30/07/2022
Maumivu ya uti wa mgongo ,ni changamoto ambayo Imekuwa ikiwasumbua watu wa rika tofauti tofauti ,ikitegemea zaidi mfumo wa maisha ya kila siku , Mambo yanayoweza kusababisha hii Hali ni pamoja na:-
1:UMRI, umri umekuwa sababu kubwa inayo sababisha Maumivu ya uti wa mgongo kwa sababu ya kuchoka zaidi kwa mifupa au pingili zinazo Unda uti wa mgongo.
2: KUBEBA MIZIGO, kuna namna bora ya kitaalam jinsi ya kubeba mizigo ,lakini watu wengi hawana elimu juu ya ubebaji sahihi wa mizigo hivyo kupelekea kuumia uti wa mgongo kwa sababu ya ubebaji mbovu wa mizigo
3:KUKAA MDA MREFU,hii huwasumbua Sana watu wanao fanya kazi zao kwa kukaa k**a vile madereva , mafundi ,wasusi, n.k,hii hupelekea mgongo kuanza kuuma kwa sababu ya kukaa Sana.
4:KUTOKUFANYA MAZOEZI, Mazoezi ni jambo mhimu Sana katika Afya ya mwanadamu ,hivyo basi k**a hutojihusisha kufanya mazoezi kuna asilimia kubwa ya kupata shida mbali mbali za kiafya likiwemo la uti wa mgongo.
5: ULEMAVU,Hii huwapa zaidi watu wenye ulemavu k**a vile mguu mmoja kuwa mfupi hii inaweza kusababisha uti wa mgongo kutokupata balansi Hadi kupelekea Maumivu
6: MAGONJWA,Kuna baadhi ya magonjwa yanayoweza kushambulia uti wa mgongo ,k**a vile homa ya uti wa mgongo, TB ya uti wa mgongo, hivyo basi huweza kusababisha Maumivu makali
HONGERA KWA KUJALI AFTA YAKO!! KARIBU
Send a message to learn more