16/05/2023
Njia ya uzazi huanza kutoa majimaji wakati wa balehe. Hii ni hali ya kawaida.
Maji yanayotoka ukeni huwa yamechanganyika na vimelea.
Maji maji haya husaidia kuondoa ngozi ya uke iliyokufa hivyo kufanya uke kuwa katika hali ya usafi na yenye afya.
Iwapo sehemu ya uke inatoa harufu kali au uchafu usiokuwa wa kawaida hali hiyo hutokana maambukizi au magonjwa mengine.
Hapa chini naonyesha aina ya uchafu unaotoka, Maana yake au chanzo chake na dalili ambazo zitatokea kwenye mwili
1⃣ UCHAFU WENYE DAMU AU RANGI YA KAHAWIA
• Hi ni dalili ya mzunguko wa mwezi wa mwanamke uliovurugika na Mara chache ni dalili ya cancer ya servix au aina nyingine ya cancer iitwayo endometrial cancer. Mwanamke mwenye tatizo hili atatoa damu nyingi uken na kuumwa nyonga.
2⃣UCHAFU WA NJANO AU KIJANI WENYE HARUFU MBAYA
• Endapo uchafu ukatoka k**a mapovu,wenye rangi ya kijani au njano ukiambatana na harufu mbaya ,Hi ni dalili ya Trichomoniasis .Maambukizo ya (parasitic) yanayotokana na Ngono zembe.dalili ingine ni kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo.
3⃣ UCHAFU MWEUPE ,WA NJANO AU KIJIVU WENYE HARUFU YA SAMAKI.
• Uchafu wa aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria (vaginosis), P.ID n.k. Mwanamke mwenye tatizo hili atasikia miwasho au maumivu ,kuvimba kwa uke au sehemu ya nje ya uke (v***a)
4⃣ UCHAFU WENYE RANGI YA MAWINGU AU NJANO
• Hi ni dalili ya ugonjwa wa kisonono (Gonerhea) mwanamke atatokwa na damu katikati ya Siku zake, Atatokwa na mkojo bila kukusudia na kupata maumivu ya nyonga.
5⃣ UCHAFU MWEUPE MZITO K**A JIBINI
• Hi ni dalili ya maambukizi ya aina ya fungas (yeast infection)
Na dalili zingine atakazozisikia mwanamke huyu ni kuvimba na maumivu kwenye sehemu za nje za siri (v***a) Kuwashwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.
MUHIMU :Ukiona unatokwa na harufu au uchafu kwa kutoosha sehemu za ndani ya uke , basi ujue una magonjwa ya bacteria au fungus, na unatakiwa umuone daktari kwa hata ili upate ushauri Na tiba 🤝.
Kwa msaada zaidi, Zungumza nami kwa Whatsapp no: 0754477559
Calls:0754477559