08/09/2025
Mtu anahoji juu ya thamani ya Yanga ya Tsh 100bn😄
Binafsi naamini Yanga wana thamani hiyo au zaidi✍️
Miongoni mwa vitu ambavyo vinaipa thamani timu ya mpira ni pamoja na assets/mali,revenue/mapato,Brand/ Chapa ya klabu n.k.
1. Assets/mali.
Leo Yanga wana ardhi Jangwani yenye “square meter” 37500. Kwa bei ya leo ya ardhi ya kariakoo na maeneo jirani square meter moja ina thamani ya Tsh 1,500,000 ukizidisha bei hiyo x 37500 utagundua ardhi ya Yanga pale jangwani ina thamani ya tsh 56,250,000,000 yes! Ni billion 56.
Yanga wana kiwanja Kigamboni ambacho walipewa na Mh. Makonda,Yanga wana jengo lao jingine,Yanga wana Bus la Wachezaji,Yanga wana kikosi chenye nyota kadhaa mfano thamani ya sasa ya Mzize ni zaidi ya tsh 4bn……hizo zote ni assets za Yanga.
2.revenue/mapato.
✍️Kwenye mapato kuna issue ya jezi,lakini pia 2021 Yanga na Azam walisaini mkataba wa maudhui wenye thamani ya Tsh 41bn kwa miaka 10.
Pia Yanga wanavuna hela Ya Matangazo ya Television kutoka Azam Tv👇
2021-2022.... Million 200(kwa mwezi)
2022-2023.... Million 220(kwa mwezi)
2023-2024.... Million 240(kwa mwezi)
2024-2025.... Million 260(kwa mwezi)
2025-2026.... Million 280(kwa mwezi)
2026-2027... Million 300 (kwa mwezi)
2027-2028.... Million 320(kwa mwezi)
2028-2029.... Million 340(kwa mwezi)
2029-2030... Million 360(kwa mwezi)
2030-2031.... Million 380(kwa mwezi)
✍️Pia Yanga wana mkataba na Sportpesa wenye thamani ya Tsh 21.7bn.
✍️ Yanga wana mkataba na Haier wenye thamani ya 3.3bn.
✍️kupitia kadi za wanachama Yanga kwa mwaka wanaingiza 1.1bn.
3. Brand/Chapa.
Chapa Ya Yanga imetengenezwa kwa muda mrefu pia nyuma Yake kuna mashabiki wengi,ndio maana ukitaka kulipia Tangazo la kukaa kufuani kwa Yanga na Mbao FC Bei ni tofauti…..ule ukubwa wa Yanga na Fanbase yake inaongeza thamani.
Kwa kifupi hapo ukipiga hesabu utagundua Yanga ina thamani zaidi ya Tsh 100bn kwa sasa…..hata Simba wamevuka hiyo 100bn.
Tusijichukulie poa.