27/09/2025
*Phytotherapist* ni mtaalamu wa afya anayebobea katika kutumia mimea ya dawa (*medicinal plants*) kutibu au kusaidia kuzuia magonjwa. Anafanya kazi chini ya taaluma ya *Phytotherapy*, ambayo ni tiba ya kisayansi inayotumia mimea asilia, tofauti na mitishamba ya jadi isiyo na viwango vya kitaalamu.
Majukumu ya Phytotherapist:
- Kutambua mimea yenye viambata hai vyenye faida kiafya.
- Kuandaa dawa kutoka kwenye mizizi, majani, magome au matunda ya mimea.
- Kuchanganya mimea kwa kipimo sahihi kulingana na ugonjwa.
- Kutoa tiba mbadala au kusaidia tiba za hospitali.
- Kufanya tafiti juu ya usalama na ufanisi wa mimea ya dawa.
Elimu:
Phytotherapist anaweza kuwa na elimu ya:
- *Bachelor/Diploma* ya Phytotherapy, Herbal Medicine, Botany au Pharmacognosy.
- Mafunzo ya maabara juu ya uchambuzi wa kemikali za mimea (phytochemistry).
- Taaluma hii inafundishwa rasmi katika nchi mbalimbali barani Ulaya, Asia na Afrika.
Tofauti na Mganga wa Jadi:
- *Phytotherapist* hutumia mbinu za kisayansi na mara nyingi hushirikiana na madaktari wa kawaida.
- *Mganga wa jadi* hutegemea zaidi mila, imani au urithi wa kifamilia, bila kipimo cha kitaalamu.
DR.HERB
0653796582
Ilham herbal clinic
Medical