chama cha msalaba mwekundu Tanzania katika mkoa wa Mara kina matawi yafuatayo; Musoma, Bunda, Rorya, Serengeti, Butiama, na Tarime na yote yanafanya kazi chini ya kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu. Katika mkoa wa mara tunatoa elimu ya huduma ya kwanza katika jamii, pia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali mfano, JHPIEGO kwenye mradi wa Afya ya uzazi ya mama na mtoto (MCSP) PACT TANZANIA, TCDC, CARE INTERNATIONAL, PSI (BCC Malaria), Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto mradi wa (MRC) UNICEF (cholera response) tunasaidia jamii katika huduma za afya ,pia kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na yatima. Mbali na hayo tunajaribu kupunguza idadi ya vifo, majeruhi na madhara ya yanayosababishwa na majanga mbalimbali, ajali na magonjwa kwa kutoa elimu na hamasa juu ya huduma ya kwanza na kujikinga na majanga. Tanzanian Red Cross Society in Mara Region is part of the International Red Cross and Crescent Movement. The TRCS Mara consists out of the Branches in Musoma, Bunda and Tarime and all work in the name of International Committee of Red Cross. In Mara Region we give First Aid Classes, take care of health education and join projects concerning the support of most vulnerable children and orphans and other projects that seem to strengthen community health. Moreover we try to reduce the number of deaths, injuries and impact from disasters, accidents and diseases.