07/09/2025
NAEL HAND WASH 500ML
Leo tuangalie :
FAIDA ZA KUNAWA MIKONO KWA KUTUMIA PRODUCT SAHIHI
- Kuua bakteria wanaoweza kusababisha maambukizi kutoka sehemu moja ya mwili kwenda ingine mfano : sehemu ya haja kubwa kwenda mdomoni
- Kuondoa uchafu
- Kuondoa harufu mbaya na mafuta mafuta mikononi kutokana na kushika shika vitu mbali mbali mfano : nyama, samaki, dagaa nk
- Kulainisha mikono yako na kuiweka katika hali nzuri
- Kuacha mikono yako ikiwa na harufu nzuurii sana 🥰
- Inaongeza kujiamini pale utakaposalimiana na watu na kukupa tabasamu muda wote 😘
HASARA ZA KUNAWA MIKONO KWA KUTUMIA PRODUCTS ISIYOKUWA SAHIHI
- Kutokuua vimelea wanaoweza kusababisha maambukizi kutoka sehemu moja kwenda ingine mfano :
Vitu : kutoka kwenye vitasa vya milango,kalamu, mafail nk kwenda mdomoni,
Mwilini : kutoka sehemu ya haja kubwa kwenda mdomoni nk.
Mtu mmoja hadi mwingine : kusalimiana kwa kushikana mikono, kumhudumia mgonjwa nk.
- Kukak**aza mikono : hii ni kutokana na PRODUCT kutokuwa na viambata vinavyofanya kazi ya kulainisha ngozi.
- Kutokujiamini : hii itatokana na baada ya kunawa mikono ikabaki migumu kulingana na aina ya product uliyotumia.
- Kutokuondoa harufu mbaya katika mikono yako mfano : pale unapokuwa umekula aina fulani ya chakula k**a nyama, samaki nk
NI WAKATI GANI UNAWE MIKONO YAKO?
- Wakati unapoamka kabla ya kuanza shughuli yoyote :
kituo cha kwanza kiwe katika Sink lako la kunawia mikono, au unawe kwa maji tiririka, hii ni kutokana na kushika shika sehemu za mwili wako wakati wa usiku kwa kujua / kutokujua mfano : nywele, ngozi ya mwili yenye mafuta na joto la usiku.
- Baada ya kutoka chooni :
:- hii itakusaidia kuondoa bakteria ( enterobius ) wanaoweza kusababisha magonjwa ya tumbo k**a Amoeba.
:- itasaidia pia kuua bakteria ( Escherichia Coli) wanaoweza kupelekea maambukizi katika njia ya mkojo mfano UTI ( Urinary Tract Infection)
- Kabla na baada ya kula chakula, bites au kitu chochote kinachoingia kinywani kwako
- Kabla ya kumbeba / kumhudumia/ kumnyonyesha mtoto wako mchanga / mdogo ( hapa mama unatakiwa uoshe/ usafishe maziwa yako pia )
- Mara baada tu ya kutoka kazini / Katika majukumu / mizunguko yako ya kila siku