20/05/2023
NA VIDONDA VYA TUMBO*
na
MJAMZITO anaweza kupata vidonda vya tumbo kabla au baada ya ujauzito. Umakini unahitajika sana katika kumchunguza mama mjamzito ili kuelewa nini kitakuwa ndiyo chanzo cha vidonda vya tumbo kwake. Mwanamke ambaye ulikuwa unaumwa vidonda vya tumbo hata kabla ya kushika ujauzito unaweza kuendelea kutumia baadhi ya dawa rafiki za kutibu au kuzuia dalili za vidonda vya tumbo hata baada ya kuwa umepata ujauzito.
Kwa kawaida, kila dawa huwa na matokeo ya aina mbili yaani matokeo chanya (uponyaji) na matokeo hasi (uharibifu) na matokeo hasi yanapozidi huweza kusababisha hata kifo. Moja ya matokeo hasi ya matumizi mabaya ya dawa za kutibu vidonda vya tumbo kwa kina mama wajawazito ni pamoja na mtoto kuzaliwa kilema, mtoto kufia tumboni na hata kifo kwa mama.
Wakati wa ujauzito, mama mjamzito anaweza kutokewa na kiungulia mara kwa mara na hata kiasi cha asidi kuongezeka mwilini. Ni wakati huu mwanamke anaweza kuanza kutafuta matibabu kwa ajili ya vidonda vya tumbo na ndipo umakini mkubwa unapohitajika. Hivyo, dawa rafiki, yaani dawa ambazo hazina madhara hasi, ndizo zitumike kwa ajili ya mama mjamzito hasa katika kipindi cha majuma 10 ya kwanza ya ujauzito.
Licha ya kwamba dalili za vidonda vya tumbo hutoweka wakati wa ujauzito kwa wanawake wengi, baadhi ya wanawake hulalamika kuwa na maumivu makali. Hii kwa kawaida hutokea kwa wanawake ambao maumivu ya vidonda vya tumbo yalikuwa makali walipokuwa si wajawazito.
K**a nilivyosema hapo juu, kina mama wengi wanaweza kujihisi wamepona kabisa vidonda vya tumbo wakati wanapata ujauzito au wakati wote wa kipindi cha ujauzito, ingawa baadhi yao hutokewa na maumivu makali hata wakati wa ujauzito, na hii inatokea kwa wale ambao hata kabla ya kupata ujauzito walikuwa wakipatwa na maumivu hayo makali.
Hivyo bado nashauri wakati huu wa ujauzito mama apewe dawa rafiki tu hasa zile zitokanazo na vyakula na mimea hadi hapo atakapojifungua. Wakati huohuo kuwa makini kutokutumia vy