03/10/2025
Acid Reflux kwa Kiswahili mara nyingi huitwa kurudi kwa asidi tumboni au kiungulia. Ni hali ambapo juisi yenye asidi kutoka tumboni inapanda juu kuelekea kwenye mrija wa chakula (esophagus).
Dalili za Acid Reflux
Kiungulia (uchungu au moto kifuani, hasa baada ya kula au unapolala).
Hali ya kurudi chakula au maji yenye ladha ya asidi kooni au mdomoni.
Shida ya kumeza chakula.
Kukohoa mara kwa mara bila homa.
Sauti kubadilika / kukwaruza (hoarseness).
Kukosa pumzi au kuhisi kubanwa kifuani.
Sababu za Acid Reflux
Ulaji wa vyakula fulani: vya mafuta mengi, vyakula vya kukaanga, pilipili, vyakula vyenye tindikali (k**a machungwa, nyanya).
Vinywaji: pombe, soda, kahawa, chai yenye kafeini.
Uzito mkubwa/kitambi – huchangia presha tumboni.
Kulala mara moja baada ya kula.
Kuvaa nguo zinazobana tumbo.
Matatizo ya kimsuli: valve (LES – lower esophageal sphincter) kushindwa kufunga vizuri.
Ujauzito kutokana na presha ya mtoto tumboni.
Uvutaji sigara.
Madhara ya Acid Reflux (ikiwa haitatibiwa)
Vidonda kwenye mrija wa chakula (esophagitis).
Mrija wa chakula kukaza (stricture) – husababisha ugumu wa kumeza.
Kuchakaa kwa meno kutokana na asidi.
Kukohoa sugu na matatizo ya koo.
Kansa ya koo / esophagus (kwa hali ya muda mrefu bila kudhibitiwa).
Maisha ya kila siku kuathirika kutokana na maumivu na usumbufu.