27/02/2025
U.T.I (Urinary Tract Infection) ni maambukizi kwenye mfumo wa mkojo. Ili kujikinga na U.T.I, fuata mambo haya:
1. Kunywa maji ya kutosha
Husaidia kusafisha mfumo wa mkojo na kuondoa bakteria wabaya.
2. Usibane mkojo kwa muda mrefu
Kukojoa mara kwa mara husaidia kuondoa bakteria kabla hawajaongezeka.
3. Osha sehemu za siri kwa usahihi
Kwa wanawake, jisafishe kutoka mbele kwenda nyuma ili kuepuka kupeleka bakteria kutoka sehemu ya haja kubwa kwenda kwenye njia ya mkojo.
4. Epuka kutumia sabuni kali kwenye sehemu za siri
Sabuni zenye harufu kali zinaweza kusababisha muwasho na kubadilisha mazingira ya asili ya uke, jambo linalowapa bakteria nafasi ya kuzaliana.
5. Kojoa baada ya tendo la ndoa
Hii husaidia kuondoa bakteria walioweza kuingia kwenye njia ya mkojo wakati wa tendo.
6. Vaa nguo za ndani safi na zinazopitisha hewa
Epuka chupi za nailoni na zisizobadilishwa mara kwa mara, kwani joto na unyevunyevu huongeza hatari ya maambukizi.
7. Tumia tiba ya asili kwa kinga
Juisi ya cranberry au bidhaa zenye probiotics (k**a maziwa mgando) husaidia kuzuia kuzaliana kwa bakteria wabaya.
8. Epuka matumizi ya bidhaa za kemikali ukeni
Douching na manukato kwenye uke vinaweza kuharibu uwiano wa bakteria wa asili na kuongeza hatari ya maambukizi.
Ukiona dalili k**a maumivu wakati wa kukojoa, mkojo wenye harufu kali au rangi isiyo ya kawaida, unahitaji kupata tiba mapema.
https://wa.link/1eczjk