16/06/2021
BAWASIRI ni ugonjwa unaojitokeza katika njia ya haja kubwa, hujitokeza k**a uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa Kiingereza ugonjwa huu huitwa Haemorrhoids au piles.
Bawasiri inaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini lakini unaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji au kwa kutumia dawa mbadala kwa kipindi cha kuanzia wiki sita na kuendelea, inategemea imejijenga kiasi gani
SABABU ZA BAWASIRI
Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kukufanya ukapata ugonjwa huu:
👉Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
👉Ujauzito; wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa.
👉Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
👉Uzee; kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu.
👉Sababu za kurithi; baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni kwa asilimia ndogo.
👉Kuharisha kwa muda mrefu.
👉Kutumia vyoo vya kukaa.
👉Kunyanyua vyuma vizito.
👉Mfadhaiko
👉Uzito na unene kupita kiasi
DALILI ZA BAWASIRI
👉Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
👉kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
👉kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
👉kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
Kwa ushauri
Call/sms/WhatsApp 0657353123