03/09/2019
ONGEZEKO LA SUKARI LA KUDUMU KATIKA DAMU.
Baada ya kula chakula kwenye asili ya wanga mwili wako hukivunja kuwa sukari Rahisi(glucose).
°Mwili hutengeneza Homoni ya insulin ambayo husaidia matumizi na uhifadhi wa sukari iliyo katika damu.
°Pale unapokuwa na kisukari mwili wako hauna uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha,ama insulin iliyopo kutotumika vizuri.Hali hii hupelekea wewe kuwa na sukari ya kuzidi katika damu(Hyperglycemia).
SUKARI YA KUZIDI KATIKA DAMU(HYPERGLYCEMIA)
--------------------------------------------------------
Hutokea pale ambapo:-
1.Usipotumia Dawa za kisukari ama kuchoma insulin(Kwa wale walio na kisukari)
2.Pale unapotumia madawa mengine ambayo yanaongeza sukari kwenye damu.K**a vile Corticosteroids na Beta blockers
3.Kula vyakula vingi na vyenye asili ya wanga.
4.Kutofanya mazoezi ya kutosha,ama kutojishughulisha.
5.Kuugua,Kupata ajali au kupata upasuaji.Hii inatokana na kwamba Kwa sababu ya kuugua hutoacha kula japo utaacha kuwajibika.
Hii itakudhuru tu kwa sababu mwili una kanuni ya kubaki kwenye uwiano sahihi "Kiasi kinacho ingia kiwiane na Kiasi kinachotoka.
6.Msongo wa mawazo,mfadhaiko na mashaka.
7.Kubadikika kwa kiwango Cha Homoni (Hasa kwa wanawake)
DALILI ZA ZIDIO LA SUKARI KWENYE DAMU.
°Kiu Kali kupita Kiasi.
°Kukojoa Sana na mara kwa mara.
°Kuhisi uchovu muda wote.
°Kuona maluweluwe.
Usipotatia tatizo la zidio la sukari(Hyperglycemia) inaweza kupelekea kuwa katika hatari ya Kisukari,na matatizo mengine.
Hatua za mwanzo za kuchukua Ni Hizi.
°Kufahamu uwiano wa sukari yako katika usawa
°Unapokuta sukari imezidi ghafla-Kunywa maji ya kutosha.
°K**a una kisukari Fuata taratibu za Matibabu unayoendelea nayo(VIDONGE,Sindano,Dawa asili ?)
°Usiongeze Dawa bila ushauri wa mtoa Huduma wa afya.
°K**a una kisukari angalia sukari yako Kila Baada ya masaa 4 Tangu ilipopanda kwa awamu 3 Mfululizo.
°Fuata kanuni za mlo sahihi was kila siku.
°Ongeza uwajibishaji mwili(Mazoezi)
°Usifanye mazoezi K**a SUKARI yako Ni zaidi ya 11.