07/04/2021
MTIZAMO WA AFYA KATIKA TENDO LA NDOA
Familia yenye furaha inasaidia kufanya mazingira bora na mazuri ambayo yatawasaidia na kuwawezesha watoto wakue na kufanikiwa. Familia ya namna hii imeundwa na kufungwa na vifungo vya upendo na hisia njema kwa wanandoa. Upendo wa kweli katika familia ububujika kutoka katika hali ya wazazi kufurahiana na kuridhikana katika maisha yao ya nyumbani. Katika kupata hali hii ya furaha, ni muhimu kwa wanandoa hao kuwa na hisia zenye afya kabisa katika tendo la ndoa baina yao. Mtizamo wao katika suala hili la tendo la ndoa linatokana na mengi yanayoendelea katika mahusiano yao na mazingira yanayowazunguka. Mahusiano yenye afya na furaha huleta unafuu na kutuepusha na wimbi la msongo na kututua mizigo na misuguano au migongano inayotuelemea kutokana na mbio za kukimbizana na majukumu mbali mbali ya kimaisha katika kutimiza wajibu sehemu zetu za kazi na maeneo mengine yanayotupatia riziki za kila siku. Mahusiano ya aina hii huwajengea heshima na thamani wanandoa , huwaletea maisha mazuri yenye furaha na kuridhikana kwa pamoja.
Ikiwa k**a mume na mke watachukua jukumu kamili na hisia kamili ya ndoa , hakika wanandoa hao watafurahiana na kuelewana kikamilifu. Hakika watajua sababu halisi ya kiasi na kujitawala ambayo hutofautisha mwanadamu na viumbe wengine. Lakini ikiwa k**a wanandoa hao watakosa fikara mathubuti na watakosa kutambua kile kinachowapasa kufanya juu ya ndoa yao , hakika uzoefu wa mapenzi utakuwa k**a pigo kubwa kwao, mathalani kwa wale ambao ni wahoga. Kwakweli matokeo yake huwa ni matokeo yasiyo na furaha , na pengine inaweza pia ikaongeza wimbi kubwa la hofu na uoga.
Lakini mengi hutegemea na jinsi gani marekebisho yanafanywa wakati wa mapumziko ya wanandoa (Honeymoon), kwa sababu hapa ndio wakati sahihi kabisa wa kujenga msingi wa ndoa yenye mafanikio. Ndoa nyingi zinazoshindwa hutokana na kukosa ufahamu wa jukumu lako na kukosa maelezo sahihi na ya msingi katika kujenga ndoa. Baadhi ya wanandoa wachanga walipotoshwa katika maelekezo na mwisho wa siku wanajikuta katika mkondo wa kujuta au kuona wamekosea pindi wanapokumbuka yale mahusiano mengine. Hii itatia doa katika mwenendo na mtazamo mzima wa maisha na kupelekea mkandamizo mkubwa ambao unaweza kupelekea kupoa na kukosa hisia na kutoelewana na mwenza wako. Watu hawa watakuwa na mwenendo wa kinafiki baina yao, na matokeo yake hata ndoa yenyewe itakuwa imepoteza uhalisia wake. Suruhu pekee kwa tatizo hili ni muhimu kabisa kujikubali na kujiamini kikamilifu na kukubaliana na dhana kamili ya maisha mapya.
Ingawa ni kweli kabisa kuna wanandoa wengine wanaishi pamoja wakiwa na fikira na mitizamo tofauti kabisa kuhusu swala la tendo la ndoa, ila hawa katika ujumla wake ni wachache sana katika hali hiyo isiyo ya kawaida. Kwakweli katika hatua hii ndipo hasa ndoa nyingi zinazoshindwa kuendelea huwa zinakwamishwa na kigingi hiki. Madaktari pia wanashauriwa kulikumbuka hili, maana magonjwa mengi makubwa au yanayotesa watu hapa ndipo hasa chimbuko lake.
Maharifa ya kina katika anatomy ya binadamu na fiziolojia itasaidia kutatua baadhi ya haya matatizo yanayotokea kati ya mume na mke. Kila mmoja lazima atambue kwamba tendo la ndoa ni kitu cha msingi na cha kawaida kwa wanandoa katika maisha, k**a vile kupumua, kula au kulala. Katika mazingira sahihi ya tendo hili kusiwepo yoyote wa kusababisha kero kwa mwenzake. Lakini ikumbukwe pia kiasi ni jambo la muhimu, ikiwa k**a kuna yeyote baina ya wenza hawa atahitaji tendo la ndoa kupitiliza viwango vya kawaida kwa mwenza wako vile anavyoweza kustahimili, ikumbukwe inaweza kuwasababishia udhaifu hata ugonjwa katika afya.