22/02/2026
Mgagani au Cleome gynandra ni mboga ya majani k**a zilivo mboga zingine za majani.
Utofauti wa mboga hii ni ladha yake yenye ukakasi na uchungu kwa mbaaali.
Ni moja ya mimea inayotumika k**a mboga yenye virutubisho na wakati mwingine k**a dawa ya asili.
Kwa upande wa virutubisho mboga hii inakadiriwa kuwa na kiwango kikubwa cha madini k**a potassium, chuma, magnesium, calcium, zinc huku vitamini zikiwa ni C, A, K na B9 bila kusahau antioxidants k**a flavonoids, glucosinates, na phenolic compounds.
Uwepo wa virutubisho hivi vinaifanya mboga hii kuusaidia mwili kujenga kinga, uono wa macho, afya ya mifupa pamoja na mmeng'enyo wa chakula, kuondoa sumu mwilini na kuongeza kiwango cha damu mwilini.
Licha ya kuwa na virutubisho vingi lakini pia ni mboga yenye Oxalates na phytates (anti nutrients) kwa wingi ambazo huzuia ufyonzwaji wa virutubisho k**a madini chuma, calcium, magnesium pamoja na zinc.
Njia ya kupunguza anti nutrients kwenye mgagani ni kuchemsha na kumwaga maji ya kwanza japo ni rahisi kupoteza virutubisho vingine hasa vitamin C.
Kwa upande wa dawa ya asili inatumika kupunguza maumivu ya misuli na joint, maumivu ya kichwa, pamoja na maumivu ya tumbo lakini hii tuifanye iwe stori ya siku nyingine.
K**a umeshawahi kutumia mgagani tuambie kwenye comment unafahamu nini kuhusu mgagani??.