua kwa hatua za mwanzoni za ugonjwa hadi kuthibitisha kwa vipimo
𝗠𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗮𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗱𝗮𝗹𝗶𝗹𝗶 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶 𝗸𝗮𝗺𝗮 𝘇𝗶𝗳𝘂𝗮𝘁𝗮𝘇𝗼:
✔️ Tumbo kujaa gesi mara kwa mara na kuwa gumu
✔️ Mgonjwa kupoteza hamu ya kula na muda mwingine kuhisi hali ya kichefuchefu
✔️ Maumivu ya tumbo upande wa kulia wa tumbo chini ya mbavu
✔️ Kuhisi hali ya kiungulia, vichomi na asidi ya tumbo
✔️ Uchovu mwingi yani uchovu wa mara kwa mara
✔️ Miwasho ya ngozi, Maumivu ya viungo, kukaza kwa misuli
✔️ Mkojo wa njano kwa hatua za awali lakini huja kuwa na rangi mweusi kwa hatua za juu
✔️ Kubadilika rangi kwa kinyesi na kuwa cheupe sana au chenye rangi ya udongo
✔️Macho na ngozi kuwa na rangi ya njano (jaundice)
✔️ Tumbo kujaa maji na kuvimba kwa miguu pamoja na uso
𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨 𝗬𝗔 𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜, 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢 𝗡𝗔 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜:
✔️ Tumia dawa salama za Antivirus za kuuwa virus vya homa ya ini k**a vile 𝗗𝗶𝗿𝗲𝗰𝘁-𝗔𝗰𝘁𝗶𝗻𝗴, 𝗣𝗼𝗹𝘆𝘀𝗮𝗰𝗰𝗵𝗮𝗿𝗶𝗱𝗲𝘀, 𝗧𝗿𝗶𝘁𝗲𝗿𝗽𝗲𝗻𝗼𝗶𝗱𝘀 𝗻𝗮 𝗔𝗻𝘁𝗿𝗼𝗱𝗶𝗮
✔️ Usitumie dawa za maumivu ni hatari unaweza kuongeza ugonjwa
✔️ Usinywe kilevi chochote k**a vile pombe wala kuvuga sigara
✔️ Punguza kutumia vyakula vyenye kupikwa na mafuta mengi k**a vile chips, maandazi au vitumbua
✔️ Punguza msongo wa mawazo, fanya mazoezi na jichanganye kwa marafiki usiwe mpweke
✔️ Kula matunda, mboga za majani, chai ya tangawizi pamoja na supu ya samaki au kuku alie chunwa ngozi
✔️ Fanya vipimo mara kwa mara k**a vile Hepatitis B surface antigen, Liver function test, Viral load, liver ultrasound pamoja na full blood count
✔️ Baada ya kupona hakikisha unachoma chanjo ya homa ya ini hepatitis B kujirinda zaidi
𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:- Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.
𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 +255 0750 969 698