02/04/2020
KUHUSU UGONJWA WA HOMA KALI YA MAPAFU INAYO SABABISHWA NA VIRUSI VYA CORONA (COVID-19).
Kwanza tuitambue dhana ya kwanini tunajikinga na kuwa kinga wengine.
Virusi vya corona vinaweza kumuathiri yeyote,lakini watu wenye matatizo ya kiafya na wazee wanadhaniwa kuwa katika hatari ya kuathirika zaidi na dalili zake.
Ikiwa una ugonjwa wa muda mrefu(chronic illness) unaweza kuwa na wasiwasi, hivyo basi huu ndio ushauri wa wataalamu.
Ni nani hasa aliye hatarini?
Kuwa na tatizo la kiafya haikufanyi wewe kuwa mtu anayeweza kupata maambukizi ya coronavirus kuliko mtu mwingine yeyote.
Lakini inaonekana watu wenye umri mkubwa zaidi (wazee), wale ambao mfumo wao wa kinga ya mwili umedhoofika na watu wenye magonjwa ya kudumu ukiwemo moyo, kisukari, au pumu wana hatari zaidi ya kuathiriwa, kwa kiingereza tunaweza sema kwamba, the signs and symptoms of COVID-19 are exacerbated in immuno-compromised patients such as age extreme (elders children) as well as patients with chronic illnesses.
Watu wengi huanza kupona haraka coronavirus baada ya kupumzika kwa siku kadhaa. Kwa baadhi ya watu , inaweza kuwasababishia kuugua sana na wengine hata kutishia maisha yao.
Dalili zake ni sawa na za magonjwa mengine ambayo ni ya kawaida, k**a vile mafua na homa:
kikohozi
joto la juu ya mwili
kushindwa kupumua/kupumua kwa shida
Watu walio katika hatari kubwa ni pamoja na wale wenye umri wa zaidi ya miaka 70, iwe wana ugonjwa wa kudumu au la, na watu wenye chini ya miaka 70 wenye maradhi ya muda mrefu.
Maradhi ya kudumu ya mfumo wa kupumua, k**a vile pumu
Ugonjwa wa moyo wa kudumu k**a vile, kiharusi
Ugonjwa wa kudumu wa figo
Ugonjwa wa kudumu wa ini
Ugonjwa wa kudumu wa neva, k**a Parkinson , na mengine
Seli mundu( sickle cell disease)
Mfumo dhaifu wa kinga ya mwili kutokana na maradhi k**a HIV na Ukimwi, na wakati unapotumia tiba k**a tembe za steroid au tiba ya mionzi
Unapokua na uzito wa mwili wa kupindukia
Wale wenye ujauzito
Kila mtu anaambiwa kufuata hatua za kutosogeleana na mtu mwingine ili kusaidia kupunguza uwezekano wa kuambukizwa na kusambaza coronavirus.
Watu walio katika hatari kubwa wanashauriwa kufuata ushauri huu kikamilifu.
Takriban watu milioni 1.5 wenye matatizo makubwa, k**a vile wagonjwa wanaopokea tiba ya saratani au watu wanaoongezewa kinga ya mwili,wanaombwa kujitenga nyumbani kwa wiki walau 12 ili kujilinda na maambukizi nchini Uingereza.
Mfano,
Mwenye maradhi ya pumu, anapaswa kufanya nini ?
Wagonjwa wa pumu wanashauriwa kutumia inhaler ya kuzuia (ambayo kwa kawaida ina rangi nyekundu ) kila siku k**a walivyoagizwa na daktari. Hii itakusaidia kupunguza hatari ya shambulio la pumu linaloweza kusababishwa na virusi vya aina yoyote vinavyoweza kushambulia mfumo wa kupumua , vikiwemo coronavirus.
Watu walio na maradhi ya pumu wametakiwa kuwa makini kuepuka maambukizi
Tembea na inhaler yako ya rangi ya bluu kila wakati, ili utakaposikia dalili ya shambulio la pumu uitumie mara moja. K**a pumu yako itakuwa mbaya zaidi inaweza kua una coronavirus, na hivyo basi unatakiwa kupiga simu kwenye namba za huduma za tiba ya coronavirus katika nchi yako ili upate ushauri zaidi wa kitaalamu.
Mfano tena,
Mimi ni mzee, je ninapaswa kujitenga binafsi?
Ndiyo,
Kila mtu bila kujali umri -anapaswa sasa kuepuka mikusanyiko au kukaribina na mtu mwingine bila sababu ili kusaidia kuzuia kusambaa kwa virusi na kuwalinda walio katika hatari zaidi ya kupata maambukizi. Hiyo ina maana kwamba epuka kukutana na marafiki na familia pamoja na maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu.
Hii ni muhimu hasa kwa watu wenye umri wa miaka zaidi ya 70 na wale wenye magonjwa ya kudumu kwasababu wako katika hatari kubwa ya kupata dalili mbaya iwapo watapatwa na maambukizi ya coronavirus .
Kuna dhana kwamba mtu asiye mzee wala asiye na ugonjwa wa mda mrefu hapaswi kuwa na hofu ya COVID-19, je ni kweli?
Tafadhari sana,
Tuwe makini na ugonjwa huu,
Unaweza ukadhani kinga yako inaweza kuhimili maambukizi Haya ya corona virus lakini ikawa tofauti kutokana pia na vinasaba.
Lakini vile vile Unaweza ukawa na Haya maambukizi na usioneshe dalili zake kwa kiasi kikubwa, lakini ukawa chanzo cha maambukizi kwa watu walio katika Hatari (susceptible group) Mfano wazee na wenye magonjwa ya kudumu.
Hivyo sote tuchukue tahadhari bila kujali tupo kundi gani kwenye dalili kuwa dhahiri sana au lah!.
Kujilinda kwako ni kumlinda mwenzako na ndivyo unavoilinda jamii na taifa kwa ujumla.